MWITONGO MAARIFA
JF-Expert Member
- Aug 11, 2018
- 276
- 1,428
Serikali ya awamu ya Tano inatengeneza mazingira ya ujamaa kwa nchi yetu na kututoa kwenye mixed economy.
Mashirika hayo hapo Juu yanafufuliwa kwa kasi lakini ufufuaji wake si wa ushindani bali ni kupitia kuwadhibiti washindani wao kwa kutumia dola ili wateja wahamie kwenye mashirika hayo.
Ni wazo zuri kuwa na mashirika ya umma ila ni vyema kuwa na mashirika ya umma yaliyoibuka na kukuwa kupitia ushindani wa wazi. Ukibebwa na kulipiwa kila kitu hauwezi kuwa imara bali unaandaliwa kuwa mtegemezi.
Mashirika ya simu yanaandamwa kuilinda TTCL ambayo ubunifu wake ni mdogo Sana lakini pia pesa za uendeshaji hazipangwi na kundi la wataalamu ndani ya shirika bali Hadi wapate ruzuku kutoka serikalini. Watendaji siyo wabunifu kwani ajira zake zinafuata mfumo wa serikali unaozingatia vyeti bila kujali uzalishaji unaotokana na huyo mwenye vyeti husika. Mishahara yake si yakuvutia kulingana na sekta binafsi.
Bank ya posta naona inajitanua na kuanza kuwa mbadilishaji fedha mkuu lakini ukiwaangalia watoa huduma katika benki hii hawawezi kuchukua kasi iliyokuwa inafanywa na bureau de change zinazofungwa kwa kasi. Badala ya kuisadia benki hii tumezalisha biashara haramu ya ubadilishaji fedha. Lakini pia huduma nyingine za kibenki hazileti ushindani kwa sabababu shirika halipo kibiashara
Fast jet imekufa kupisha ATC wakati mashirika haya yote yalipaswa kufanya kazi pamoja kwa sababu yanalipa kodi
Pamoja na Nia nzuri ya serikali ninaona Kama tunatumia fedha nyingi kwenye mashirika haya lakini akija mtawala mwingine atapuuza juhudi za mashirika haya na kuja na mipango mipya na hivyo serikali kuendelea kupata hasara.
Kama serikali ya Sasa imeweza kuua miradi mingi iliyoanzishwa na hawamu zilizopita ikiwemo mradi wa DART na Shirika la utangazaji basi lazima tuchukue taadhari kuweka mafedha kwenye mashirika ya umma na kuyajengea uwezo wa ushindani yajiendeshe yenyewe.
Kutumia dola kuboresha mashirika hakuyajengi yakawa imara bali yanapaswa kuacha yasimamame kushindana na sekta binafsi.
Sent using Jamii Forums mobile app