Yona F. Maro
R I P
- Nov 2, 2006
- 4,202
- 218
Kila siku inavyozidi ndio Mtandao unazidi kuwa mkubwa zaidi , ndio tovuti zinazidi kuongezeka na maudhui kwenye mtandao yanazidi kuongezeka na programu za kuendesha maudhui na masuala mengine kwenye mtandao zinazidi kuongezeka na kuwa bora zaidi .
Watu wengi duniani wanazidi kuongeza vitu kwa njia ya mtandao kwa ajili ya biashara , kusomwa na kufurahia hivi vitu vinavyoingizwa kwenye mtandao na kuuboresha zaidi kwa ajili ya kusoma yaani content /maudhui vinaweza kuwa biashara kubwa na nzuri kwa baadhi ya watu duniani .
Kuna watu wengi sana duniani kote wanaanzisha tovuti , blogu na shuguli kadhaa kwa njia ya mtandao lakini wanakosa content/maudhui ya kuweka kwenye mitandao yao ili iweze kusomeka au kutembelewa na watu wanavyotafuta kitu Fulani kwa njia ya mtandao .
Matokeo ya kukosa maudhui ni kushuka viwango vya watembeleaji wa tovuti husika au kupoteza mwelekeo wa taarifa Fulani inayofuatiliwa kwenye mtandao lakini vile vile kukosesha mapato kwa baadhi ya kampuni na watu binafsi waliotengeneza kurasa hivi kwa nia ya kujitengenezea kipato kwa njia ya matangazo .
Content au maudhui kwenye tovuti nyingi za kitanzania imekuwa mbaya na isiyoleta tija kwa watazamani wengi matokeo yake ni kwa wengi kwenda tovuti au blogu za picha pekee na inahusiana na utamaduni wa watanzania wengi wa kusoma hata kitu kidogo
.
Hii ni fursa Adimu sana ambayo wenye blogu , tovuti na wale wanaotaka kuanzisha blogu zao wanaweza kuitumia kujitengenezea kipato na kuajiri watu wengi kwa ajili ya kuwaandalia maudhui ya tovuti au blogu zao ziweze kupata wasomaji wengi kwa kipindi kifupi na iwe hivyo endelevu .
CHANGAMOTO ZILIZOPO
Kwa nchi ya Tanzania hatuna chombo maalumu kinachosimamia maudhui kwenye mitandao ya kitanzania matokeo yake ni watu kuibiana kazi na wale wenye kazi zao zilizopo kwenye mtandao kukosa haki nazo , kuna nchi kadhaa zinazodhibiti maudhui kama uchina ,iran na jimbo la Kaduna nchini Nigeria .
Kuna tatizo la lugha kwenye mitandao mingi hili linaonekana halishtui watu hata pale unapokutana na mtandao unaoweza kuuamini sana napo watu wengi wanaweza kuwa hawaandiki lugha sanifu .
Watanzania haswa wadau wa sekta ya teknohama na serikali yao wanatakiwa watambue kazi ya kujenga maudhui kwenye mtandao ni yao tena kwa lugha ya Kiswahili , hii sio kazi ya google au yahoo ni yao bila wao hawataweza kuendelea vizuri kwenye sekta hii .
Maudhui imara na bora ni yale yaliyoandaliwa kwa lugha za kinyumbani kama Kiswahili , kichina na haya ndio ambayo yanaweza kuchujwa na kutengenezwa vizuri kwa ajili ya kizazi kijacho .