Tuangalie usalama wa mitandao kidogo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tuangalie usalama wa mitandao kidogo

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by Yona F. Maro, Nov 11, 2009.

 1. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #1
  Nov 11, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  Kwa muda sasa baadhi ya antivirus , internet security hata firewalls zimekuwa na programu maalumu ambayo inakuwezesha kutambua kama tovuti au kurasa za mtandao unazotembelea ni haramu au la , kuna nyingine unaweza kuweka setting tu kwamba ifunge moja kwa moja tovuti hizo au ublock kabisa zingine zinakujulisha tu ila unapoingia kwenye tovuti hiyo inakujulisha pia kwamba unaingia tovuti ambayo sio salama .

  Kwa kutambua njia hizi za kampuni zinazotengeneza bidhaa hizo sasa hivi wahalifu wengi wa mtandao wanazotovuti ambazo labda wanaweka habari zinazohusu uhalifu wa mtandao lakini ndani yake mhalifu huyo anatumia njia hiyo kuweza kuchukuwa barua pepe na taarifa zingine za watu wanaoweka malalamiko yao humo mwisho wa siku uhalifu unaendelea kama kawaida .
  Kwenye wimbi la tovuti hizi kuna ambazo zina link na kampuni za kampuni kubwa za kutengeneza programu , zingine ni hizi social media , forums mbalimbali na hata wahalifu hawa kuanzisha kampuni kwenye baadhi ya nchi kwa ajili ya shuguli hizi tu lakini hii inategemeana zaidi na uwingi wa watumiaji wa mitandao katika nchi husika na sheria za nchi hizo kuhusu masuala ya mitandao .

  Katika suala la kuanzisha tovuti , kampuni na kuajiri watu hili limefanyika sana katika nchi za afrika ya magharibi hawa vijana huko Nigeria kwa mfano wanaitwa Yahoo Boys kazi yao ni kutafuta email address na kuwatumia watu kadhaa barua za maombi na aina nyingine ya vivutio vya kibiashara unakuta ni mtu amesajili biashara yake kwa mfano ya internet café hii inafanana na vijana Fulani ambao kazi yao ni kutengeneza account za ovi mail za nokia ndani ya internet café inawezekana wakatumia taarifa hizo kwa uhalifu
  Hapa nchini tukiwahi kuwa na sheria pamoja na usimamizi mzuri matukio kama haya yanaweza yasitokee kwa siku za karibuni au kuibuka kabisa hata hivyo itahitajika pia aina mpya ya leseni haswa kwa watu wanaoendesha huduma za internet café na upigaji simu .

  Ukiacha hii ya kuanzisha tovuti kama hizo kuna wengine pia wanaweka program za bure ambazo wamezicrack kwa ajili ya watu kudownload na kutumia mtu anavyodownload hizi program haoni lolote mpaka pale ambapo anapoextract ili aweze kuinstall kwenye computer ndio unaweza kuona kwamba kuna virus kwenye kitu ulichodownload hata hivyo ni antivirus chache sana zinazoweza kutambua au kuscan ndani ya folder ambalo limekuwa compressed au zipped na kufanikiwa kuondoa virus huyo .

  Kama sio virus kuna weza kuwa na programu ambazo zinauwezo wa kurekodi kazi za keyboard yako , mouse na hata tovuti unazotembelea kisha kumtumia mhalifu popote alipo kwa sababu programu hiyo inakuwa imetengenezwa kwa shuguli hizo .

  Kwahiyo unaona wakati njia nyingi zaidi zinabuniwa kulinda watumiaji wa computer na mitandao , wahalifu nao wanaendelea kuwa na njia nyingi na tofauti kuweza kupata taarifa ambazo zinaweza kuwawezesha kuharibu computer au kuweza kuchukuwa taarifa za mteja Fulani kwa ajiliya kufanyia uhalifu sehemu zingine .

  Kwa kumalizia ni vizuri watu wachukuwe tahadhari zaidi kuhusu matishio mapya yanayojitokeza kila mara kwa ajili ya ulinzi wa mali zao wanapokuwa kwenye mitandao , kwenye upande wa makazini ni vizuri wawe na Sheria zao zinazowaongoza katika matumizi ya vifaa vya mawasiliano na kwa upande wa kampuni zinazotengeneza programu tofauti ni vizuri wafikirie jinsi wanavyoweza kupunguza bei ya programu zao kwa jamii za watu wa kipato cha chini ili waweze kununua programu hizo .

  Na wengine kama sisi tunaofanya kazi kwenye mazingira ya vitu kama hivi tujenge mazoea ya kuibua mada mbalimbali na kujadili haswa kwa lugha ya Kiswahili ili kuwezesha watu wengi zaidi kujua kinachoendelea , kujifunza na hata kuuliza au na wenyewe kushiriki mijadala hii .

  Yona F Maro
  www.wanabidii.net
  www.naombakazi.com
  www.askmaro.blogspot.com
  THINK GLOBAL – ACT LOCAL
   
Loading...