TTCL Yavuna Wateja Wapya 215,000

mamayoyo1

JF-Expert Member
Jul 25, 2018
1,011
1,019
SHIRIKA la Mawasiliano Nchini (TTCL) katika kipindi cha siku 30 limeweza kusajili wateja wapya 215,000, ikiwa ni Mpango Mkakati wa Shirika hilo katika kujiinua kibiashara na kuongeza wigo huduma ya Mawasiliano kwa Watanzania ikiwa ni utekezaji wa agizo la Rais Dkt. John Magufuli.

Akizungumza Alhamisi (Julai 4, 2019) katika Maonesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam yanayoendelea katika Viwanja vya Julius Nyerere, Meneja Mawasiliano wa TTCL Nicodemus Mushi alisema Shirika hilo limetekeleza kwa vitendo agizo la Rais Dkt. John Magufuli alilolitoa kwa Shirika hilo tarehe 21 Mei, mwaka huu.

Mushi alisema hadi sasa huduma za Mawasiliano za Kampuni hiyo katika Mfumo wa 4G zinapatikana katika Mikoa 16 nchini na mpango uliopo ni kuhakikisha kuwa maeneo yaliyobaki yanapata huduma za Shirika kupitia Mpango Mkakati wa Shirika hilo uliojiwekea na hivyo kuweza kuleta ushindani wa huduma ya mawasiliano na makampuni mengine nchini.

“Mwaka uliopita tulijiwekea Mpango Mkakati wetu ambao utahakikisha kuwa tunaweza kuleta ushindani na makampuni mengine na hivi sasa kama unavyoona tumeweza kupata wateja wapya 215,000 na kupitia maonesho hayo tutaweza kuongeza wateja wengi zaidi ” alisema Mushi.

Aliongeza kuwa kwa sasa Shirika hilo limeweza kupata wateja wengi zaidi wakiwemo watumishi wa serikali, ambapo kwa kutambua umuhimu huo, TTCL imeanzisha kifurushi maalum cha ‘watumishi pack’ ambacho kinaweza kutumiwa na wafanyakazi wote wa serikali kwa kuweza kukamilisha taratibu mbalimbali ikiwemo vitambulisho vya kazi.

Akifafanua zaidi Mushi, alisema kauli zinatolewa na watu mbalimbali kuhusu kauli ya Rais Dkt. John Magufuli kuwataka wafanyakazi wa serikali kutumia huduma za mawasiliano za shirika hilo, ni kuwa zitawahusu watumishi wa umma ambao wanalipiwa huduma za mawasiliano ya simu na serikali na si kinyume na maelekezo hayo.

Aliongeza kuwa malengo ya Taasisi hiyo ni kuweza kujipanga ili kuendelea kutoa huduma bora na zenye viwango ili kuweza kuongoza na kuwa kampuni bora ya mawasiliano inayotoa huduma bora kwa wateja wake nchini.

“Sisi kwa upande wetu tumeendelea kuwalipa vizuri mawakala wetu ikiwemo kutoa kamisheni nzuri kwao ili kuhakikisha kuwa huduma zetu zinazotolewa zinakuwa zinakidhi matakwa ya wateja na soko la mawasiliano kwa ujumla” alisema Mushi.
 
Ila nilipo ni km 14 toka City Center Mtandao unasoma Edge
 
Mbona idara yetu hawajaja?walitudanganya wanakuja tukaandaa watu wetu hawakuja,wanafikri tutawafuata,wenzao walikuja wakasajili wiki mzima, nasikia hata magereza nasikia waliwadanganya hivyohivyo,
 
Wanavuna wasichopanda na wanavuna kwenye mashamba ya wengine...wengine walihangaika juani, TTCL wanakula kivulini.
 
Unavuna ulipopanda. Sasa TTCL imepanda wapi?

Sema TTCL imekwiba wateja 215,000 toka makampuni mengine kwa kushurutishwa na Rais
 
wapanue zaidi 4G kwenye miji mbalimbali, mimi binafsi nafurahia mno huduma zao hususani 'boom pack', baada ya kunyanyaswa sana na voda nikaamua kurudi nyumbani na sijawahi juta.
Ni kweli. Njia ni kuboresha huduma na kutofanya makosa ambayo yanafanywa na kampuni nyingine. Wateja wengi wa kampuni zote za simu huwa wana malalamiko yanayofanana. Wakiweza kuwa tofauti watapata wateja wengi sana.
 
Mbona idara yetu hawajaja?walitudanganya wanakuja tukaandaa watu wetu hawakuja,wanafikri tutawafuata,wenzao walikuja wakasajili wiki mzima, nasikia hata magereza nasikia waliwadanganya hivyohivyo,
MHH
 
Mbona idara yetu hawajaja?walitudanganya wanakuja tukaandaa watu wetu hawakuja,wanafikri tutawafuata,wenzao walikuja wakasajili wiki mzima, nasikia hata magereza nasikia waliwadanganya hivyohivyo,
MHH
 
Mkurugenzi wa masoko ttcl ni polepole au zitto au mbowe? mnajitangaza kisiasa sana!

kati ya laini 200,000? ngapi zimeongezewa salio zaidi ya Mara 10?

achaneni na matamko na ngojera!

fanyeni yafuatayo

1. sambazeni miundomsingi

2. chezea bando tu, jifanye dk 20 mitandao yote kwa siku 3 na mb 300 kama hamuwakalishi wenzenu.

siasa waachueni wanasiasa.
 
Huduma zao ni Cheap sanaa hakuna mtandao unatoa 5GB kwa Sh.5,000/= kwa sasa na Vifurushi vingine vingi tuu nahisi restructuring ya Voda ya kupandisha Bei wakiona Unamudu bando fulani ndo inaongeza market share ya TTCL
 
Umesahau Bandika bandua ya Buku unapata GB 4 na ya usiku kuanzia sa 5 buku unapata GB 10.
 
Mbona idara yetu hawajaja?walitudanganya wanakuja tukaandaa watu wetu hawakuja,wanafikri tutawafuata,wenzao walikuja wakasajili wiki mzima, nasikia hata magereza nasikia waliwadanganya hivyohivyo,
TTCL ni wajinga, kwa kuwa tunataka tuwe mfano wa kuigwa tunasajili laini ila wengi wanazitia kapuni hazina lolote
 
TTCL Hapa Majohe hamna kitu. Bado ni mtandao wa mjini tu. Huo ndio ukweli wenyewe
 
Back
Top Bottom