Tuanze kupata background ya Mulongo

Tuanze kupata background ya Mulongo

alisababisha mama msemwa aliyekuwa DED BAGAMOYO kufikishwa mahakamani, kwa wasiomjua MULONGO MAGESA kabla yakuwa DC BAGAMOYO alikuwa anafanya kazi TISS

Hajawahi kufanya kazi TISS hiyo akili hana kuingia TISS wakati huo chini ya Mkapa au Mwinyi jamaa kabla hajaingia siasa alikuwa mfanyakazi wa posta akajiunga na umoja wa vijana CCM akawa kambi ya mafisadi ya akina Kikwete mwaka 2005 ndipo alipozawadiwa ukuu wa wilaya. Ila sijui elimu yake mwenye faili la kiwango cha elimu yake atuambie na kutufahamisha

Mulongo is ignorant, arrogant, uninformed, unwise, elusive, evasive and incompetent leader with no quality of leadership. By looking his body language and facial expression when he was giving speech at college compound you will see Mulongo lacks leadership skills and qualities but possess simple mind and low knowleage that cannot govern at such capacity level of regional commissioner except as a ward secretary at his home town.

Mulongo has proven as again that most Tanzania leaders get there through nepotisim, favoritism and cronyism rather than merits, intellect, integrity and professionalism.
 
Alikuwa Buhemba JKT mwaka 1993 oparesheni Miezi Sita akiwa kitengo cha Makisai!
 
Huyu Mulongo nilikua nikimuona Sumbawanga kama meneja TTCL,na mwezi mei mwishoni 2006 raisi JK alifanya ziara mkoani RUkwa kushukuru kwa kura nyingi walizompatia ktk uchaguzi wa 2005,ndipo ghafla alikutana na huyu jamaa na akashangaa kumkuta kule nadhani walikua wanafahamiana vizuri huko nyuma,basi baada ya muda akaaga kuwa amekua DC Bukombe na ndio hadi sasa kawa RC.
 
Kikwete haya mapumbavu huwa anayatoa wapi hivi?
 
Kwani huyu mzee yuko kwenye kambi ya wazee kama kule ughaibuni ambako ukipata nafasi ya kuwaosha masaburi na miguu unajidai kwani una uhakika wa kurudi bongo na mkweche?


Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums

kama kazi anayofanya Chris Lukosi huko London..nasikia hao wazee wanampa likizo mwezi wa sita.
 
Katumwa huyo...
Wabunge wa vyama vya upinzani wa Mkoa wa Arusha wamemtupia lawama Mkuu wa mkoa huo, Magesa Mulongo, kwamba amekuwa akiwatenga kwa kutowashirikisha katika matukio muhimu ya kitaifa yanayofanyika mkoani humo.

Wabunge hao wanadai kuwa miongoni mwa shughuli ambazo Mulongo anawatenga zinahusisha ziara za viongozi wa kitaifa na wa kimataifa.

Kwa nyakati tofauti wabunge hao walisema Mulongo amekuwa kikwazo katika mkoa huo kwani tangu alipoteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha amekuwa akiwashirikisha wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) peke yao katika matukio mbalimbali yanayofanyika mkoani humo huku akiwatenga wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Wabunge hao wa Chadema walitoa mfano wa ziara ya wiki iliyopita ya Waziri Mkuu wa Denmark, Helle Schimidt, aliyoifanya katika wilaya za Arumeru, Arusha Mjini na Monduli kuwa hawakujulisha ujio wa kiongozi huyo licha ya kwamba wao ni wawakilishi halali wa wananchi katika majimbo hayo.

"Mimi nilishasahau kabisa mialiko kutoka ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha kunapokuwa na ziara kama Rais, Waziri Mkuu au kiongozi yeyote kutoka nje, huwa naishia kusikia ving'ora kama wananchi wengine na baada ya kuulizia ndipo naelezwa kuwa kuna kiongozi fulani wa kitaifa," alisema Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema.

Lema alisema kuwa Isdory Shirima alipokuwa Mkuu wa mkoa huo, wabunge wa vyama vya upinzani walikuwa wakipata ushirikiano wa kutoka ofisi ya mkuu wa mkoa, lakini tangu ateuliwe Mulongo kushika wadhifa huo, hawashirikishi kabisa.

"Ujio wa Waziri Mkuu wa Denmark nilikuwa sifahamu, lakini siku hiyo wakati amefika Arusha nilimpigia simu Mkuu wa Mkoa wa Arusha kumuomba ‘appointment' (miadi) ya kuonana naye tujadiliane suala la kufungwa kwa barabara ya Kanisa ambayo imekuwa ikilalamikiwa na wananchi ndipo akanieleza niende uwanja wa ndege nikaonane naye huko kwa sababu alikuwa anamsubiri Waziri Mkuu wa Denmark," alisema Lema.

Waziri Mkuu wa Denmark katika ziara yake mjini Arusha, alitembelea Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR) na Makao Makuu ya Ofisi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).

Akiwa katika Jimbo la Arumeru Mashariki, alitembelea Chuo cha Mafunzo ya Maendeleo na Ushirikiano wa Kimataifa (TCDC) na wakati wa ziara ya Jimbo la Monduli alitembelea Boma la kimasai lililoko katika kijiji cha Nanja.TCDC inaendeshwa kw ushirikiano wa serikali ya Tanzania na Denmark.

Lema alisema siyo kwamba anang'ang'ania kualikwa katika matukio muhimu, lakini serikali ya mkoa wa Arusha lazima itambue kuwa yeye ni mbunge halali ambaye alichaguliwa na maelfu ya wananchi wa Arusha, hivyo ni lazima utaratibu ufuatwe wa kumwalika kama mwakilishi wa wananchi.

Naye Mbunge wa Karatu (Chadema), Mchungaji Israel Natse, alisema hawapewi ushirikiano na ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha pamoja na ofisi za wakuu wa wilaya wakati wao ni wawakilishi wa wananchi kwenye majimbo yao.

"Ushirikishwaji ni dhaifu sana kwa RC (Mkuu wa Mkoa) na DC (Mkuu wa Wilaya), viongozi wa kitaifa wanapofanya ziara katika majimbo yetu hatujulishwi na tukiuliza tunaambiwa hayo ni mambo ya ‘private' (binafsi),"alisema Mchungaji Natse.

Mchungaji Natse alisema pamoja na mkakati wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa na Mkuu wa Wilaya wa kuwatenga katika matukio muhimu, wanashukuru kuwa wananchi katika majimbo yao wanawaamini sana, hivyo mpango huo kama unalenga kutaka kuwadhoofisha kisiasa, kamwe hautafanikiwa. Kwa upande wake Mbunge wa Arumeru Mashariki (Chadema), Joshua Nassari, alisema kama ilivyo kwa wabunge wenzake wa vyama vya upinzania, naye amekuwa akitengwa kwa kutojulishwa na ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha kunapotokea ziara za viongozi wa kitaifa na wa kimataifa.

Baadhi ya matukio ambayo wabunge hao walitengwa ni uzinduzi wa jengo la Makao makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki na Uziduzi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha. Mulongo alipoulizwa na NIPASHE kuhusiana na malalamiko ya wabunge hao, alisema amekuwa akiwapatia taarifa za kushiriki katika shughuli mbalimbali kwa kuwapigia simu na siyo kwa kuwaandikia barua kama wanavyotaka. Mulongo alisema kuwa hata hivyo, wabunge hao wa upinzani licha ya kujulishwa, wamekuwa wakitoa udhuru kwamba hawatahudhuria.

"Wanang'ang'ania niwaandikie barua, mambo hayo yalishapitwa na wakati, mimi kama Mkuu wa Mkoa ninapokupigia simu bado tu huamini unataka mpaka nikuandikie barua, mbunge hata akinisema hainipunguzii chochote kwa sababu kwanza kazi yangu siyo kualika wabunge," alisema Mulongo. Mulongo alisema baadhi ya wabunge wanataka wapewe mialiko kwa barua wakati baadhi yao hawakai hata katika ofisi zao. Hata hivyo, hakuwataka kwa majina.

Alisema cha msingi wabunge washirikiane na serikali kusaidia kuleta maendeleo ya wananchi wa Mkoa wa Arusha na siyo kuzua malumbano ambayo hayana faida kwa wananchi.
SOURCE: NIPASHE
 
Akili na uwezo wa rais utautambua kwa uteuzi wa aina ya watendaji wake sasa hapo ndipo unaona akili ya kikwete.
 
Anasema kazi yake si kualika wabunge, sasa hizo simu huwa anawapigia za nini kama si kazi yake.
Ni mtu mwenye visasi na ubabe ubabe,JK amempeleka pale makusudi kwa nia maalum.Pinda alishawahi kumwonya kwa mambo yake hayo hayo asiyotumia akili wala busara katika utendaji wake,lakini JK bado akampeleka Arusha.
 
alianzia u dc bukombe. kabla ya hapo alikuwa meneja ttcl rukwa.

KAMA KAWAIDA YANGU NITASIMAMIA UTAIFA ZAIDI NA SI UCHAMA. NI KWAMBA HATA KAMA LEMA ANAKOSA KUONGEA NA WANAFUNZI KWA LUGHA ZA KUNDI HILO ILI WAMSIKILIZE ZAIDI PIA NI MOJA YA MBINU YA KUVUTA HISIA ZA KUNDI UNALOONGEA NAO.

MBINU ALIYOITUMIA MAGESA SI YA KIUONGOZI KABISA TENA KATIKA U RC, MAANA KIONGOZI ANATAKIWA AWE NA QUALITY ZIFUATAZO;
  1. MOBILIZATION POWER.
  2. ORGANIZING POWER.
  3. CONTROLING POWER.

SASA NDUGU YETU MAGESA KAKOSA NA HII IMEJIDHILISHA KWA MATUKIO MAKUBWA YAFUATAYO;


  • UKIANGALIA VIDEO ALIPOKUWA AKIONGEA NA WANAFUNZI WA HICHO CHUO CHA UHASIBU ARUSHA.
  • PIA ALIPOWAHI KUMTUKANA MBELE YA HADHARA KIONGOZI WA NGAZI ZA JUU WA JESHI LA POLISI WILAYANI BAGAMOYO WAKATI AKIWA DC, NA ALIMTUKANA MATUSI YA NGUONI NA KUMDHALILISHA OFISA HUYO ETI NI MLA RUSHWA MKUBWA NA AKAMFUKUZA KATIKA MKUTANO. HATA KAMA HUYO OFISA ALIKUWA NI MLA RUSHWA KWA CHEO CHAKE NA PIA NI MTUMISHI WA UMMA KUNA CHOMBO CHA KINIDHAMU KINGEWEZA KUCHUKUA HATUA NA SIO KUTUKANA TENA MBELE YA WANANCHI NA ASKARI WA VYEO VYA CHINI.

HIVYO HUYU KWA KWELI SI KIONGOZI. ILA NI BOSI. ANAFAA KUWA BOSI NA SI KIONGOZI.:angry:
 
alipokuwa DC wa Bukombe aliwahi kumpiga vibao mwandishi wa habari wa gazeti la Nipashe.
 
alipokuwa DC wa Bukombe aliwahi kumpiga vibao mwandishi wa habari wa gazeti la Nipashe.
Nimeunganisha comment zake nimepata picha ya hata tabia zake za utotoni, kumbe JF ni noma hata mie Jodoki mkinitafuta na ID yangu hii ya kichina mtanipata
 
Hana lolote huyu,ni mtu wa kutisha watumishi wenzake, wananchi wa Bukombe wanamjua kwa kukalia siasa za ccm na kuingilia ofis ya mkurugenzi akititafuta pesa za kuchakachua maana ofisi za madc hazipelekewi pesa za maendele na hawana mamlaka nazo.Baada ya Bukombe akahamishiwa Bagamoyo ambako baadae akapewa zawadi ya ukuu wa mkoa baada ya kufanya kazi katika mashamba ya bwana mkubwa.
 
alipokuwa DC wa Bukombe aliwahi kumpiga vibao mwandishi wa habari wa gazeti la Nipashe.
Sasa watu wa aina hii ndio tunatakiwa tujue baada ta ukombozi tuwafanyie nini, au tuwapeleke wapi.
 
Back
Top Bottom