TTCL, Benki ya Posta, ATC, TRL taswira ya ujamaa

MWITONGO MAARIFA

JF-Expert Member
Aug 11, 2018
276
1,000
Serikali ya awamu ya Tano inatengeneza mazingira ya ujamaa kwa nchi yetu na kututoa kwenye mixed economy.

Mashirika hayo hapo Juu yanafufuliwa kwa kasi lakini ufufuaji wake si wa ushindani bali ni kupitia kuwadhibiti washindani wao kwa kutumia dola ili wateja wahamie kwenye mashirika hayo.

Ni wazo zuri kuwa na mashirika ya umma ila ni vyema kuwa na mashirika ya umma yaliyoibuka na kukuwa kupitia ushindani wa wazi. Ukibebwa na kulipiwa kila kitu hauwezi kuwa imara bali unaandaliwa kuwa mtegemezi.

Mashirika ya simu yanaandamwa kuilinda TTCL ambayo ubunifu wake ni mdogo Sana lakini pia pesa za uendeshaji hazipangwi na kundi la wataalamu ndani ya shirika bali Hadi wapate ruzuku kutoka serikalini. Watendaji siyo wabunifu kwani ajira zake zinafuata mfumo wa serikali unaozingatia vyeti bila kujali uzalishaji unaotokana na huyo mwenye vyeti husika. Mishahara yake si yakuvutia kulingana na sekta binafsi.

Bank ya posta naona inajitanua na kuanza kuwa mbadilishaji fedha mkuu lakini ukiwaangalia watoa huduma katika benki hii hawawezi kuchukua kasi iliyokuwa inafanywa na bureau de change zinazofungwa kwa kasi. Badala ya kuisadia benki hii tumezalisha biashara haramu ya ubadilishaji fedha. Lakini pia huduma nyingine za kibenki hazileti ushindani kwa sabababu shirika halipo kibiashara

Fast jet imekufa kupisha ATC wakati mashirika haya yote yalipaswa kufanya kazi pamoja kwa sababu yanalipa kodi

Pamoja na Nia nzuri ya serikali ninaona Kama tunatumia fedha nyingi kwenye mashirika haya lakini akija mtawala mwingine atapuuza juhudi za mashirika haya na kuja na mipango mipya na hivyo serikali kuendelea kupata hasara.

Kama serikali ya Sasa imeweza kuua miradi mingi iliyoanzishwa na hawamu zilizopita ikiwemo mradi wa DART na Shirika la utangazaji basi lazima tuchukue taadhari kuweka mafedha kwenye mashirika ya umma na kuyajengea uwezo wa ushindani yajiendeshe yenyewe.

Kutumia dola kuboresha mashirika hakuyajengi yakawa imara bali yanapaswa kuacha yasimamame kushindana na sekta binafsi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kinyungu

JF-Expert Member
Apr 6, 2008
10,792
2,000
Ujamaa ni mfumo wa maisha ulioshindwa popote pale duniani ambako wamejaribu kuutumia. Ujamaa upo kinyume na hulka ya mwanadamu. Wale wanaotaka kuturudisha huko wamejiandaa kushindwa kabla ya kufanikiwa kutufikisha kwenye huu ujamaa-mamboleo wao.
 
Shark

JF-Expert Member
Jan 25, 2010
26,834
2,000
Jana nilienda kubadili fedha za kigeni kwenye benki moja hivi. Rate ilikua mbaya ajabu ila ndo iliyowekwa, kutoka hapo mbadala wake ningepaswa kuifuata benki ingine kilometa kadhaa, ningetumia muda na mafuta labda so nikawa sina jinsi. Ushindani wa Bureau De Change haupo tena, ni mwendo wa kupangiana tu rate. Benki nako foleni ajabu. Hii ndo Tanzania tuliyopo now.
 
TIBIM

JF-Expert Member
Dec 1, 2017
8,022
2,000
Mjamaa ana ABC za uchumi keshafail kama alivofail Nyerere na ujamaa wake,dunia imebadilika sana.Tunarudia makosa Yale Yale aliyofanya Nyerere toka lini mswahili akafanya chenye tija,tumeshindwa mwendokasi ndo tuweze hayo. Wangeeachia competition itawale wabaki kukusanya mapato ,utoaji tu hela wa kuyaendesha hayo mashirika ni shida wanachojua ni kukamua Maziwa tu kulisha hawawezi.
 
PTER

JF-Expert Member
Dec 28, 2014
13,847
2,000
Serikali ya awamu ya Tano inatengeneza mazingira ya ujamaa kwa nchi yetu na kututoa kwenye mixed economy.

Mashirika hayo hapo Juu yanafufuliwa kwa kasi lakini ufufuaji wake si wa ushindani bali ni kupitia kuwadhibiti washindani wao kwa kutumia dola ili wateja wahamie kwenye mashirika hayo.

Ni wazo zuri kuwa na mashirika ya umma ila ni vyema kuwa na mashirika ya umma yaliyoibuka na kukuwa kupitia ushindani wa wazi. Ukibebwa na kulipiwa kila kitu hauwezi kuwa imara bali unaandaliwa kuwa mtegemezi.

Mashirika ya simu yanaandamwa kuilinda TTCL ambayo ubunifu wake ni mdogo Sana lakini pia pesa za uendeshaji hazipangwi na kundi la wataalamu ndani ya shirika bali Hadi wapate ruzuku kutoka serikalini. Watendaji siyo wabunifu kwani ajira zake zinafuata mfumo wa serikali unaozingatia vyeti bila kujali uzalishaji unaotokana na huyo mwenye vyeti husika. Mishahara yake si yakuvutia kulingana na sekta binafsi.

Bank ya posta naona inajitanua na kuanza kuwa mbadilishaji fedha mkuu lakini ukiwaangalia watoa huduma katika benki hii hawawezi kuchukua kasi iliyokuwa inafanywa na bureau de change zinazofungwa kwa kasi. Badala ya kuisadia benki hii tumezalisha biashara haramu ya ubadilishaji fedha. Lakini pia huduma nyingine za kibenki hazileti ushindani kwa sabababu shirika halipo kibiashara

Fast jet imekufa kupisha ATC wakati mashirika haya yote yalipaswa kufanya kazi pamoja kwa sababu yanalipa kodi

Pamoja na Nia nzuri ya serikali ninaona Kama tunatumia fedha nyingi kwenye mashirika haya lakini akija mtawala mwingine atapuuza juhudi za mashirika haya na kuja na mipango mipya na hivyo serikali kuendelea kupata hasara.

Kama serikali ya Sasa imeweza kuua miradi mingi iliyoanzishwa na hawamu zilizopita ikiwemo mradi wa DART na Shirika la utangazaji basi lazima tuchukue taadhari kuweka mafedha kwenye mashirika ya umma na kuyajengea uwezo wa ushindani yajiendeshe yenyewe.

Kutumia dola kuboresha mashirika hakuyajengi yakawa imara bali yanapaswa kuacha yasimamame kushindana na sekta binafsi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ujamaa haujawahi kufanikiwa popote duniani.
Matokeo makubwa ya ujamaa ni kama yafuatayo.
1 kufukarisha watu
2 watawala kuwa miungu watu
3 uvunjifu wa haki za binadamu
4 uonevu kwa wananchi
5 kudumaza fikra kwa jamii
Na mengine mengi yenye chembechembe za uovu.

Kifupi ujamaa ni mfumo unaohalalisha uovu wa kidola.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Zawadini

JF-Expert Member
Feb 2, 2012
1,452
2,000
Wacha wamalize akija mwingine atakuja na mfumo mwingine. Hii ndo Tanzania
 
barafu

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
6,692
2,000
Jana nilienda kubadili fedha za kigeni kwenye benki moja hivi. Rate ilikua mbaya ajabu ila ndo iliyowekwa, kutoka hapo mbadala wake ningepaswa kuifuata benki ingine kilometa kadhaa, ningetumia muda na mafuta labda so nikawa sina jinsi. Ushindani wa Bureau De Change haupo tena, ni mwendo wa kupangiana tu rate. Benki nako foleni ajabu. Hii ndo Tanzania tuliyopo now.
Mkuu,kwamba sasa pesa ni lazima ukabadilishie Bank?Ina maana zile Bureau za Kkoo na Posta zimefungwa?Hii habari chungu sana
 
sblandes

JF-Expert Member
Apr 25, 2010
5,398
2,000
Shida mmoja kubwa makampuni binafsi yanakuwa na vipaumbele vyao,
kwa mfano wazawa kuhudumia ndege zao ni wachache na kazi nzito kama marubani na ma engineer ni wageni.
Vivyo hivyo wahindi waliomiliki reli mswahili alitupwa nje.
Miaka ya nyuma wazawa chini ya serikali ya Nyerere walipata mafunzo mbambali ya kuendesha taasisi za umma.
Lakini baada ya taasisi za umma kuuzwa kwa watu binafsi hakuna mafunzo yakina hasa kwenye ufundi mitambo n.k
Tukiwaachia watu binafsi kila kitu tutabakia na nini?
 
Ndyali

JF-Expert Member
Nov 24, 2011
1,488
2,000
Hospitali za binafsi zimewekewa kitanzi, shule za binafsi zinahujumiwa, vyuo na vyuo vikuu binafsi full mizengwe, vyombo vya matangazo binafsi vinalazimika kutangaza matangazo ya kusifu sifa kulazimishwa, vya vya upinzani halisi vimetungiwa Sheria ya kuharamishwa. Tulioishi maisha ya enzi za ujamaa tunaiona Tanzania ikitumbukia kwenye shimo refu bila kujali madhira yaliyotupa huko nyuma.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom