Tuache kuutumia huu uongo

Tuache kuutumia huu uongo

Wisest man

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2013
Posts
993
Reaction score
333
Kuna baadhi ya waandishi wakitaka kuzungumzia watu waliofumaniwa wanasema ".... wakivunja amri ya 6" nimejiuliza sana hiyo amri ya sita inayosema usizini imeandikwa ktk kitabu gani? na kwa nini hawasemi ni amri ya 5 au ya 7? hakuna sehemu yoyote ktk biblia inayosema kuwa amri ya 6 inasema usizini, hebu kama soma biblia kitabu cha kutoka 20:1-17 hizi ni amri kumi alizozitamka mungu mwenyewe
 
To say of what is that it is not, or of what is not that it is, is false, while to say of what is that it is and of what is not that it is not, is true.
aristotle
 
Kutoka ; sura ya 20:
Aya ya 3 Usiwe na miungu mingine ila mimi. – Amri ya kwanza
Aya ya 4 hadi ya 6 ni ufafanuzi wa amri iliyo kwenye Aya ya 3
Aya ya 7 Usilitaje bure jina langu mimi Mwenyezi Mungu – Anri ya pili
Aya ya 8 Usisahahu kuweka kitakatifu siku ya sabato – Amri ya tatu
Aya ya 9 hadi 11 ni ufafanuzi wa amri iliyo kwenye Aya ya 8
Aya ya 12 Waheshimu baba na mama yako…. – Amri ya nne
Aya ya 13 Usiue – Amri ya tano
Aya ya 14 Usizini – Amri ya sita
Aya ya 15 Usiibe - Amri ya saba
Aya ya 16 Usimshuhudie jirani yako uongo _amri ya nane
Aya ya 17 Usitamani nyumba ya jirani yako, wla mke wake wala mtumwa wakiume au wa kike,wala ng'ombe wake, wala punda wake wala kitu chochiote kilicho mali yake.
Aya hii inazungumzia vitu viwili, mke na mali ndiyo maana zikawekwa kuwa amri mbili:
Usitamani mke wa jirani yako – Amri ya tisa
Usitamani mali ya jirani yako – Amri ya kumi
 
Kuna baadhi ya waandishi wakitaka kuzungumzia watu waliofumaniwa wanasema ".... wakivunja amri ya 6" nimejiuliza sana hiyo amri ya sita inayosema usizini imeandikwa ktk kitabu gani? na kwa nini hawasemi ni amri ya 5 au ya 7? hakuna sehemu yoyote ktk biblia inayosema kuwa amri ya 6 inasema usizini, hebu kama soma biblia kitabu cha kutoka 20:1-17 hizi ni amri kumi alizozitamka mungu mwenyewe

Si kila aya ina amri. Zingatia hilo
 
hawasemi aya ya saba, wanasema amri ya saba!
Kwani kwenye hiyo sura kuna amri ngapi? Na usizini kimtiririko inakuwa ya ngapi?

Kumbuka sio kila aya ina amri!
 
wewe ndo walewale tu, mnaodhani ukatoliki ndo ukristo, amri ya sita inasema usiue wewe unasema usizini!!!i
 
Mmmh huyu kama sio shahidi wa yehova na habari za mnara wa mlinzi basi atakuwa msabato maana anabishia paka biblia labda utuambie mwezetu unatumia version gani au unayo ambayo umeamua kuimodify kwa maslai ya dhehebu lako
 
Daaahh aiseee huyu atakua ni msabato....daaah nimeshangaaaa kwa kweli....duuuuhhhhh....
 
Kutoka ; sura ya 20:
Aya ya 3 Usiwe na miungu mingine ila mimi. – Amri ya kwanza
Aya ya 4 hadi ya 6 ni ufafanuzi wa amri iliyo kwenye Aya ya 3
Aya ya 7 Usilitaje bure jina langu mimi Mwenyezi Mungu – Anri ya pili
Aya ya 8 Usisahahu kuweka kitakatifu siku ya sabato – Amri ya tatu
Aya ya 9 hadi 11 ni ufafanuzi wa amri iliyo kwenye Aya ya 8
Aya ya 12 Waheshimu baba na mama yako…. – Amri ya nne
Aya ya 13 Usiue – Amri ya tano
Aya ya 14 Usizini – Amri ya sita
Aya ya 15 Usiibe - Amri ya saba
Aya ya 16 Usimshuhudie jirani yako uongo _amri ya nane
Aya ya 17 Usitamani nyumba ya jirani yako, wla mke wake wala mtumwa wakiume au wa kike,wala ng’ombe wake, wala punda wake wala kitu chochiote kilicho mali yake.
Aya hii inazungumzia vitu viwili, mke na mali ndiyo maana zikawekwa kuwa amri mbili:
Usitamani mke wa jirani yako – Amri ya tisa
Usitamani mali ya jirani yako – Amri ya kumi

mbona amri juu ya kuiheshimu sabato imepindishwa pindishwa?
 
Nani anapingana na biblia katika hali ya kawaida wewe soma tu maswali yake amri ya sita inajulika...ni usizini...

kwenye biblia hakuna sehemu iliyoandikwa USISAHAU KUWEKA KITAKATIFU SIKU YA SABATO!km unaijua hebu tupia hapa
 
Unaposoma bible omba MUNGU akupe roho wake mtakatifu akueleweshe,pia kuzijua amri na kutozitenda ni bure,YESU alimuuliza kijana fulani je wazijua amri akasema ndio toka utoto wangu,akamwambia kauze ulivyo navyo na uwape maskini na kisha unifuate je alivunja amri ipi kati ya zile kumi?
 
Back
Top Bottom