Tuachieni Nyerere Wetu

Tuachieni Nyerere Wetu

Companero

Platinum Member
Joined
Jul 12, 2008
Posts
5,609
Reaction score
1,731
UDADISI: Rethinking in Action: TUACHIENI NYERERE WETU


MMETUPORA KILA KILICHO CHETU, TUACHIENI NYERERE WETU


Na Mwl. Sabatho Nyamsenda


Wanyonge walia, waporaji washerehekea
Siku ya leo nchi yetu inaadhimisha miaka 14 tangu kuondokewa na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Hivyo, leo ni siku ya furaha na huzuni; ni siku ya harusi na matanga. Kwa waporaji, wanyonyaji, wabaguzi wa rangi, wadini na wakabila, leo ni siku ya kunywa mvinyo na kusherehekea. Ule mwiba uliowachoma siku zote na kuwakosesha raha hatimaye uliondoka siku kama ya leo, nao wakapata nafasi ya kutamba.


Kwa wanyonge – wakulima wadogo, wafugaji wadogo, warina asali, waokota makopo, wafagia barabara, wabeba zege, machinga, mama ntiliye, wafanyakazi wa ngazi za chini, na wote wanaoishi katika dhiki na kukosa huduma bora za afya, maji, elimu na malazi – leo ni siku ya huzuni. Lile jabali lililoongoza mapambano yao hatimaye lilistaafu rasmi kazi ya kupambana siku kama ya leo. Nyerere, msemaji wa wanyonge, akaacha kusema. Kambarage, mshairi wa makabwela, akaacha rasmi utunzi wa mashairi. Julius, mfasiri wa vitabu, akaweka kalamu chini huku akiwa amekamilisha kutafsiri kwa Kiswahili kitabu cha mwanafalsafa wa Kiyunani, Plato, kiitwacho ‘‘The Republic’’. Mwalimu wa wanyonge akakoma kufundisha. Akatulia tuli. Akalala usingizi wa kudumu.


Tufurahie maisha yake kuliko kuomboleza kifo chake
Je, ni sahihi kwa wanyonge kulia? Ni haki kwa wanyonge kuomboleza? Kulia na kuomboleza ni haki ya kila ampotezae mpendwa wake. Lakini kwa kuwa Nyerere alikuwa binadamu wa kawaida na sio malaika aliyeshushwa toka angani hatukutegemea kwamba ataishi milele. Binadamu huzaliwa, hukua, huzeeka, huugua, hufariki. Ndicho kilichotokea kwa Mwalimu. Pengine siku ya leo yapaswa kuwa siku ya kufurahia maisha ya Mwalimu kuliko kuhuzunikia kifo chake. Kwa maana hiyo, siku kama ya leo twapaswa kuzitafakari kwa kina fikra zake na jinsi tutakavyozitumia kuendeleza mapambano ya wanyonge.

Nyerere hajafa, sisi ndio Nyerere
Aina hii ya kumwenzi kiongozi wa mapambano kwa kuendeleza yale aliyoyapigania niliiona kwa Wavenezuela walipoondokewa na shujaa wao wa mapinduzi ya kidemokrasia, rais wa wanyonge, Hugo Chavez, alipofariki mwezi machi mwaka huu. Nilipowaona katika televisheni mamilioni ya wanyonge wa Venezuela wakitiririkwa na machozi, nilidhani huo ndio mwisho wa mapinduzi ya kijamaa ya kibolivari (The Bolivarian Socialist Revolution) waliyoyaasisi wanyonge wa nchi hiyo wakiongozwa Chavez.


Kilichonitisha zaidi ni jinsi viongozi wa mataifa ya mabeberu, na hasa Barack Obama wa Marekani, walivyotoa kauli za kusherehekea kifo cha gwiji hilo la mapambano. Na mabeberu walikuwa na haki kushangilia kifo hicho kwani ni Chavez aliyehakikisha kuwa utajiri wa mafuta ya nchi hiyo unaenda kuwafaidisha wanyonge kwa kuwapatia hudumu bora za kijamii zisizo na malipo. Mawakala wa ubeberu nchini Venezuela wakisaidiwa na majasusi wa Marekani walijaribu kumpindua Chavez lakini mamilioni ya wanyonge waliandamana hadi aliporejeshwa madarakani.
Lakini kauli za wanyonge wa Venezuela zilinipa matumaini: pamoja na kutiririkwa machozi, walipohojiwa na waandishi wa nchi za Magharibi juu ya kifo cha kiongozi wao, walijibu: ‘‘Chavez hajafa. Sisi ndio Chavez’’. Kwa kauli hiyo wanyonge walikula yamini kuendeleza mapinduzi ya kijamaa na kuhakikisha kuwa utajiri wa nchi yao unaendelea kuwafaidisha wanyonge badala ya kikundi kidogo cha mawakala wa mabeberu na mabwana wao.
Tena wanyonge wa Venezuela wameonyesha mshikamano wa kitabaka na wanyonge wa nchi nyingine kama Cuba, Ecuador, Nicaragua na Bolivia ambazo zote zinaongozwa na serikali za kijamaa. Mathalani, Cuba yenye madaktari wengi waliobobea huwapeleka Venezuela ili kutoa huduma za afya kwa wanyonge mijini na vijijini, wakati Venezuela ikiipatia Cuba mafuta kwa bei rahisi na kuisaidia kiuchumi ili iondokane na hali ngumu inayosababishwa na vikwazo vya Marekani.


Kambarage mpinga unyanyasaji
Historia ya Kambarage inaonyesha kuwa tangu akiwa mdogo alichukia kila aina ya uonevu, ubaguzi, unyanyasaji na ukandamizaji. Akiwa mtoto mdogo, Kambarage alikuwa akimsindikiza mama yake shambani ; mama akiwa analima, Kambarage alikuwa akimbembeleza mdogo wake. Huruma ilikiwa ikimwingia Kambarage kumwona mama yake akifanya kazi za suluba siku nzima bila kupumzika. Hivyo akabuni mbinu ya kumpumzisha mama yake. Akawa anamfinya mdogo wake, na kitoto kile kichanga kikawa kikitoa kilio kikali, kilio kilichomfanya mama adhani kuwa kichanga yule ana njaa. Hivyo, mama akaacha kulima na kuja kumnyonyesha mwanawe. Kamnyonyesha mtoto, lakini pia kapumzika. Kambarage alitabasamu na kujiona mshindi, hata kama ushindi wenyewe ulikuwa wa muda mfupi tu.

Miaka mingi sana baadaye kitoto hiki, ki-Kambarage, sasa akiwa kijana wa umri wa miaka 22 na mwanafunzi wa Makerere aliandika insha ya kiswahili iliyoitwa ‘‘Uhuru wa Wanawake’’. Ndani ya insha hiyo kijana Julius aliichambua na kuilaani mifumo ya jamii zetu za Kiafrika iliyokuwa ikiwakandamiza na kuwanyanyasa wanawake kana kwamba wao si binadamu kamili. Na ni mfumo wa kikoloni ulichochea moto na kuhalalisha mfumo dume.


Insha hiyo, ambayo ambayo ilishinda tuzo ya Kamati ya Lugha ya Afrika Mashariki kwa wakati huo, na sasa imechapwa katika kitabu, inaishia na kisa cha kifaranga cha tai kilichochanganywa na kuku, kikalishwa chakula cha kuku, hata chenyewe kudhani ni kuku. Lakini tai huyo alipopelekwa kilimani na mtaalamu wa wanyama, na kuambiwa: tai, wewe sio kuku, kwako ni angani, hivyo ruka uende angani. Tai akaruka na kupotelea mawinguni. Kwa kutumia mfano huo, Nyerere akawataka wanawake kutokubali madhila ya mfumo kandamizi unaowaaminisha kuwa wao ni kuku, warukia chini, ilhali wao ni tai, warukia juu. Hivyo walipaswa kuruka na kupaa.


Hata hivyo mtazamo wa Mwalimu haukuwa finyu kwa kudhani kuwa ni wanawake pekee ndio waliokandamizwa na kunyimwa fursa. Mfumo wa kibepari, ambao kwa wakati huo ulichukua sura ya ukoloni, uliwakandamiza wanyonge wote, wake kwa waume, katika Afrika na mabara mengine. Hivyo, wanyonge wote walipaswa kupambana na kuushinda ukoloni. Ndio maana Nyerere alikuwa mbele kuongoza mapambano dhidi ya ukoloni, ubaguzi wa rangi na ukandamizaji, katika Afrika na dunia nzima kwa ujumla.

Julius asiyenunulika
Shuleni Tabora, Julius alipewa ukiranja. Hii ilitokea baada ya yeye kuamua kuacha shule kutokana na kunyamazishwa na mwalimu mkuu wakati wa mdahalo. Kambarage alikuwa ametoa hoja za kupinga uonevu na unyonyaji wa serikali ya kikoloni hali iliyomwudhi mwalimu mkuu wa kizungu na kumwamuru akae chini. Kwa nini anyamazishwe? Mwanafunzi huyo aliamua kufunga virago vyake na kurudi kwao lakini utawala wa shule kwa kushirikiana na serikali ya kikoloni walimkatiza na kumrudisha shuleni kisha wakampatia uongozi.
Kama walimu wa kikoloni walidhani kwa kumpa ukiranja walikuwa wamemnunua Julius basi walikuwa wakiota ndoto mchana kweupe. Ukiranja wa shule ulimpa Kambarage haki ya kupata nusu lita ya maziwa kila siku, ilhali wasio viranja walipata robo lita. Ni Kambarage, si mwingine, aliyeongoza mgomo wa wanafunzi kupinga ubaguzi huo na kudai wanafunzi wote wapate mgao sawa wa maziwa. Mgao huwa wa kibaguzi ukakoma. Tayari Nyerere alishaanza kupigania usawa.


Miongo kadhaa baadae serikali ya kikoloni ilimpatia ujumbe wa Baraza la Kutunga Sheria la Tanganyika (ubunge kwa wakati huo). Walidhani wamemnunua na kumnyamazisha. Lakini alipoona hoja zake hazipewi nafasi Nyerere alijiuzulu ubunge huo na kuyarejea maisha yake ya dhiki aliyokuwa akiishi baada ya kuacha kazi ya ualimu. Alikataa kuwasaliti wanyonge.


Kipo kisa katika kitabu cha Mohamed Said kiitwacho Uamuzi wa Busara wa Tabora kinachoonyesha maisha aliyoishi Nyerere baada ya kuacha kazi ya ualimu iliyokuwa na mshahara mnono kwa wakati huo ili kuongoza mapambano ya uhuru. Familia yake ikakosa hata mlo wa kueleweka. Siku moja, akiwa hana hata senti moja mfukoni, Mwalimu aliamua kutembea kwa mguu toka nyumbani kwake Magomeni hadi Kariakoo, akitegemea huenda atabahatisha kupata chakula. Njiani akakutana na mzee Msume Kiate, mwana TANU ambaye alikuwa akifanya biashara ya kuuza samaki. Baada ya kusikiliza shida ya Mwalimu, mzee Kiate akampatia shilingi mia mbili akanunue mahitaji yake. Na baada ya hapo mzee Kiate na wana TANU wenzake walijitolea kuihudumia familia ya Mwalimu kwa chakula na wakaendelea kufanya hivyo hata baada ya uhuru kupatikana. Tunapomkumbuka Nyerere tunapaswa pia kuwakumbuka mashujaa wengine, kama Mshume Kiate, ambao vitabu vingi vya historia havitaji majina yao.

Mwalimu Nyerere, kiongozi wa makabwela
Kitabaka, Mwalimu hakuwa katika kundi la makabwela. Kwa kuzaliwa katika familia ya kichifu tayari alikuwa na fursa ambazo watoto wengine hawakuwa nazo. Moja ya fursa hizo ilikuwa elimu. Lakini elimu ikamfungua na kuiona dunia. Kadiri ilivyomfungua ndivyo ilivyomtenganisha na watu wake. Toka Butiama akaenda Musoma, toka Musoma akapita Mwanza, Shinyanga hadi Tabora. Akavuka mipaka ya kijiji na mikoa. Akavuka mipaka ya nchi, akaenda Uganda. Akavuka mipaka ya bara, akaenda Uingereza. Elimu yake haikumvusha mipaka ya ramani tu bali mipaka ya kitabaka. Kadiri alivyoongeza vidato na shahada ndivyo alivyolihama tabaka la “walalahoi”.


Lakini japokuwa kitabaka alikuwa katika “walalahai” kabla ya uhuru, na kuhamia katika “walalaheri” baada ya uhuru, Mwalimu mwenyewe aliamua kwa makusudi kabisa kuliasi tabaka lake. Hivyo usomi wake haukuwa na bei (exchange value) bali ulikuwa na thamani (use value). Katika fikra za Mwalimu, msomi anayejitapa kuwa yeye hawezi kutumika kwa wanyonge mpaka alipwe kiasi fulani cha fedha huyo si binadamu kamili bali ni mtumwa. Binadamu pekee mwenye bei na anayeuzika sokoni ni mtumwa.


Ndio maana hata baada ya kutoka Uingereza, akiwa Mtanganyika wa kwanza kupata shahada ya umahiri (master’s degree), Mwalimu hakuhangaika kutafuta fursa za kujitajirisha na kuishi maisha ya anasa. Kwa kuwa maslahi hayo ya kitabaka alishayaaga haikuwa vigumu kwake kuachia nyadhifa zenye malipo manono ili akawapiganie wanyonge.
Hata baada ya kukaa Ikulu kwa zaidi ya miaka 20, alifanikiwa kujenga kajumba kadogo na ka kawaida kabisa kijijini Butiama, na nyumba yake ya Msasani aliijenga kwa mkopo ambao hata hivyo alishindwa kuumalizia, na kuiomba serikali imalizie mkopo na kuchukua nyumba hiyo. Serikali ya Mwinyi ikafanya hivyo lakini ikampatia Mwalimu nyumba hiyo. Mwaka 1966 Mwalimu alikata mshahara wake kwa asilimia 20. Wakati huo alikuwa akipokea shilingi 5,000/=, hivyo akabakia na shilingi 4,000/= na hakuwahi kujiongezea mshahara mpaka anaondoka madarakani. Hivyo, wapo watumishi wengi kabisa wa serikali, wakiwemo maprofesa, waliopokea mshahara mkubwa kumzidi.


Azimio liliwajali wanyonge
Lakini kutopenda mali inaweza kuwa hulka ya mtu yeyote kabisa. Mkristo au mwislamu mzuri, anayeamini katika pepo ya baadae, hawezi kujikita katika anasa za kidunia. Ila Nyerere alifanya hivyo si kwa sababu ya ukristo wake, ila kwa sababu ya itikadi iliyomwongoza, itikadi ya kijamaa. Ndiyo maana, baada ya kuwaona viongozi wenzake wanatumia nyadhifa zao kujitajirisha, aliasisi Azimio la Arusha, ambalo pamoja na mambo mengine liliwazuia viongozi kumiliki nyumba za kupangisha, kupokea mishahara miwili au zaidi na kumiliki hisa au kuwa wakurugenzi katika kampuni za kibepari.


Kupitia Azimio la Arusha, njia kuu za uzalishaji-mali na rasilimali za taifa, kama viwanda, mabenki, misitu, madini, ardhi, njia na vyombo vya usafiri wa anga, reli na maji, viliwekwa mikononi mwa umma. Umma wa wanyonge ulichagua serikali kwa njia ya kidemokrasia, serikali ambayo ilipewa jukumu la kusimamia rasilimali hizo kwa niaba ya wanyonge. Faida inayozalishwa ilitakiwa kwenda kuwahudumia wanyonge, na sio kikundi cha watawala. Azimio lilisisitiza juu ya kuwajali wakulima vijijini, na kuonya juu ya misaada kutoka ughaibuni.


Azimio likahujumiwa na kupinduliwa
Kama inavyofahamika, wanyonge, wake kwa waume, vijana kwa wazee, waliandamana nchi nzima kuunga mkono Azimio la Arusha. Lilikuwa ramani yao kuelekea nchi ya usawa na matumaini. Lakini hata hivyo, utekelezaji wa Azimio uliwekwa mikononi mwa watu walewale walioanza kujitajirisha. Japo katika miaka ya 1970 sera za kijamaa zilifanya vema na serikali ikaanza kuonyesha mafanikio katika kutoa hudumu bora kwa jamii bila malipo, hali ilibadilika katika kipindi cha miaka ya 1980.


Nchi za kibeberu, Marekani na Uingereza, zilishikwa na waumini wa sera za uliberali mambo-leo na hivyo kuzilazimisha nchi maskini kufuata sera hizo kwa kubinafsisha kila kilichotaifishwa, kufuta ruzuku katika kilimo na vyakula, na kuacha mara moja kutoa huduma zisizo na malipo. Ndani ya nchi, tena Mwalimu akiwa bado madarakani, sera hizi zilipata mashabiki wengi. Wachache walijionyesha waziwazi. Wengi walijificha na kuendelea kuhujumu chini chini.


Nchi ikiwa imetoka vitani, bidhaa za msingi zikawa hazipatikani. Zilikuwa zimehodhiwa na kikundi cha watu wachache, baadhi wakiwa katika dola na baadhi nje ya dola. Hivyo, baada ya vita vya Uganda, Mwalimu alikuwa na vita viwili vya kupigana: vita dhidi ya wahujumu uchumi/ujamaa ndani ya nchi, na vita dhidi ya mabeberu nje ya nchi. Makundi hayo yalikuwa yakishirikiana kwa ukaribu sana, na hata yakafanikiwa kuupindua Ujamaa baada ya Mwalimu kung’atuka.


Sera za kiporaji
Uzoefu wa zaidi ya miaka 25 ya utekelezaji wa sera za uliberali mambo-leo umetuonyesha kuwa mfumo huu ni katili zaidi pengine kuliko hata biashara ya utumwa na ukoloni. Rasilimali za wanyonge zinaporwa, na wanyonge wanapojaribu kupinga hutumiwa majeshi na serikali zao au za mabeberu. Tumeyaona hayo nchini mwetu. Pia tumeyaona barani kwetu na duniani kote mifano ikiwa ni uvamizi wa Libya na Iraq uliopelekea kuchinjwa kwa viongozi wa nchi hizo, na mamilioni ya wanyonge kuuawa.


Akihutubia mjini Mbeya katika sherehe za Mei Mosi mwaka 1995, Mwalimu aliziita sera za ubinafsishaji na uwekezaji kuwa ni za kinyang’anyi. Akasema kuwa zitazalisha mabilionea, lakini watakuwa wachache. Lakini pia zitazalisha maskini, na hao watakuwa wengi sana. Hayo ndiyo yatokeayo nchini mwetu na duniani kote.

Jengeni sanamu zake, sisi tutazienzi fikra zake
Mwaka mmoja kabla ya kufariki Mwalimu alikuwa ametabiri kuwa ipo siku Tanzania itarejea katika misingi ya Azimio la Arusha. Katika Kongamano la kuadhimisha miaka 44 ya Azimio la Arusha, Profesa Issa Shivji naye pia alisisitiza juu ya uwepo wa dalili zinazoonyesha kuwa Watanzania walio wengi wameanza kupigania kurudi katika misingi ya Azimio la Arusha lakini akaonya kuwa dalili hizo zinaweza kuzimwa na kakundi ka watu wachache kanakofaidika na mfumo uliopo.


Nafikiri kuwa miongoni mwa mbinu za kuzima dalili hizo ni kuhodhi jina la Mwalimu huku wakijidai wanamuenzi. Eti wanamuenzi kwa kuongeza idadi ya sanamu zake, na taasisi na viwanja vyenye jina lake ilhali Mwalimu mwenyewe alishakataa hayo tangu akiwa hai. Wakijidai kugusia fikra zake basi wanamhubiri kama mpenda amani na umoja. Lakini ni Mwalimu mwenyewe aliyesema kuwa mahali pasipo na haki (justice) wala usawa (equity) hapawezi kuwa na amani. Pia hauwezi kuwa na umoja kati ya wanyonyaji/waporaji wachache na mafukara wengi.
Ili nisionekane nabandika maneno katika mdomo wa Mwalimu, nitanukuu sehemu ya hotuba yake aliyoitoa mwezi mei mwaka 1989 wakati akifungua semina ya wazalishaji wakubwa iliyoandaliwa na Chama cha Mapinduzi:


“Si kwamba Azimio la Arusha limeondoa umaskini hata kidogo, wala halikutoa ahadi hiyo. Azimio la Arusha limetoa ahadi ya matumaini. Ya haki, ahadi ya matumaini kwa wengi, ndio watu wengi wa Tanzania wanaendelea na kuwa na matumaini hayo. Madhali yapo matumaini hayo, mtaendelea kuwa na amani… Kama wengi hawana matumaini, tunajenga ‘volcano’. Siku moja italipuka na lazima ilipuke. Isipokuwa watu hao wajinga. Wengi wa nchi hiyo wajinga, wanakubali kutawaliwa hivi hivi. Kuonewa hivi hivi na wingi wanao, wajinga hao. Kwa hiyo, Watanzania hawa watakuwa wajinga, wapumbavu, kama wataendelea kukubali kuonewa na watu wachache katika nchi yao. Kwa nini?’’


Waporaji wa rasilimali za nchi, wavunaji wa jasho la wanyonge, vibaraka wa mabeberu (wasemao ‘tunapendwa huko nje’) hawana haki ya kutumia jina la Mwalimu. Wametupora kila kilicho chetu (tangu viwanda, ardhi, madini hadi nyumba), wamewanyang’anya wanyonge haki ya kupata huduma bora za afya, elimu, malazi na chakula. Hawa hawana haki ya kutaja jina la Mwalimu. Njia ambayo wanyonge wanaweza kumuenzi Mwalimu ni kwa kuzichambua kwa kina ---- zake, na hasa Azimio la Arusha, na kuzitumia kama silaha ya mapambano!


Mwandishi wa makala haya ni mwalimu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, idara ya Sayansi ya Siasa na Utawala wa Umma. Anapatikana kwa barua-pepe: sany7th@yahoo.com
 
Mwalimu wa chuo kikuu sidhani kama amefuatilia vizuri what happened in venezuela kiuchumi, majengo mengi yalibaki despite large numbers of homelessness serikali aikuwa na huwezo wa kumaliza majengo ambayo yalikuwa bure kwao baada ya outside investors kuyatelekeza na viwanda vingi vilikufa pia. Ujamaa on its own is no longer an option in our times a mixture of capitalism is needed even Nyerere knew that in the end please keep ya Azimio in the past and that is where it belongs.

Swala la uongozi wa sasa kwa mtu yeyote anaetetea kila kitu ana namna. Mbali na tatizo la ufisadi, serikali imekosa dira kauli tofauti za viongozi wa serikali moja kutofautiana mara kwa mara inaonyesha there is not team input and a clear government policy kila mtu anatafuta umaarufu kivyake na kuiba kivyake.

Halikadhalika siafiki ya kuwa matatizo ya wengi chanzo ni serikali pekee watanzania wenyewe also contribute to the problems especially at cities. Serikali ingawa inatoa huduma bure kumekuwa na ongezeko la watu mijini without the economy to support them. Hili ndio zao la wagonjwa kulala chini kutokana na hospitali kupokea wagonjwa kuliko huwezo wa capacity zake especially wamama/wadada amabao hawana mchango kwenye uchumi tofauti na wale wanaopata ajira na kuweza kulipia matibabu na huduma zingine.

Swali la kujiuliza can the government accommodate those moving into cities with the current national economic positioning or may be people are just making unrealistic accusation; those are the lines that needed be justified lakini tuache hizi tabia za kutoa lawama as if the government has unlimited resources to solve all the national problems at whim without addressing the problem and its causes.
 
Maneno meeeengi lkn kwa mtanzania mwenye kuufahamu ukweli haya maana yoyote ! Na ni uongo mtupu!

We unamsifia MDINI? NA MBAGUZI?

Nyerere ktk umri wake toka baada tu ya kupata uhuru YYT ASIEKUWA.MKRISTO KWAKE ALIKUWA NI UCHAFU TU!

Kanisa aliliweka.mbele mpaka kwenye ruzuku za serikali.
We kaa ukijaribu kudanganya watu kuwa Nyerere alikuwa mwema!
Yule alikuwa ni nyoka anae kuuma huku anakupuliza! Anakuchekea hadharani akiingia ndani anakuwekea sumu kwenye chakula!
Ikiwa unampenda kiasi cha kutetea uovu wake hadharani namna hii! Basi mfate huko KUZIMU.

Wewe ni mwalimu wa kigalatia ambae usingefika kumsifia huyu muovu ispokuwa ule MFUMO KRISTO aliuacha umekufikisha hapo ulipo na kwa kuandika description zako na wapi unapatikana NI MOJA YA KUTAFUTA SIFA ZISIZO KUWA NA MAANA!

Ukitetea uovu basi iko siku utakudhuru wewe au kizazi chako! Watch out!!
 
....Kanisa aliliweka.mbele mpaka kwenye ruzuku za serikali.
We kaa ukijaribu kudanganya watu kuwa Nyerere alikuwa mwema!
Yule alikuwa ni nyoka anae kuuma huku anakupuliza! Anakuchekea hadharani akiingia ndani anakuwekea sumu kwenye chakula!
Ikiwa unampenda kiasi cha kutetea uovu wake hadharani namna hii! Basi mfate huko KUZIMU.....
  • ​Hapa umenipa changamoto ya kujifunza zaidi tulikotoka, tulipo na tunakoelekea. Thanks
 
Leo taifa liko katika kumbukumbu za tangu alipotutoka kiongozi shupavu,kipenzi cha watanzania na mwanafalsafa nguli kuwahi kuzaliwa nchini,"Baba wa taifa Mwl. JK NYERERE".Ni kiongozi huyu makini aliyelijenga taifa letu katika misingi ya umoja,amani,upendo na mshikamano.

Nyerere enzi za uhai wake alilaani na kupinga vikali ubaguzi wa rangi,jinsi,dini na kabila kutamalaki nchini,pia alishiriki kwa vitendo kupinga na kupiga vita aliowaita maadui wakuu wa mtanzania yaani,UJINGA,UMASKINI na MARADHI na kuwataka wananchi wakupiga vita pale wawaonapo.

Ni kiongozi huyu alipenda elimu kwa lengo la kuhakikisha watanzania wanapata mwanga wa ukweli ili kukabiliana na changamoto za ujenzi wa taifa.

Alichukia kwa viwango vyote ubinafsi,ufisadi,ulimbikizaji wa mali,ulaghai na wizi katika sekta na taasisi za serikali.Ndugu zangu ni kosa kuu kutomuenzi mpiganiaji mahiri huyu wa haki za mtanzania na wengine wa style yake,katika mchango wao wa kulea na kutengeneza mazingira ya amani na upendo tunaojivunia leo.(R.I.P JK NYERERE).
 
Unaposema ni dhambi kwa mujibu wa andiko lipi? Acha mahaba ya chama kupita kiasi mwishowe utakufuru mungu bure.
 
Hivi venezuela wana nini cha kujivunia kuhusu hugo chavez, binafsi sioni.

Ukijaribu kutafakari kipindi Mwl alichojaliwa kuongaza nchi hii, zaidi ya miaka 20. Unawezaje kumtenga na haya tunayo ya shuhudia kuendelea hapa nchini? Pengine ni seme hivi yeye anamchango mkubwa sana kama kiongozi katika matatizo yanayo tupata sasa kama taifa.

Huyu ni kiongozi aliyepata kuaminiwa sana na wananchi wake, alipewa ushirikiano sana kuliko viongozi waliokuja baada yake, lakini nasikitika kusema kuwa hakuweza kuweka misingi endelevu katika taifa hili.
 
Fikiria kuhusu makaripio yake juu ya ufisadi, udini, chuki, mauza uza ya muungano na ubaguzi halafu tazama purukushani na vuta nikuvute iliyopo, je wewe unadhani Mwl.Nyerere alikuwa na nini cha ziada ambacho viongozi wa sasa wamepungukiwa kiasi kwamba nchi haiko shwari tena (ingawa watawala wanajiaminisha kwamba hakuna tatizo) katika nchi hii. Pili, je kuna mtanzania yeyote kwa sasa anayeweza kuvaa viatu vya mwalimu kwa kujikana yeye mwenyewe na familia yake na marafiki zake kwa kuiweka tanzania kipaumbele namba moja? Karibuni wote.
 
Hivi venezuela wana nini cha kujivunia kuhusu hugo chavez, binafsi sioni.

Ukijaribu kutafakari kipindi Mwl alichojaliwa kuongaza nchi hii, zaidi ya miaka 20. Unawezaje kumtenga na haya tunayo ya shuhudia kuendelea hapa nchini? Pengine ni seme hivi yeye anamchango mkubwa sana kama kiongozi katika matatizo yanayo tupata sasa kama taifa.

Huyu ni kiongozi aliyepata kuaminiwa sana na wananchi wake, alipewa ushirikiano sana kuliko viongozi waliokuja baada yake, lakini nasikitika kusema kuwa hakuweza kuweka misingi endelevu katika taifa hili.

Hapo mkuu umepiga ikulu! Na enzi zake nyerere sasa hivi wangekuwa wanakutafuta ukafungwe bila kupitia mahakamani!
 
Maneno meeeengi lkn kwa mtanzania mwenye kuufahamu ukweli haya maana yoyote ! Na ni uongo mtupu!

We unamsifia MDINI? NA MBAGUZI?

Nyerere ktk umri wake toka baada tu ya kupata uhuru YYT ASIEKUWA.MKRISTO KWAKE ALIKUWA NI UCHAFU TU!

Kanisa aliliweka.mbele mpaka kwenye ruzuku za serikali.
We kaa ukijaribu kudanganya watu kuwa Nyerere alikuwa mwema!
Yule alikuwa ni nyoka anae kuuma huku anakupuliza! Anakuchekea hadharani akiingia ndani anakuwekea sumu kwenye chakula!
Ikiwa unampenda kiasi cha kutetea uovu wake hadharani namna hii! Basi mfate huko KUZIMU.

Wewe ni mwalimu wa kigalatia ambae usingefika kumsifia huyu muovu ispokuwa ule MFUMO KRISTO aliuacha umekufikisha hapo ulipo na kwa kuandika description zako na wapi unapatikana NI MOJA YA KUTAFUTA SIFA ZISIZO KUWA NA MAANA!

Ukitetea uovu basi iko siku utakudhuru wewe au kizazi chako! Watch out!!
una fikra za kidhaifu hadi unasikitisha. pole sana
 
Huyu ni kiongozi aliyepata kuaminiwa sana na wananchi wake, alipewa ushirikiano sana kuliko viongozi waliokuja baada yake, lakini nasikitika kusema kuwa hakuweza kuweka misingi endelevu katika taifa hili.

na mimi nasikitika kukuambia kuwa hujui lolote kuhusiana na historia ya nchi hii, kama sikosei wewe utakuwa mhamiaji haramu otherwise huwezi kusema kuwa Mwl. Nyerere hakuweka misingi endelevu. Nakushauri nenda kasome kitu kinaitwa nation building all over the Afrika then utaona ni kwa jinsi gani Mwl. Nyerere alifanikiwa kuliko viongozi wengine Afrika
 
Fikiria kuhusu makaripio yake juu ya ufisadi, udini, chuki, mauza uza ya muungano na ubaguzi halafu tazama purukushani na vuta nikuvute iliyopo, je wewe unadhani Mwl.Nyerere alikuwa na nini cha ziada ambacho viongozi wa sasa wamepungukiwa kiasi kwamba nchi haiko shwari tena (ingawa watawala wanajiaminisha kwamba hakuna tatizo) katika nchi hii. Pili, je kuna mtanzania yeyote kwa sasa anayeweza kuvaa viatu vya mwalimu kwa kujikana yeye mwenyewe na familia yake na marafiki zake kwa kuiweka tanzania kipaumbele namba moja? Karibuni wote.


Ndg yangu achana na hizi propoganda watz tulizo kuwa na bado tunaendelea kulishwa.

Kukana familia yake, kukana marafiki zake sina hakika siwezi kulisemea. Ila kujikana mwenyewe sio kweli ni uongo tena mchana kweupe.

Hivi mtu aliye jikana mwenyewe anawezaje kuendeshwa kwenye mercedez benz s class huku akimwekee raia sheria inayomtaka kuomba kibali ikulu akitaka kumiliki vw beetle? Kuna mtu angeweza mbishiaa Nyerere kama angetaka kutumia hata punda badala ya gari?

Hebu jaribu kufuatilia maisha ya waastafu waliokuwa viongozi na hata wafanyakazi wa serikali iliyoongozwa na Nyerere uone dhiki walizo nazo au kufa wakiwa nazo, halafu jiulize kwa nini watu wameamua kuchagua ufisadi.

Alichokuwa na ziada ni kwamba alikuwa hana jf.
 
Siku ya alhamisi tarehe 14 OCT 1999 mida ya saa 3 paka saa 5 asubuhi ulikuwa wapi? ulikuwa unafanya nini na ulijiskiaje? baada yakupata habari ya kifo cha hayati baba wa taifa (MWL J. K. NYERERE)
Binafsi nakumbuka nilikuwa shule na tulikuwa nje ya darasa kama watu 7 hivi tupo nakiredio tunasikiliza RTD. Baada ya kutangazwa kifo cha mwalimu kitu kilichonijia akilin nilihisi Tz ndo mwisho wa amani na nikaona kama nchi imegubikwa na wingu zito na hatujui chakufanya. lakin zaid ilinishangaza maana lengo la safari ya mwalim ilikua kwenda kucheki afya kama sijakosea lakin akarudi akiwa kwenye jeneza.! Paka hii leo taifa lilipoteza nguzo muhim sana na kuna pengo lisilozibika' paka mda fulan huwa nafikilia kwanini viongozi wa sasa hawazitumii hotuba na vitabu vya mwalim wakichanya na akili zao ili kulisukuma gurudum la maendeleo. yote kwayote Mwenyezi Mungu ampe pumziko la milele na tunatambua mchango wake kwa taifa'' pia yale aliyokuwa anayaona nakuyaongelea leo hii tunayashudia'' hivyo nachelea kusema mwalimu alikua na maono kama nabii. Haijatokea na haitatokea kiongozi makini, mwadilifu, mzalendo na mwenye kujiamini kama JK Nyerere.
 
na mimi nasikitika kukuambia kuwa hujui lolote kuhusiana na historia ya nchi hii, kama sikosei wewe utakuwa mhamiaji haramu otherwise huwezi kusema kuwa Mwl. Nyerere hakuweka misingi endelevu. Nakushauri nenda kasome kitu kinaitwa nation building all over the Afrika then utaona ni kwa jinsi gani Mwl. Nyerere alifanikiwa kuliko viongozi wengine Afrika

Mafanikio gani unayo yaongelea hapa!
Hebu tafadhali usichafue mazingira hapa!
Kupanga foleni ya unga wa njano ndio mafanikio hayo?
Kugawiwa sukari nusu kilo kwa mwenzi ndio mafanikioa hayo??
Kunyimwa uhuru wa kuikemea serikali na watu kutiwa mahabusu miaka chungu mzima ndio mafanikio hayo!?
Kutuletea MFUMO.KRISTO ndio mafanikio hayo??
Ustake kunchafua hapa! Baadhi ya Wenzetu wa Afrika wameanza kuona matunda ya uhuru mara baada tu ya wakoloni kuondoka!
Sisi badala ya kufurahi wakoloni kuondoka! Wazee wetu walinza kulaani namna serikali chini ya uongozi wa huyo mkatoliki ilivyo kuwa ina wanyanyasa!
Walitamani waingereza warudi kuendelea kuwatawala!
Sasa usiongee vitu kama huna kichwa!!
 
Back
Top Bottom