Tsd majukumu yake ni yapi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tsd majukumu yake ni yapi?

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by segwanga, Sep 27, 2011.

 1. segwanga

  segwanga JF-Expert Member

  #1
  Sep 27, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 2,790
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Wadau heshma kwenu
  Nimepewa assignment na katibu wa mnoko wa Teachers service department (TSD) wa pande nilipo eti hawezi kupokea fomu zangu za kuomba tsd namba bila kujua majukumu ya tsd.Great thinkers nisaidieni
   
 2. figganigga

  figganigga JF-Expert Member

  #2
  Sep 27, 2011
  Joined: Oct 17, 2010
  Messages: 14,975
  Likes Received: 6,613
  Trophy Points: 280
  ni taasisi ndani ya wizara ya elimu.
  1.kumfukuza na kumwajiri mwalimu kazi
  2.kumsimamisha mwalimu kazi au kumpa nusu mshahara.
  3.inaongeza vyeo vya walimu na kupandisha mishahara
  4.kuingia mkataba na walimu wapya kwa niaba ya serikali.
  kwa ufupi ndivyo niujuavyo.mia
   
 3. HAZOLE

  HAZOLE JF-Expert Member

  #3
  Sep 27, 2011
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 1,332
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  figganiga upo sawa. tatizo nini segwanga?? pia tafuta public service act itakusaidia kujua taratibu nzima za utumishi wa umma.
   
 4. SG8

  SG8 JF-Expert Member

  #4
  Sep 28, 2011
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 3,204
  Likes Received: 264
  Trophy Points: 180
  Haipo chini ya Wizara ya Elimu bali ni Idara ndani ya Ofisi ya Rais-Tume ya Utumishi wa Umma.
  Kazi zake zipo kwenye Public Service Act ya 2002 as amended in 2008, Kanuni za Utumishi za mwaka 2003 na Teachers Scheme of service.
  1.Kusajili Walimu (waliosoma na kufuzu)
  2.Kushughulikia masuala ya nidhamu na maadili ya watumisihi wa kada ya ualimu
  3.Kushughulikia mambo ya mirathi za walimu
  4.Kuandaa na kutunza tange (seniority list) ya walimu wote waliopo katika utumishi wa umma.
  5.Kupandisha walimu vyeo kwa kadri ya bajeti na mapendekezo ya mwajiri kupitia vikao vya kisheria
   
 5. figganigga

  figganigga JF-Expert Member

  #5
  Sep 28, 2011
  Joined: Oct 17, 2010
  Messages: 14,975
  Likes Received: 6,613
  Trophy Points: 280
  mkuu Gerrard asante kwa kunifumbua macho.mimi nilikua naijua jujuu.ni aktika hali ya kupeana mwanga.hata wewe upo sahihi kabisa.ngoja niendelee kufuatilia mambo yao.asante sana.mia
   
 6. segwanga

  segwanga JF-Expert Member

  #6
  Sep 28, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 2,790
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Greater thinkers nawashukuru na nitaendelea kuwashukuru kwa michango yenu.Niende mbele kidogo kwa kuelezea kisa cha mimi kuambiwa mpaka nijue majukumu ya tsd ndio fomu zangu zipokelewa.
  Nilienda ofsi za tsd nikiwa nimevaa t-shirt (nzuri tu) na suruali ya kadet (nzuri pia) na ndipo msala ulianzia hapo. Nikaambiwa hayo mavazi hayatakiwi kwa mtumishi wa serikali.Mi nikajitetea nikasema ninapokuwepo kazn kwangu sivai hvyo.Akaniambia hata hapo (ofsi za tsd) niko ofsin kwangu na mm nikamkatalia na ndo chanzo cha kutoelewana.Wadau tuhabarishane hilo ni kosa?
   
 7. SG8

  SG8 JF-Expert Member

  #7
  Sep 28, 2011
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 3,204
  Likes Received: 264
  Trophy Points: 180
  Mkoa gani huo Mkuu? Hata hivyo jambo la msingi sio mavazi ya kiofisi ila mavazi rasmi na T-shirt sio vazi rasmi labda kwa watu kama bank na NSSF kuna siku kama Ijumaa au J'mosi wanavaa T-shirt (sare). Kuna waraka wa mavazi kwa mtumishi wa umma, tafuta na usome utajua kwanini huyo Katibu alikusumbua. Kuna Mwalimu alikwenda kwenye semina ya kusimamia mitihani ya darasa la saba akiwa na rasta jamaa wakambana sana. Alijitetea akidai ni dini yake, Afisa Elimu kimya kimya akfuatilia mkataba aliojaza akiwa wilaya nyingine ikathibitika jamaa alijaza dini yake kama Mkristo basi ikala kwake
   
Loading...