Tsvangirai awakana mabalozi wa Mugabe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tsvangirai awakana mabalozi wa Mugabe

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MziziMkavu, Oct 13, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Oct 13, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  [​IMG]Rais Robert Mugabe na Bw Morgan Tsvangirai


  Waziri Mkuu Morgan Tsvangirai amewaandikia viongozi duniani akisema mabalozi wa Zimbabwe hawaiwakilishi serikali yake.
  Alisema wawakilishi hao wameteuliwa tu na Rais Robert Mugabe, ambapo Bw Tsvangirai anagawana naye madaraka.
  Lakini Bw Tsvangirai alisema hakushauriwa katika uteuzi huo, ambapo anasema inavunja makubaliano ya umoja wa serikali.
  Haijajulikana iwapo Umoja wa Ulaya, Umoja wa Mataifa na Afrika Kusini itawatambua mabalozi hao.
  Hizi ni ishara za mpasuko zilizojitokeza hivi karibuni katika makubaliano ya kugawana madaraka, huku uchaguzi ukitarajiwa kufanyika mwakani.
  Wiki iliyopita, Bw Tsvangirai alimshutumu Bw Mugabe kwa kukiuka makubaliano baada ya kuteua wengine wengi bila kumshirikisha.
  Msemaji wa Bw Tsvangirai Luke Tamborinyoka aliiambia BBC siku ya Jumanne, "Hao si mabalozi- ni vibaraka wa Zanu-PF."
  Lakini alikataa kusema Bw Tsvangirai angependa hatua gani zichukuliwe na serikali za kigeni.
  Alisema, "huo ni uamuzi wao".
  Bw Tsvangirai alikutana na wanadiplomasia mjini Harare kuelezea msimamo wake.
  Pia aliziandikia nchi za Italia, Sweden na Uswizi, kuhusiana na mabalozi wa Zimbabwe katika nchi hizo.
  Kiongozi wa Movement for Democratic Change hivi karibuni alilalamika juu ya vurugu zilizofanywa wakati wa mikutano ya umma wakikusanya maoni ya katiba mpya.
  Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch limewashutumu wafuasi wa Zanu-PF kwa kuhusika na mashambulio hayo.
  Bw Mugabe na Bw Tsvangirai, ambao wamekuwa wapinzani kwa muda mrefu, wamekubali kugawana madaraka baada ya ghasia za baada ya uchaguzi wa mwaka 2008.
  Katika makubaliano ya serikali ya muungano, wanasiasa hao wawili walikubali kutengeneza katiba mpya itakayofuatiwa na kura ya maoni, halafu uchaguzi mpya.


  chanzo: BBC Swahili - Habari - Tsvangirai awakana mabalozi wa Mugabe
   
 2. K

  Kekuye Senior Member

  #2
  Oct 13, 2010
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 116
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hii inazidi kudhihirisha ni kwa jinsi gani demokrasia tunayojaribu kuifuata haina manufaa kwa nchi za Afrika. Ukweli serikali mseto, shirikishi, jumuishi, n.k hazifanyi kazi zinazowaendeleza wananchi zaidi ya kuishia kulumbana bila sababu. Sasa hapo ni suala la uteuzi wa mabalozi peke yake, itakapofikia mabadiliko ya katiba itakuwaje?
   
 3. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #3
  Oct 14, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  hahaaa Mugabe bwana..usiwe kama CCM
   
 4. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #4
  Oct 14, 2010
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,584
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Tsivangirai alifanya kosa kubwa kuingia serikali ya pamoja na king'ang'anizi Mugabe. Sasa inakula kwake.
   
Loading...