tuanze mwaka vyema

tuanze mwaka vyema

Dr Nickname

New Member
Joined
Dec 28, 2017
Posts
4
Reaction score
3
hello Jf

Ni fursa nyingine tena tumepewa ili tuishi kwa faida hapa duniani, hili ni jema kw Mungu na hata kwa wanadamu. Natambua zinaweza kuweko sababu mbalimbali tunazoweza kujustfy-kwa nini tule sikuu hii sisi pekee yetu na familia zetu. Ila nasikia kukuhamasisha, hebu tuanze mwaka huu vyema, kwa kumshirikisha mema ya nchi jirani yako mhitaji.

Fanya kuwatembelea jirani zako leo, wakumbuke masela pale kitaani pako, agharabu shiriki nao hata soda na sahani ya pilau. Waachie tabasamu lako zuri yatima wale na mjane yule ili wapate cha kumshukuru Mungu kwa maisha haya. Fanya tu hata kama nafsi yako haitoi ushirikiano mzuri, uwezi jua utapanda mbegu gani kwenye ulimwengu wa mwili na roho. lakini uwe na hakika yeye aonaye sirini katu hatoisahau sadaka yako.

Naelewa, masikini wengi hatuna marafiki, ila ni hakika upendo wetu huwa ni wa kweli.
hatuna uwezo wa kukuletea zawadi, ila hakika tunamaanisha tukikwambia wewe ni thamani kwetu.

Natanguliza shukrani zangu kwa watu wangu wa nguvu coz najua wataitikia wito

usiache kunipa mrejesho
 
Back
Top Bottom