Determinantor
Platinum Member
- Mar 17, 2008
- 57,789
- 92,245
Hii biashara ya kusema Watanzania ni Wavivu, hawana akili sijui hawana njaa ni udhalilishaji! Hawa ndio walitusomesha kwa kuchoma mkaa, kwa kutembea kwa miguu zaidi ya 20km kwenda sokoni kuuza uwele,.mahindi au mtama, hawa ndio wanaoamka asubuhi na kwenda Shamba wakimuomba Mungu mvua japo inyeshe. Hawa hawa ndio waliowapigia kura baada ya kuwarubuni, eti Leo tunawaita Wavivu?
Inauma sana Aisee, tumewanyima elimu, tukawaacha na magonjwa yao, wakafiwa wakalia wakazika wakasahau, kisha Leo tunawaita Wavivu!!!! Mungu atuepushe.
Inauma sana Aisee, tumewanyima elimu, tukawaacha na magonjwa yao, wakafiwa wakalia wakazika wakasahau, kisha Leo tunawaita Wavivu!!!! Mungu atuepushe.