Tuache kujichubua(skin bleaching)

Tuache kujichubua(skin bleaching)

Kwanza huku nyuma ya shingo maskini sijui hawajionagi au ndio vipako havireact
Wanaangalia mbele tu wakishika kioo focus Iko pale kwenye uso..ule weusi huku nyuma hawauoni.sie ndo tunauona
 
Kizazi Cha Sasa sio wanawake Wala wanaume tuko obsessed na kuwa weupe,wengine tunajidanganya Kwa jina la kuglow.

Kuglow uglow na rangi yako halisia huku unawaka na kumeremeta,rangi yako halisi,ngozi yako safi
kwani nani kasema weusi ni mbaya?

Weusi ni rangi adimu yenye thamani sana hata wazungu wanatamani wawe nao ila ndo hivo,wanatudharau tunavyojibabua.

Watu wenye ualbino (albinism) wanatamani wawe na hii rangi tunayoichezea lakini wapi..hawawezi.

Ndani ya mwili Kuna seli zinazalishwa tuziite melanocytes,hizi zinaachia kitu inaitwa melanin..hii ndo huchochea rangi ya ngozi nywele na macho yako.sasa unapopaka mikorogo ama kipodozi chenye kubleach huwa kinapenya na kuingia ndani ya mfumo wako wa damu,zile kemikali toka kwenye mafuta ulopaka zinaenda na kuingilia uzalishaji wa melanin, ni kama kinabock na huku Kuna nyingine inabrighten ngozi yako,utaanza kuwa wa njano au mweupe.

Lakini umewahi kujiuliza utakapoacha kutumia mkorogo utabaki hivohivo? hapana
Ukikosa pesa ya mikorogo tu utaanza kuwa kituko kama kuku aliebanikwa unajua kwanini? Sababu umeua uzalishaji wa melanin,inakulinda dhidi mionzi ya jua,so Kwa ngozi iliyochubuliwa haiwezi kupambana na mionzi ya jua na ikizidiwa kinachofuata ni kansa.

Ukioverdose matumizi ya mkorogozile kemikali Zina uwezo wa kuua kabisa seli zako mwilini.hutarudi awali tena.jua litakuwa adui yako,mionzi ikikuzidia kifuatacho ni kansa. Huoni kwanini wenye albinism wanapata tabu juani Hadi wajilinde Kwa kupaka mafuta maalum ya kuwalinda dhid ya mionzi ya jua. Sababu hawana melanin..kinyume na hapo wakikosa hayo mafuta wakipigwa na jua sana wanatoka vidonda na kansa za ngozi ndio tishio lao kuu.
Hata wazungu wanapaka sunblocks,jua sio rafiki kwao.

Kama melanin inasaidia macho tarajia macho yako kufa au uoni hafifu.huoni wenye albinism wanavyopata shida ya macho
Mkorogo unaua macho yako!

Tuthamini tulichopewa.sisi ni wazuri!
Tujikubali.

View attachment 3333527
Ni sahihi muache kujikoboa.Mkifanya hivyo huwa mnafanana na ngedere kabisa.
 
Dah1Kama mwanaume anatumia kwa ushauri kitabibu sawa.Ila kama anatumia kujikoboa hilo ni tatizo hasa wanaume wengi wa kikongo.
cc;Levis,Lengos,Kambale Muyali,Petit Numbi,Uvira na papaa Kibundila wakiwa pale Kisangani Congo DR,kwa taatifa.
Sio congo..hapa Tz mbezi beach,kawe,kinondoni nk
Wamejaa tele
 
Yes Mkuu Ila. Kujichubua ni issue ya kiakili zaidi .

Una we za kusoma huu mtiririko

Self -image
Self esteem
Self confidence

So Ku-bleach is denial of self image means kuikataa picha yako ya Asili
Nimekuelewa mkuu
 
Huu ushauri wakina mwajuma ndala ndefu hawezi kukuelewa kabisa
20250206_141858.jpg
 
Back
Top Bottom