Tuandamane dhidi ya mgomo wa Madaktari | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tuandamane dhidi ya mgomo wa Madaktari

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Samsindima, Mar 9, 2012.

 1. S

  Samsindima Member

  #1
  Mar 9, 2012
  Joined: Jan 18, 2012
  Messages: 37
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Inasikitisha kuona Madaktari ambao ni watoto wa nchi hii wameamua kuzama kwenye malumbano dhidi ya serikali ambapo waathirika ni sisi wananchi tunaotegemea huduma yao. Sikujua kwamba Daktari amalizapo shahada yake analipwa zaidi ya milioni 1 na wahitimu wa shahada nyingine wanapata nusu yakiwango hicho. Sikujua pia kwamba wanapokuwa masomoni wanapata asilimia 100 ya fedha ya mkopo ambayo sina uhakika kama ni exempted. Leo hii wanadai maslahi zaidi sio kitu kibaya kulinganisha na uzito wa kazi yao. Lakini
  kututelekeza tufe kwa vile hawamtaki Waziri au Naibu wake ni kutokututendea haki. Ninavyojua watu hao 2 si watendaji na uwepo au kutokuwepo kwao hakuathiri shughuli zao madaktari hasa baada ya kujua unyeti wa tatizo lenyewe. Nawashauri waaache kuendeleza mgomo wao la sivyo tutaanzisha kampeni dhidi yao nchi nzima wasije juta. Maafa ya mgomo wa awali tumeyapata sidhani kama kuna anayependa yajirudie.
   
 2. Nyetk

  Nyetk JF-Expert Member

  #2
  Mar 9, 2012
  Joined: Feb 28, 2012
  Messages: 1,624
  Likes Received: 819
  Trophy Points: 280


  SAMSINDIMA, Hayo maneno mekundu yasingekuwepo na badala yake yawepo maneno hayo ya kijani, ningekuunga mkono!


  MADAKTARI WANAOGOMA HAWATUFAI KWA LOLOTE NA TUPO MBIONI KUWAFUTA KTK HISTORIA!
  MINDLESS TERRORISTS!
   
 3. M

  MJM JF-Expert Member

  #3
  Mar 9, 2012
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 461
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Serikali kukumbatia watu wawili tu kwa maafa ya nchi nzima ndiyo unaiona Sikivu, Inayowajali wananchi? Saa ya ukombozi mbona mnaisogeza mbali sana? Madudu yote yaliyofanywa ndani ya wizara hiyo na kugharimu maisha ya watanzania tulitegemea wenyewe tu wawajibike na kushindwa kuwajibika kwao walitakiwa kuwekwa pembeni ili mambo yaende. Bora wawili hawa waondoke ili mambo yasonge mbele na kama wanawapenda sana wawatafutie ulaji mwingine kama walivyozoea.

  Hatutakiwi kuwashambulia madaktari katika hili bali serikali. Kama walikubali kutekeleza hilo katika kikao cha muafaka sasa wanakataa nini? Serikali kutafuna maneno yake yenyewe siyo kosa kubwa? Nadhani kwa sababu hawa wawili ni muhimu sana tulitakiwa kwenda juu zaidi kwa serikali nzima kuwajibishwa kwa manufaa ya umma.

  Sisi tunaoumia tutakaa kimya na kuwashambulia madaktari kumbe serikali inahitaji kupumzishwa, imechoka na haijui inakoelekea kama mmefanya tathmini ya kina. Yetu macho na masikio wakati tukisubiri "mchiriku wa wazee wa CCM jioni"
   
Loading...