titimunda
JF-Expert Member
- Nov 26, 2014
- 7,565
- 9,806
Yes MkuuMkuu,kwamba sasa pesa ni lazima ukabadilishie Bank?Ina maana zile Bureau za Kkoo na Posta zimefungwa?Hii habari chungu sana
Soko holela liliua mashirika hayo sio mbaya kuyarejeshea uhai
Mkuu,kwamba sasa pesa ni lazima ukabadilishie Bank?Ina maana zile Bureau za Kkoo na Posta zimefungwa?Hii habari chungu sana
Soko holela liliua mashirika hayo sio mbaya kuyarejeshea uhai
Mbaya kiasi gani? Mimi nilibadili dola kwenda Tshs kwa 2370 kwenye bureau moja Kariakoo, baada ya siku kadhaa nikaenda kubadili tena ika ndio zikawa zimefungwa nikabadiki benki ta posta kwa rate ya 2330 nikaona sio mbaya sana maana nilitegemea ingeshushwa hadi 2200 huko..Jana nilienda kubadili fedha za kigeni kwenye benki moja hivi. Rate ilikua mbaya ajabu ila ndo iliyowekwa, kutoka hapo mbadala wake ningepaswa kuifuata benki ingine kilometa kadhaa, ningetumia muda na mafuta labda so nikawa sina jinsi. Ushindani wa Bureau De Change haupo tena, ni mwendo wa kupangiana tu rate. Benki nako foleni ajabu. Hii ndo Tanzania tuliyopo now.
Zinafungwa nchi nzima, BOT walitangazaMkuu,kwamba sasa pesa ni lazima ukabadilishie Bank?Ina maana zile Bureau za Kkoo na Posta zimefungwa?Hii habari chungu sana
Kim Jung Un in the making......Serikali ya awamu ya Tano inatengeneza mazingira ya ujamaa kwa nchi yetu na kututoa kwenye mixed economy.
Mashirika hayo hapo Juu yanafufuliwa kwa kasi lakini ufufuaji wake si wa ushindani bali ni kupitia kuwadhibiti washindani wao kwa kutumia dola ili wateja wahamie kwenye mashirika hayo.
Ni wazo zuri kuwa na mashirika ya umma ila ni vyema kuwa na mashirika ya umma yaliyoibuka na kukuwa kupitia ushindani wa wazi. Ukibebwa na kulipiwa kila kitu hauwezi kuwa imara bali unaandaliwa kuwa mtegemezi.
Mashirika ya simu yanaandamwa kuilinda TTCL ambayo ubunifu wake ni mdogo Sana lakini pia pesa za uendeshaji hazipangwi na kundi la wataalamu ndani ya shirika bali Hadi wapate ruzuku kutoka serikalini. Watendaji siyo wabunifu kwani ajira zake zinafuata mfumo wa serikali unaozingatia vyeti bila kujali uzalishaji unaotokana na huyo mwenye vyeti husika. Mishahara yake si yakuvutia kulingana na sekta binafsi.
Bank ya posta naona inajitanua na kuanza kuwa mbadilishaji fedha mkuu lakini ukiwaangalia watoa huduma katika benki hii hawawezi kuchukua kasi iliyokuwa inafanywa na bureau de change zinazofungwa kwa kasi. Badala ya kuisadia benki hii tumezalisha biashara haramu ya ubadilishaji fedha. Lakini pia huduma nyingine za kibenki hazileti ushindani kwa sabababu shirika halipo kibiashara
Fast jet imekufa kupisha ATC wakati mashirika haya yote yalipaswa kufanya kazi pamoja kwa sababu yanalipa kodi
Pamoja na Nia nzuri ya serikali ninaona Kama tunatumia fedha nyingi kwenye mashirika haya lakini akija mtawala mwingine atapuuza juhudi za mashirika haya na kuja na mipango mipya na hivyo serikali kuendelea kupata hasara.
Kama serikali ya Sasa imeweza kuua miradi mingi iliyoanzishwa na hawamu zilizopita ikiwemo mradi wa DART na Shirika la utangazaji basi lazima tuchukue taadhari kuweka mafedha kwenye mashirika ya umma na kuyajengea uwezo wa ushindani yajiendeshe yenyewe.
Kutumia dola kuboresha mashirika hakuyajengi yakawa imara bali yanapaswa kuacha yasimamame kushindana na sekta binafsi.
Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa kuwa tulihitaji Magufuli ili tujue uzuri wa KIKWETE, tulihitaji UMAGUFULI ili tujue ubovu wa UJAMAA, basi tulihitaji pia UJAMAA ili tujue umuhimu wa siasa za kati, kama wanavyofanya nchi kama SWEDEN, NORWAY. ubepari siyo mzuri pia.
Haya yote yangeweza kudhibitiwa na sheria madhubuti.Shida mmoja kubwa makampuni binafsi yanakuwa na vipaumbele vyao,
kwa mfano wazawa kuhudumia ndege zao ni wachache na kazi nzito kama marubani na ma engineer ni wageni.
Vivyo hivyo wahindi waliomiliki reli mswahili alitupwa nje.
Miaka ya nyuma wazawa chini ya serikali ya Nyerere walipata mafunzo mbambali ya kuendesha taasisi za umma.
Lakini baada ya taasisi za umma kuuzwa kwa watu binafsi hakuna mafunzo yakina hasa kwenye ufundi mitambo n.k
Tukiwaachia watu binafsi kila kitu tutabakia na nini?
Mkuu zipo sheria za kulinda ajira LAKINI njaa mbaya wapo watu wamehujumu fursa za wazawa.Haya yote yangeweza kudhibitiwa na sheria madhubuti.
Mfano, sheria ingependekeza uwiano mzuri kazini kati ya wageni na watanzania (ambao watatakiwa wengi >80%), sheria/serikali kuhakikisha wananchi wake wanalipwa vizuri.
Nadhani makampuni binafsi wangekubaliana na haya kwanza kabla ya kuanzisha biashara zao nchini serikali,wananchi pamoja na hao wawekezaji wote kwa pamoja wangeweza kuattain a 'win - win' situation bila shida wala lawama.
Sent using Jamii Forums mobile app
mkuu wacha ubishi ni.posta barua na sio.posta bank wanaofanya hii bishara. pita posta mpyaa pale utajionea.Kuna Bank pia,
TPB
mkuu wacha ubishi ni.posta barua na sio.posta bank wanaofanya hii bishara. pita posta mpyaa pale utajionea.Kuna Bank pia,
TPB