Samsindima
Member
- Jan 18, 2012
- 37
- 0
Inasikitisha kuona Madaktari ambao ni watoto wa nchi hii wameamua kuzama kwenye malumbano dhidi ya serikali ambapo waathirika ni sisi wananchi tunaotegemea huduma yao. Sikujua kwamba Daktari amalizapo shahada yake analipwa zaidi ya milioni 1 na wahitimu wa shahada nyingine wanapata nusu yakiwango hicho. Sikujua pia kwamba wanapokuwa masomoni wanapata asilimia 100 ya fedha ya mkopo ambayo sina uhakika kama ni exempted. Leo hii wanadai maslahi zaidi sio kitu kibaya kulinganisha na uzito wa kazi yao. Lakini
kututelekeza tufe kwa vile hawamtaki Waziri au Naibu wake ni kutokututendea haki. Ninavyojua watu hao 2 si watendaji na uwepo au kutokuwepo kwao hakuathiri shughuli zao madaktari hasa baada ya kujua unyeti wa tatizo lenyewe. Nawashauri waaache kuendeleza mgomo wao la sivyo tutaanzisha kampeni dhidi yao nchi nzima wasije juta. Maafa ya mgomo wa awali tumeyapata sidhani kama kuna anayependa yajirudie.