Shirika lipo kwenye sekta ya ushindani unaohitaji akili kubwa, bahati mbaya serikali yetu si unajua utendaji kazi wake?, Basi TTCL iwe reference kwa mashirika mengine kama ATCL.
Ngoja nikupe mkasa kidogo ulionikuta... Kuna kipindi walibadili karatasi za vocha ya buku, zile vocha mpya sehem ya kukwangua ilikuwa ngum kidogo na delicate,nilikuwa nakwangua hadi namba za vocha. Nilifikisha kama vocha nane hivi nimekwangua vibaya na bahati nzuri vocha zote nilikuwa nazihifadhi.
Sku moja nikawapigia huduma kwa wateja, hapo ndo niliona mauza mauza na kuwaza kama ulivyowaza lakin badae nilipata jibu kuwa halihujumiwi. Nilipiga simu siku ya kwanza nikahudumia vizuri nikazitaja serials number za vocha zote wakaahidi watalifanyia kazi ndani ya masaa 24 then nitarudishiwa tokens za vocha nikatoa na ushauri warudishe zile karatasi za awali, nikaambiwa tumeupokea ushauri wako. Baada ya masaa 24 niliyoahidiwa kimya. Zikapita siku tatu kimya, sku ya nne nikapiga simu. Nikaanza upya kujielezea tatizo langu. Ahadi ikiwa kama siku ya kwanza.
Inshot nilipiga simu zaidi ya mara tano, huyu wa mwisho nikama tulikaliliana, nikamuuliza ebu niambie kinaga ubaga tatizo liko wapi kwa kitu kidogo hivyo. Akasema mandet ya kushughulikia vocha hawana wanachofanya ni kureport kwa muhuska na details za tatizo. Nikamuuliza muhuska kasafiri akasema yupo. So hapo nikajiongeza mwwnyewe (typical ni kama yule nurse aliekuwa anamwambia mkemia unautaka ufanyakazi bora).
Kipindi hicho DG alikuwa somebody Waziri, nikatafta email yake, nikamwandikia email ya mararamiko yangu jinsi nilivyohudumiwa na hadi sasa sjapata msaada wowote ule, kwenye email nikabbc.
Technically akajua hapa yawezekana nimebbc mkubwa, si unajua tena enzi za jiwe..
Siku hiyo hiyo nilipigiwa simu zaidi ya mara tatu kusoviwa tatizo langu, simu nyingine ilipigwa saa tatu usku kuulizwa kama tatzo langu limeisha.
Huyu wa mwisho nilimwambia tatizo ni mifumo yenu ya kiutendaji haiko sawa, watu hawawajibiki, hawafanyi system checkup kujua pending issues zinakwama kwa nani. Nikamwambie nyie mpo mpo tu, nikamuuliza mnajua ni wangapi wameacha kutumia simu zenu kwa tatizo la kupoteza hela kwenye vocha? And Y didn't you value my feedback...
Mambo ni mengi......