Tuache ulimbukeni na mapenzi ya kuji show

rosita

JF-Expert Member
Oct 18, 2013
509
468
Habari zenu wana JF
Wapendwa kwa kuwa hili ni jukwaa letu pendwa na kujadili na kushauriana mambo mbalimbali ya maisha na mahusiano

Kuna tabia ambayo me binafsi huwa inanikera sana hususani unapoamua kutoka out ukiwa na familia au marafiki zako mnaoheshimina

Kuna baadhi ya watu wanaojifanya kuwa wanapendana sana na wao ndo wa kwanza kuwa na wapenzi au kupendwa..unakuta couple iko busy sehemu ya public kushikana shikana.....kupapasana....kubusiana na baadhi mpk wanafunguana suruali na kupandisha sketi au gauni...

Kumbekeni hayo ni maeneo ya public sio ya private na kufanya hao matukio kwanza inaonesha akili zenu hazijawa matured au mmeruka stage...na mapenzi ya kujishow mara chache sana huwa yanadumu...unakuta mwanamke ndo anadhalilishwa zaidi anavuliwa mpk nguo na wakiwa na assumption kuwa hawaonekani sijui...

Mapenzi ni raha sana ila inabidi tuwe na staha...mwanamke at least onyesha heshima yako kama mwanamke sio kukubali kuvuliwa nguo kwenye public area tena mbele za watu tena wengine ni kama kaka zako na wajomba zako

Jamani mkiona mmezidiwa na nyege nendeni katika mahala penye utulivu fanyeni yenu kuliko kujitia aibu mbele za watu

Kumbukeni sie ni watanzania acheni kuiga mpaka vitu visivyoigwa...tunaishi dunia ya kisasa lakini tusiache kubehave kwa heshima na kuwaheshimu wanaotunzunguka

Hivi mnadhani couple tusioshikana shikana hadharani hatuna genye au hatupendani..tena tunapendana kuliko nyie wenye mapenzi ya kujishow

Juzi nilikaa somewhere na wafanyakazi wenzangu tunaoheshimiana sana na tulikuwa pale kwa ajili ya kikao cha send off ya mtumishi mwenzetu..baada ya kikao tukaamua kupata nyama choma pamoja huku tukipapasa macho kwa kuangalia mpira....mara akaja jamaa mmoja na mdada ambae kavaa vizuri nguo ya kitenge kapendeza...ila mpk ametoka lile eneo kila mtu alikuwa kawadharau...watu waliacha kuangalia mpira na kuendelea kuangalia upuuzi wao...mara wakiss mara wanyweshane wine.
.mara wapapasane...yule mwanaume alipandisha sketi ya kushona ya yule dada mpaka mapajani akawa anampapasa mapaja...mwanaume nae akafungua zipu yule dada akawa anapapasa dyudyu yake..mpk wanaondoka pale watu waliacha kujadili mpira wakawa wao ndo gumzo....kibaya zaidi unakaa public area ukiwa unajua hufamiki kumbe wako baadhi ya watu wanaokufahamu ila wewe unaweza usiwafaham...kumbe yule bi mdada alifahamika na mmoja wa watu wa eneo lile kuwa anafanya kazi somewhere..So imagine heshima yako mbele ya jamii inakuaje endapo utakubali kujidhalilisha vile mbele za watu.

Hebu nisaidiane wana JF labda mie rosita ni mshamba...ila kwa mtazamo wangu naona mapenzi ya dizaini hiyo ni ya kishamba na kujishow kwa sifa za kijinga..na sidhani kama mwanaume akikufanyia hivyo mbele za watu anakupenda na kukuheshimu..mwanaume anayekupenda na kukuheshimu kamwe hawezi kuonesha mapaja yako na kukuvua vua nguo mbele za watu..Atapenda uwe na staha na uheshimike mbele za watu.

Wengine mnaweza sema huyu nae akikaa maeneo kama hayo si afuate yake na aachane na maisha ya watu...macho hayana pazia nimetumia muda wangu kuwaelimisha kama kuna baadhi yetu tunabehave kama hivyo katika maeneo yasio rasmi basi tuelimike na kuwa wastarabu...ustarabu kitu cha bure wapendwa..niwatakie week end njema wapendwa.
 
Tuendelee kuwa washamba tu best yangu..wacha fasheni itupite...kuvuliwa nguo hadharani hapana
Huo uzungu unaowafanya wafanye mambo ambayo hata wazungu hawayafanyi ninashindwa kuelewa. Zile cinema wanazoona ni kuwa watu wako location tu.
 
Maisha yangu yote ya mahusiano hata kutembea na nchi za watu sijawahi ona watu kuvuana nguo sijui kufungua zip in public, watu huwa wanashia ku kiss tu tena sio ile kilimbukeni hvyo (u can just tell ni love partners).

Ki ukweli hii mambo ipo hapa Dar sehem kadhaa nimeona. Mara nyingi ukiwafatilia such people utanote hawana shule kichwani / poor living standards.

Thats just too gross...i can imagine. Hata chakula huiva vizuri kikifunikwa. Ni ufal.a to be honest.
 
Ha aha ha sana sana wenye age 20-25 kwenda juu huko ni nadra sana kuona huo utumbo wanafanya hadharani
 
Nakumbuka kuna kipindi nilienda Club jamaa wakaanza kucheza style ya Blues kila mziki uliokuwa unapigwa..Iwe ndombolo..Iwe kwaito wao ni mwendo wa Blues tu kidogo wakasogezana kwenye nguzo kwenye dance floor kidogo mama kageuka kwa mbele kidogo...kidogoo...kidogoo..Hee watu kushangaa jamaa anakula mzigo sehemu ya wazi kabisa...So Pombe huwa si chai kila kitu kwa yafaa kuwa na kipimo...Hata wewe ukizidisha Pombe kidogo unaweza fanya kitu leo then kesho ukasema si wewe..
 
Hapo ndiyo binadamu anapojishusha, Mungu alitupa uwelewa wa mema na mabaya tutofautiane na wanyama sasa kama na sisi tunabehave kama wanyama sijui tutafika wapi. Mbwa anaweza kufanya hayo hadharani si ndiyo?
 
Mmmh basi huyo jamaa kichwa cha panzi kufanya such things in public.

Mi hata nipige vyombo vipi...utakacho note nimelewa huwa na mkua mpole na mkimya sanaa sio kawaida. Nikiwa na dem alone masihara mengi. Tehe
 
Mbaya sana Mkuu ndiyo maana nasema kila kitu kiwe na kiwango hapo tutakuwa salama ila tukizidisha ni mbaya mno..
 
Mmmh basi huyo jamaa kichwa cha panzi kufanya such things in public.

Mi hata nipige vyombo vipi...utakacho note nimelewa huwa na mkua mpole na mkimya sanaa sio kawaida. Nikiwa na dem alone masihara mengi. Tehe
Kila mtu yopu na style yake vyombo vinapofika mahali yake kuwa wengine watajikojolea wengine wanakuwa wapole kama wewe..Wengine ndiyo anasahau kiswahili yeye anakuwa ni YES, NO...Ila yabidi tuji-control sana maana wale watu walifanya jambo fedheha sana..
 
Aah watu hawakuwanasa makofi ?? hahaha.....daah aisee mtu ukiwa had unatoa haja ni kheri ulewe ukiwa kwako. Mjini hapa watu wataja kukubeba beba. Tehe
 
Mmmh basi huyo jamaa kichwa cha panzi kufanya such things in public.

Mi hata nipige vyombo vipi...utakacho note nimelewa huwa na mkua mpole na mkimya sanaa sio kawaida. Nikiwa na dem alone masihara mengi. Tehe
kweli mkuu ni hulka tu ya mtu ...tusisingizie pombe...mlevi hata siku moja hajichomi kisu au kunywa sumu why? Ila anaweza kufanya mapenzi na dada poa bila kondom akisingizia pombe...huyu jamaa alidhamiria before hata hajanywa kumla bi dada mbele ya halaiki.
 
Kila mtu yopu na style yake vyombo vinapofika mahali yake kuwa wengine watajikojolea wengine wanakuwa wapole kama wewe..Wengine ndiyo anasahau kiswahili yeye anakuwa ni YES, NO...Ila yabidi tuji-control sana maana wale watu walifanya jambo fedheha sana..
Yes No imenichekesha
 
Back
Top Bottom