TUACHE UNAFIKI KIDOGO, TUONGEE UKWELI

life255

JF-Expert Member
Joined
Aug 24, 2026
Posts
584
Reaction score
1,457
TUACHE UNAFIKI KIDOGO, TUONGEE UKWELI.

Kuna kitu nimekuwa nikikiona sana kwenye maisha ya watu, na sijui kama ni mimi nimekiona au wengi tunakiona ila tunaogopa kusema.

Kwanini mtu akianza maisha akiwa hana kitu, watu wanamwambia “vumilia, kila mtu anaanzia chini”, lakini huyo huyo mtu akifanikiwa kidogo tu, ghafla wanaanza kusema ana majivuno, amebadilika, amesahau alikotoka?

Na kibaya zaidi, wakati mwingine watu wanaotaka uendelee kuwa chini ndio hao hao wanaokuambia wanakupenda na wanakutakia mema.

Mimi nimeanza kuamini kwamba sio kila anayekushauri anataka ufanikiwe. Wengine wanataka tu usiwazidi.

Ukiwa huna pesa, wanakuita mnyenyekevu.

Ukianza kupata pesa, wanakuita mwenye maringo.

Ukiwa kimya, wanasema huna confidence.

Ukianza kujieleza, wanasema unajiona.

Ukiwa single, wanakuuliza umefeli wapi.

Ukipata mtu anayekupenda, wanaanza kuchunguza kwanini amekuchagua.

😂

Sasa swali la JF hapa ni hili:

Tunaishi kwenye jamii inayotaka mtu afanikiwe kweli, au tunataka tu afanikiwe lakini asituzidi?

Na kama unaamini watu wengi wana wivu wa mafanikio ya wengine, kwa nini huwa tunakataa kabisa tunapoitwa watu wenye wivu?

Msije na majibu ya kisiasa ya “kila mtu ana safari yake” 😂

Nataka majibu ya ukweli kabisa. Mtu akifanikiwa na maisha yake yakabadilika, ni lazima abaki yule yule ili kuwaridhisha watu waliomjua akiwa hana kitu?

Hapa ndio nataka mjadala uanze. 👀
 
Huwezi mlizisha kila mtu kwenye hii dunia ila wanasema shika hela tuijue tabia yako,wengi hubadilika wakishika hela
Watu hawabadiliki, ila pesa inafungua zile tabia zilizofichwa. Kwa mfano mwingine ana roho ya kutoa ila hana cha kutoa. Mtu kama huyo siku akipata pesa kila mgalatia atafurahia maisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…