Tsh Milioni 15 inaweza kujenga nyumba kama hii?

Unaweza,muhimu kama ni muajiliwa fanya kazi hii wakati wa likizo,namaanisha usimamie wewe mwenyewe.
Ila kabla hujaanza kununua chochote,fanya research ya vifaa vya ujenzi ujue bei zake.


Mafundi wengi wanatupiga sana tunapowaamini,ila sio wote.
Humu ndani pia kuna watu wengi wamejenga,omba msaada wa fundi mzuri na mwaminifu kulingana na eneo husika.
All the best.
 
Shukran sana bro
 
Wakuu poleni na majukumu
Naomba kuhuliza kwa budget ya milioni 15 naweza kujenga nyumba kama hii?? ukitoa gharama ya kiwanja

View attachment 1859739
Kuna vigezo vingi ndugu. Hapa kuna suala la mahali ulipo. Ujenzi Kigoma si sawa na Arusha, Dodoma, Dar , Morogoro n.k. Pia, kuna material utakazotumia. Kwa mfano, aina za tofali zinatofautiana ubora na bei. Bati halikadhalika zinatofautiana sana. Kuna ufundi pia. Mafundi wa aina gani utatumia. Utafuta taratibu za ujenzi kuanzia hatua ya awali? Mfano, ramani rasmi ya ujenzi ama zile zetu za kienyeji tu tunamwambia fundi fanyafanya ujuavyo?
 
Ndio box kwani vipi
Wewe huwajui Wabongo? Kwao ramani nzuri ni ile yenye konakona na unakuta kona nyingi lakini hazina maana yoyote. Mimi napenda hayo maboksi sasa ingia ndani ndio utajua kuna ramani au hamna.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…