Truth about Ebola

Elli...nakubaliana nawe kuwa kuna uwezekano kuwepo kwa agenda ya siri juu ya misaada tunayopokea toka kwa watu wa Marekani, labda kwa mrengo wa kutunyonya, labda kama anavyotuambia 'mkuu' "kula uliwe"...lakini nachelea kuamini kuwa agenda ya siri hiyo ni 'population control', tena kwa kutumia vita ya virusi! Na pia hoja yako imelalia kwenye 'development prgrammes', yangu imelalia kwenye service delivery, japo zote kwa njia moja ama nyingine zinaiengiliana. Bajeti yetu ni tegemezi, ni hali ni mbaya zaidi kwa bajeti ya Wizara ya Afya ambao hawapati hata 'Robo' ya bajeti yao ya mwaka...ni utani kubeza mchango wa development partners wakiwemo waMarekani kwenye kupunguza vifo nilivyotaja hapo awali. Tumeshafikia malengo ya milenia ya kupunguza vifo vya watoto, na japo JK alipokea tuzo...haikuwa juhudi za serikali bali wahisani!
 
Last edited by a moderator:

Nafikiri kwa namna moja ama nyingine tunakubaliana japo tunatofautiana kwa baadhi ya mambo. Nakubali kuwa hatuwezi kuubeza mchango wao kwenye "maendeleo" lakini pia tukubali kuwa misaada mingi inabeba ajenda ya siri. Kama sio depopulation ya moja kwa moja basi at least ile itakayoonekana in 20 or 30 yrs to come.
Asante
 
Last edited by a moderator:
Elli79 hivi unajua watu kama Riwa ndio wako wizarani huko na ndio wako kwenye nyadhifa zakuja kufanya maamuzi ajili ya wananchi. Mwafrika ambaye mpaka leo hii anaamini misaada ya Western World eti inaletwa kwa ajili ya kutusaidia huwa namdharau sana. Riwa nakudharau sana mkuu.

Naomba kwa kuanza tu usome kitabu kinaitwa The Confessions of An Economic Hitman kimeandikwa na mzungu by the way. Deception inaonekana umesoma mambo mengi, sijui ni vipi tunaweza elezea ndugu zetu waelewe ni nini conspiracy theories na ni nini ukweli.

Huyu ndugu Riwa ana uelewa mdogo sana lakini embu ngoja nijaribu kuongea nae pole pole labda nitaweza mfumbua macho angalau kidogo.


Ndugu, mradi ukiwa sponsored na hao wazungu wa kupunguza vifo e.t.c. project managers mara nyingi wanatoka wapi? Je vifaa vinavyotumika na dawa mnazopewa na nyenzo mnazopewa za kupambana na hayo majanga zinatoka hapa kwetu au kwao huko huko?

Nikupe mfano hai tu wa sasa hivi. Si kuna hii chanjo ambayo imeletwa ya Rubella, kupitia GAVI alliance.
Hii hapa chini ni link ya mchanganuo wa cost za project yenyewe:

http://www.gavi.org/Country/Tanzania/Documents/DLPAs/Decision-letter-NVS-Tanzania-2014/


Sasa, unaona budget ya mradi mzima ni zaidi ya USD million 16. Hio ni zaidi ya billion 22, ukishuka mpaka jedwali la 11, utaona mchanganuo wa jinsi hio hela itakavyotumika na jedwali la 12 inakwambia Procurement Agency ni UNICEF tu na hakuna self procurement.
Hii ina maana gani? Hii ni kwamba almost 90% if not 100% ya hio hela itapewa UNICEF kununua vitu. Na utaona vitu vyote hivyo vitatoka kwenye kampuni yenye uhusiano inderectly na GAVI. HIZO HELA ULIZOSAIDIWA ZINARUDI ZOTE KWAO!!


Sasa hilo haliishi hapo tu, huo "msaada" wa mabillioni upo kwenye kumbukumbu za hawa watu, inafika kipindi wanamfwata raisi na kumwambia "unaona miaka hii mi5 ya nyuma tumetoa misaada ya usd bill 50, tunajua tukiwauzia hamwezi kulipa, ila tunawasaidia. Sasa bwana kuna kampuni yetu ni wataalamu sana wakuchimba gesi au thahabu, embu iachie hii kampuni iingie kuchimba halafu tutaangalia namna ya kusamehe madeni na kuleta "misaada" zaidi. Hii kampuni pia itakuongezea sana pato la taifa bwana, kwa million 1 kwa mwezi, na wewe tutakuingizia million kadhaa kwenye akaunti yako na wenzako huko akaunti zenu za ulaya.

Refer kauli hii "UKITAKA KULA SHARTI ULIWEE!" Sijui unakumbuka alisema nani.

Tulivo wajinga, tunatoa mali zetu, na sababu hatuna utaalamu wowote tunaibiwa mara 100 ya thamani wanosema wanapata, huku tukiendelea kukenua meno na kuwashukuru hawa watu kwa misaada na roho nzuri waliyonayo! Tumepewa "msaada" wa billion 22, malipo yake ni billion 220.

Sasa unaweza ukadharau mfano wangu ndio maana nimekwambia usome hicho kitabu ambacho ni true story. Confessions of an Economic Hitman, upanue wigo wa uelewa wako.
Utajiri wa nchi za magharibi hauwezi ukawepo bila umaskini wa Africa na Latin America.

Kuhusu EBOLA, main aim sio population control, hapana, hilo limekua taken care of na HIV ila jiulize kwa nini mlipuko wa ugonjwa huu "wenzako" wakatuma wanajeshi elfu 4? Hao wanajeshi wanaenda kutuliza ugomvi wa nani na nani au wanaenda piga EBOLA na risasi. Ni vurugu gani itakayoweza amka katika watu wanoumwa na ikahitaji askari?
Ile ni strategy ya Mmarekani kuwa na military presence West Africa. Na je unafikiri kwa nini Mmarekani atake military presence West Africa? Nitakuacha hapa ujaribu kutumia akili yako na wewe.

Please Riwa think beyond kidogo, kidogo tu uone ni jinsi gani hawa watu wanaweza na kuendelea kuweza kutucontrol kijinga sana na sisi kuwa wajinga zaidi.
florence natumaini mfano wangu hapo juu kidogo utasaidia usi changanyikiwe. Kama bado uliza.
 
Naomba ufafanuzi "service delivery" ina utafauti gani na "development programmes"?
Naomba pia unijulishe, katika nchi tuilizokua nazo sawa na zingine actually zilikua "chini" yetu kiutajiri miaka ya 60, ni ipi imefanikiwa kupiga hatua zaidi yetu kwa kutegemea misaada ya nchi za magharibi.
Chukulia mfano, South Korea, Malaysia, China, India e.t.c. nani hapo maendeleo yake yaliletwa kwa "misaada" ya wahisani?
Hivi kwanini tuanjidharau hivi na kuona kuwa sisi hatuna uwezo wa kutatua matatizo yetu mpaka mtu mweupe ndio aje kututatulia? Kwanini hatuamni kuwa tunaweza fundisha wauguzi sisi wenyewe, tunaweza boresha maabara zetu sisi wenyewe, hivi Riwa hao wazungu unawaona ni miungu wadogo wadogo hapa duniani?

Tumekubali kupokea chanjo ya Rubella lakini hakuna taasisi yetu hata moja, iwe NIMR, Ifakara au Muhimbili iliyofanya tafiti ya kuthibitisha uhitaji wetu wa hio chanjo. Na je kuna idara yetu hata moja itakayo chukua hio chanjo na kuipima kuthibitisha kama kweli ni chanjo ya Rubella au kwa sababu imetoka tu ulaya basi lazima itakua inafaa?

Kilio changu ni kwanini hatuji na solution zetu wenyewe na tuendelee kuamini mpaka leo kua solution zetu zitaletwa na wazungu wakati makarne kwa makarne mpaka leo tunashuhudia tunavyo nyonywa na tunaona nchi zilizo amua kuachana na utegemezi huu zikipiga hatua!!!??

AMKA MWAFRIKA, UNAWEZA!!
 
Mkuu Nyamgluu umenikumbusha jambo hapa kuhusu watu wanaoitwa Expatriates yaani ukiangalia pesa wanayokula kwa mwezi unakuta wao wenyewe ni Project tosha, kwa mfano, sitataja jina ila kuna NGO moja ya hao hao ambao house rent pekee ni Usd 60,000 kwa mwaka, Ada za watoto wake kwa mwaka pale IST ni Usd 39,000, yeye salary yake ambayo tena haikatwi kodi ni Dola 12,000, na gari ya ambayo haujui mafuta wala service, simu ni postpaid na kwa mwezi si chini ya million bili ikija. Amepewa laptop ya Mac yenye thamani ya million Tatu, na iPhone. Hebu Nipigie faster hesabu kwa mwaka ni kiasi gani analipwa huyu mtu.

Ukija kwenye Procurement kuna policy kabisaaaa inaitwa Buy American yaani huruhusiwi kununua bidhaa ambazo si za Marekani, kwa mfano, magari lazima ukitaka kununua Toyota sharti upate kitu kinaitwa Waiver kutoka USAID

Kuna vitu vinaitwa NICRA hii hubaki HQ kwajili ya kuendeshea ofisi. Wao wakija kutembelea ofisi wanalala Seacliff na kwengineko kwenye gharama za juu

Sasa tunaelenga kusaidiwa au kuwasaidia wao?
 
Last edited by a moderator:

Am the one who like to know what is behind the curtain in all those disease you mention above and how to avoid it if possible.I think,it is better to make open for many without fear any argument from people who will not agree with you.
 
waswahili wanasema lisemwalooo....:A S wink:
 
Halafu kumbuka Elli mwisho wa siku huo "msaada" ni deni kwetu!

Ila sasa hapo kuna akina sisi, umepata ki channel hapo ukapewa shavu unakunja vi dola elfu 3 au 4 kwa mwezi aaaa unaona wakombozi si ndio hawa bwana! Unasimamisha kajumba kako mdogo mdogo heshima bar unaona ume win.
Bila kujua wenzako wana grand plan za kizazi chao chote kwa miaka 200 ijayo, wewe umejifikira wewe, bia ya weekend na kiaka 20/30 ijayo ukistaafu (kama basi umekumbuka kufikiri mbali hivyo).

Wakija tena na plan yao ya "msaada" wewe msomi mzima na Masters/PhD yako ya virology/parasitology/epidemiology/ e.t.c. unawekubali tu bila kudadisi kwa umakini unacholetewa na kuendeleza maangamizi ya watu wako.

Hawa jamaa, wametuweza sana. Ila mkuu, mimi kidogo nafarijika na the likes of Uhuru na Kagame. Japo kweli nao wanamapungufu mengi tu na mambo mengine ambayo sikubaliani nao, lakini na wasifu kwa kutambua kua ukombozi utakuja kutoka sisi wenyewe.
Kuna ripoti niliona investment Kenya iliyoingiza kwenye R & D ya dawa zao za asili nili staajabu sana. Sisi sasa kitengo chetu cha utafiti wa dawa asili pale muhimbili utakionea huruma.

Ila mimi mkuu, I am taking matters in my own hands, nimeona kwa kuingia kwenye siasa sitaweza leta hata ka influence kidogo, hivyo ninajaribu kuleta mabadiliko privately. Na changanya mihangaiko yangu ya private business na kuingiza idea na vimchango kwenye sekta ninazo believe in. Na pia tunaongezeka hapa Tanzania watu kama mimi amabo tumeshachoshwa na siasa na tunaamini siasa haitakua mtatuzi wa matatizo yetu, inabidi tuanze sisi kwanza!

Hasta la victorie siempre!!
 
Last edited by a moderator:
Mimi siwalaumu wazungu kabisa! Lawama zote ni sisi wenyewe kwa nini tuwategemee wazungu? Kwa nini tusiinvest kwenye research na science? Wakija na misaada yao ya kijinga tuwatumie lakini tunawatetemekea kama miungu watu!
 
Kuhusu EBOLA, main aim sio population control, hapana, hilo limekua taken care of na HIV ila jiulize kwa nini mlipuko wa ugonjwa huu "wenzako" wakatuma wanajeshi elfu 4? Hao wanajeshi wanaenda kutuliza ugomvi wa nani na nani au wanaenda piga EBOLA na risasi. Ni vurugu gani itakayoweza amka katika watu wanoumwa na ikahitaji askari?
Ile ni strategy ya Mmarekani kuwa na military presence West Africa. Na je unafikiri kwa nini Mmarekani atake military presence West Africa? Nitakuacha hapa ujaribu kutumia akili yako .[/QUOTE]

hapo ndo nnapojiuliza zaid
 
[/
QUOTE]
Kuhusu EBOLA, main aim sio population control, hapana, hilo limekua taken care of na HIV ila jiulize kwa nini mlipuko wa ugonjwa huu "wenzako" wakatuma wanajeshi elfu 4? Hao wanajeshi wanaenda kutuliza ugomvi wa nani na nani au wanaenda piga EBOLA na risasi. Ni vurugu gani itakayoweza amka katika watu wanoumwa na ikahitaji askari?
Ile ni strategy ya Mmarekani kuwa na military presence West Africa. Na je unafikiri kwa nini Mmarekani atake military presence West Africa? Nitakuacha hapa ujaribu kutumia akili yako .[/QUOTE]

hapo ndo nnapojiuliza zaid
 
Nyamgluu ... ahsante sana kwa dharau zako..na hongera sababu we ni mjuaji wa kila kitu. Point of correction: Sifanyi kazi wizara ya Afya, Sijawahi kufanya kazi wizara ya Afya...niliacha kazi serikalini 10 years ago na sijawahi fanya tena kazi serikalini. Lakini kwa capacity yangu, nafanya kazi kwa ukaribu sana na serikali na development partners through DPG-Health. I know what I am talking about..even the inside infos that I can not publicly share. We baki unachonga domo tu hapa JF na facts zako za google na kudharau watu. Huna faida wala msaada wowote kwa hii nchi ambayo wazalendo tunaipigania, kadri tuwezavyo kwa nafasi zetu. Endelea kunidharau...kwani hata heshima yako haina faida yoyote kwangu!
 
yaani mwaniacha kwenye box sielewi tena chochote
 

Hehehe ume panic brother!
 
Mushi92 na MBEBA MAONO KAJA Meljons

Nitaelezea hapa kidogo lakini msimeze tu navyovitoa bila nanyi kujishughulisha kidogo. Nitakuwa nawaelezea huku nikiwapa link za kudadavua zaidi wenyewe pale nitakapoweza. (Japo nasengenywa na data za google, hehehe)

Nianze hivi:

1. Mnajua kwa sasa China imeipita USA na kuwa nchi yenye uchumi kubwa zaidi duniani. Hizi data zinatoka IMF na sio propaganda. Fwata habari hii hapa chini upate link zaidi

China Just Overtook The US As The World's Largest Economy | Business Insider India

Sababu kubwa ya China kuweza kuipiku USA kiuchumi ni walivyoweza kutumia mishahara yao midogo (low wages) kuweza kuwa kiwanda cha dunia. Western Countries bila kujitambua walishangaa waChina wamekua na akili na technical know how kubwa sana na mishahara yao midogo sana, hivyo cost zakitengeneza mfano kijiko zinakua ndogo sana China ukiringanisha na kutengeneza kijiko hicho Marekani hata kama unakuja kuuza Marekani hio hio.
Muda si mrefu makampuni karibia yote ya ulaya na marekani yakalazimika kufanya uzalishaji China, ili yaweze ku survive in the business market.
Capitalism ilirudi kuwaumiza waanzilishi wenyewe wa Capitalism. Wanajuta!

Sasa kwa kufupisha ni hivi, Marekani haiwezi kushusha minimum pay yao ili iweze kupambana na uzalishaji wa China, HAWAWEZI!
Vichwa vikakaaa na kutafakari watafanyeje?

Source kubwa ya energy kwa ajili ya kuendesha viwanda na uzalishaji ni nishati ya MAFUTA, na hali ilivyokuwa Marekani hawezi shindana na CHINA kununua mafuta, Mchina ana hela zaidi!! Na Mchina alikua tayari kununa mafuta Iraq na Libya kwa bei kubwa sana, sababu hela anayo.
Sasa imagine wewe ndio Marekani, kuna factors kubwa 2 za uzalishaji 1 ni wafanyakazi 2. source of energy au chanzo cha nishati
Sasa basi wafanyakazi unao lakini huwezi shusha mishahara sababu maisha tayari yako juu, wafanyakazi wako wamezoea mishara mikubwa na maisha mazuri, pili huna uwezo wa kununua mafuta kwa bei ya soko huria, na nchi yako inazidi kudidimia kiuchumi kila kukicha, viwanda vinafungwa uzalishaji unadidimia. Ungefanya nini??
Fikiri kidogo.
...
...
...
...
...
Ni hivi..
Mmarekani akaamua kutumia kitu kimoja tu alichobaki nacho kama namba 1 duniani, nacho ni JESHI! Hivyo basi, tuanzishe vugu vugu la mapinduzi arabuni kote, kwa uongo wa kuleta Demokrasia, Kutokomesha Terrorism nakadhalika machafuko yakiendelea sisi tunaendelea kuwauzia hao waarabu silaha huku tukiiba mafuta na yale tutakayo shindwa iba tutawaambia watulipe silaha tunazowapa kwa mafuta. HICHO NDICHO KINACHOTOKEA UARABUNI!!

Waliingia Iraq kwa kisingizio cha WMD, hatujaziona. Wakamuua Saddam wa watu bila huruma eti kisa aliua kurds na wakasema wanaleta demokrasia. Iko wapi hio demokrasia sasa Iraq. Mbona Saudia hakuna hio demokrasia ila hawajaingia?
Wameingia Libya, wakamuua na Ghaddafi. Sababu ni nini? Embu jiulize, Gadaffi aliuliwa kwanini? Mnajua Libya ilikua nchi isiyo na deni lolote, umeme walikua hawalipi na wala kodi hakuna? Angalieni link hizi: (Msije lia tu)

LiveLeak.com - Facts About Libya Under Gaddafi That You Probably Did Not Know!

Ingieni hata wikipedia muone.
Haya basi hio Demokrasia wanayoileta iko wapi?
Jiulizi hizo silaha na risasi zisizoisha mpaka leo zinatoka wapi wakati hakuna viwanda vya silaha uarabuni?
Sasa wakati wao wanapiga, jamaa wanaiba mafuta, na vita ikiisha tu, kama basi itaisha hivi karibuni Mmarekani anakuja na deni la ma trillioni na kukwambia hili ni deni lako kwa vifaa tulivyotoa wakati wa vita. Mtatulipa kwa mafuta ambayo kampuni zetu za USA zitawasaidia kuchimba, tunawasaidia sababu ndio mmetoka kwenye vita tu jamani!

Anyways niachie hapo ila tambueni kuwa machafuko ya huko arabuni na afrika kaskazini mwa sahara ni kwa ajili ya wizi wa mafuta wa Marekani.

TURUDI HAPA KARIBU NA KWETU KWA WABANTU HAPO WEST AFRICA.

West Africa ina visima vya mafuta na hazina ya mafuta nyingi mnooo. Imekua ni nia ya USA kutaka ku control vyanzo hivi vya mafuta na rasilimali zetu kwa mda mrefu sana kuanzia enzi za ukoloni.

http://www.markswatson.com/afrioil.html

Ila wataingieje sasa? Maana kwa uarabuni wanatumia kete ya TERRORISM ili kuhamasisha na kushawishi wananchi wao wakubali nchi yao kwenda vitani Uarabuni. Terrorism imetengenezwa na CIA kwa faida ya Marekani, wale watu unaona wanachinjwa eti na kurushwa mitandaoni ile nitaongelea siku ingine.

Sasa basi, wataingieje West Africa na kui control, wanaume wakaanza kuumiza vichwa tena.
Mnakumbuka hii kampeni iliyozuka ghafla April nafikir:
Tuliona #BringBackOurGirls kila kona na dunia nzima utadhani hao BokoHaram wanashinda twitter na FB kuangalia comment zenu.



Ukweli ni kwamba ile kampeni ilikua feki tupu na propaganda kujaribu kutengeneza ushawishi duniani na hasa Marekani kuwa Boko Haram ni hatari, na jeshi la marekani linahitajika kusaidia kule WA!!
Hehehe hii mbinu ikagoma. Bahati mbaya, wamarekani wengi hawakuwajali sana wasichana mia 2 kiasi cha kuwa tayari kuruhusu Jeshi lao liende.

Basi ndio vichwa vikaja na EBOLA!!!!!!!!!
Sasa isingetosha tu kuwa na EBOLA huko mbali West Africa wananchi bado wasingekua na support kwa serikali yao kutuma Jeshi, kwahio chakufanya ni kuonyesha ya kwamba EBOLA INAWEZA KUJA MPAKA MAREKANI, SI MNAONA WATU WETU MPAKA HUKU MAREKANI WNAKUFAAA!!!!!


Obama mara moja akaagiza watumwe wanajeshi elfu 3 mia 9 kwenda kusaidia mlipuko!! NANI AIUNUE MDOMO KUBISHA, HUYO ATAKUA ENEMY OF THE STATE (ADUI WA NCHI!!!!)
Hao askari ni wakulinda maslahi ya mafuta ya Marekani yanayotoka WA, kiukweli mnaweza kufa kama inzi tu Mmareakni asijali sana, ila ni pale tu ambapo na yeye yuko hatarini. Koffi anan alisema hili juzi.


SASA MAREKANI ITAKUA INA UWEZO WA KUSHINDANA NA CHINA SABABU INAPATA NISHATI YAKE KWA GHARAMA NDOGO SANA IKITUMIA MABAVU NA STRATEGIC THINKING YA JUU!! MCHINA ATABAKI NA SILAHA YAKE YA PESA, LAKINI FOR HOW LONG?


Basi ndugu zangu hivyo ndio ambavyo mnaona jeshi la marekani limetua West Africa, na haliondoki leo wala kesho. Inawezekana kweli EBOLA ipo lakini sio tishio, tena hasahasa huko marekani kama tunavyolishwa kwenye vyombo vya habari!!!

Wenzetu wanafikira mbali sana kuhusu mistakabili ya nchi zao, achana na sisi tunaowaza kujishibisha matumbo wenyewe na kukata mauno jioni. Hawa jamaa wanapanga mikakati leo kwa vizazi vya miaka 200 mbele.

Kama una swali uliza natumaini kuna wakuu wengine hapa wako fiti kuelezea. Hivi vyote vinapatikana mtandaoni ukiwa mdadisi kidogo sana.

cc Elli BAK MziziMkavu Riwa Eiyer The hammer King Kong III Deception maziku Masunga Jr D 007

Na wengine.
 
Mpwa wangu Nyamgluu nimeisoma hadi kichwa kinanizunguka kwa hasira
 
Last edited by a moderator:
ebola ipo,ingekuwa not real wale manesi USA wasingeugua

wewe lazima ni mmoja wa wanaoamini kuwa sadam hussein alikuwa na silaha za maangamizi! Hao manesi USA uliwaona au ni kwa sababu ya news on cnn which can be created and staged? kumbuka CNN ndiyo hao hao waliopiga kelele sana kuhusu sadam husein.
 
Magonjwa yote ya kutisha hutengenezwa na yanatiba. Ni bahati mbaya lengo la watengenezaji ni kuwaangamiza watu weusi duniani.

ukienda america na ulaya mpaka chanjo ya malaria ipo ilhali hapa bongo hailetwi wakati ndipo kuna malaria mno. Tena kama europe au nchi zozote za weupe (majority) UKIMWI is not an issue ila kwa black majorities ni issue.
 
Halafu utasikia Mwafrika mwenzako anakwambia ni kwa sababu sisi waafrika tunawaza ngono tu mda wote na hatuvai condom! Unaweza mrukia kichwa aisee. Utingo umesoma kuhusu immunity ya ukimwi walionao wazungu kutokana na mutation ya protein CCR5?
Je ulishawahi kusikia Plague, au the black death iliyokumba ulaya karne ya 14?

Unajua inasemekana ilikua ni kirusi kama EBOLA!! Sasa imeanzeje ghafla WA?

Was Ebola Behind the Black Death? - ABC News
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…