Fixed Point
JF-Expert Member
- Sep 30, 2009
- 11,304
- 12,753
- Thread starter
-
- #21
that is exactly my point..... kwa nini useme uongo kuwa hutaonana na John wakati unaonana naye?Relationship is about compromise, sasa kama sababu za kutomuona John hazina mshiko na kama sitakufa nisipomuona John; basi for the sake of mahusiano na kumjengea confidence hubby basi sintamuona John. Ila kama ni lazima nimuone, nitamwambia na kumfanya aelewe kwanini l had to go n see john.
Mazingira ya kuaminiana yanakuwa cultivated kwakweli; lkn kukiwa na maswali mengi sana kwa tuvitu tudogo basi kunatoa room ya kudanganyana.
Katika swali linaloongoza kwa majibu ya UONGO ni UKO WAPI SASA HIVI?
well some people may see that question as very romantic lakini lina dalili ya kutokumuamini mtu kidizaini hivi.
ha haaa, haya babu.......Bahati mbaya mimi siyo mdau wa uongo usio na tija...
Huo wenye tija hata ukinaswa unasema kweli kwamba sikutaka kukuharibia mood...and you now that we have a great appointment tonight.....ni rahisi kueleweka IMO!!
Babu DC!!
ha haaa, kama unataka yawe kazi yatakuwa hivyo, lol!Mahusiano ni kazi sana!
Mtu asipo kuwa mwaminifu kwa kitu kidogo jua majanga hayo
Mahusiano ni kazi sana!
Kaunga no matter unamfahamu vipi mtu wako... Kwa kiasi kikubwa with time, circumstances with a combination of other forces wengine hubadilika. Kwa mfano tukio kama hili wewe unatoa ushauri upi?
Kuna wanandoa nawafahamu... The wife hana kasoro kama ideal wife anapaswa kuwa kwa mising ya vile ambavyo wengi huangalia... Ni msafi, mtulivu si mtu wa kuzurula, ni mpishi mzuri, a good mom and wife na mengine mengi. To the extent kuwa ndugu wa upande wa mke na mume wote wanampenda na kumridhia. Ana kasoro moja tu huyu dada - Tamaa! Na she has tastes ya expensive things... Ni spender mzuri sana. Tatizo lake hilo linafanya hata mumewe akimpa pesa ahifadhi; akiulizia hiyo pesa inakuwa imetumika on things ambazo si za msingi... Na haijalishe pesa ilikuwa kiasi kikubwa vipi.
Vikao vimekaliwa, utatuzi umetafutwa, 10 years in marriage mwanaume kaamua kukubali kuwa the wife ndivyo alivyo hawezi change. Kilicho baki sasa mumewe ana pesa sana, mkewe hana access hadi apewe na mwanaume hayupo open kabisa the money he has maana ikiwa tu disclosed tayari lazima pesa kubwa iombwe. Kuna cases nyingi but sasa hili ni baya saana, kuwa yule mtu ambaye ndiye alipaswa aelewe all the details ndiye anafichwa kuliko wote! WHY? Sababu ya mwenza na si mwanaume mwenyewe.
Umeeleza kwa kirefu sana rafiki na mengi ni ya msingi.......
ninachojaribu kukiangalia hapa ni je kama katika kudanganya kwako, kwa sababu yoyote ile ukakamatwa...... unakuwa umeweka wapi uaminifu wake kwako (wako kwake? kiswahili nacho kigumu!)?
ha haaaa, dada mdogo mahusiano yoyote yale, hata na shostito kamba zikiwa nyingi unaanza kujiuliza kulikoni mbona kila siku marope? sasa wewe shostito kama huyo inaweza tokea ukamwamini kwa chochote kile? hata kama this time anasema ukweli?dada mkubwa hivi mahusiano si ni pamoja na urafiki yani ule ushostito!!
sasa kama rafiki yangu au shosti yangu ananifunga kamba kila siku!kila siku yeye marope tu!yani hata sipumui!huo nao ni uongo uso na tija au?
manake wengine huwa tunaamini tuko waaminifu sana kiasi cha kushindwa hata kujiamini wenyewe!
aaaargh!
Poleni na majukumu wanaMMU...
Leo hili jambo la trust kwenye mahusiano limekuwa likijirudiarudia sana katika kichwa changu. Mahusiano mengi sana yanavunjika sababu ya kukosa uaminifu. Kuna vitu vingi nimekuwa nikijiuliza na kujijibu na vingine kukosa kabisa majibu. Kwa mtazamo wangu UAMINIFU ni jambo muhimu sana katika mahusiano. Mara nyingi napenda sana niwe katika hali ambayo namuamini mpenzi wangu, pia napenda sana kwa gharama yoyote ile kumfanya mpenzi wangu aniamini. Kama nikigundua ana wasiwasi na kitu ninachomwambia huwa najitahidi kumwuliza aniambie nifanye nini ili aniamini sababu sipendi akae akiwa na wasiwasi, na ukweli nitafanya hicho kitu ili tu aridhike.
Inawezekana mimi nipo complicated kidogo, huwa napenda sana mtu aniambie ukweli hata kama ni mbaya kiasi gani. Kwa kuujua ukweli nakuwa na uhuru wa nini la kufanya baada ya hapo.... kukusamehe na kuendelea na mahusiano au kukusamehe na kusitisha mahusiano (kusamehe kwangu huwa siyo option, lazima nisamehe ili niweze kuendelea na mambo yangu mengine).
Katika huu uzi nitazungumzia sana uaminifu wa mambo ya kawaida tu, siyo kutoka nje ya mahusiano (cheating). Utakuta sometimes mtu anaamua tu kudanganya kwa sababu yoyote anayoijua. Kwa mfano mtu anamwambia mpenzi wake naenda sokoni wakati anaenda salon, au naenda kwa dada wakati anaenda kwa shangazi.
Hivi ikatokea ndo upo kwa shangazi halafu dada akaja nyumbani kukuulizia wakati wewe uliaga kwenda kwa dada itakuwaje? hata kama kweli mpenzi ataamini kuwa ulikuwa kwa shangazi, utakuwa umejenga hisia gani kwake kuhusu wewe? kwa nini umdanganye?
Wenzangu mnalizungumziaje hili?
Karibuni kwa mjadala
Hilo swali kama kuna mwanamume haulizi basi huyo kabarikiwa....
Ila mwisho wake huwaumiza sana rohoni....from the man's perspective..!
Babu DC!1
ha haaa, kama unataka yawe kazi yatakuwa hivyo, lol!
Da Mkubwa, aksante kwa salamu jamani huyu FirstLady1 anajua ninavyomwonea wivu.............. haha. Ni kweli dada kama mpenzi ni mwelewa kuna uwongo mwingine ambao hauna tija sana sana hata akigundua kuwa unamdanganya atakushangaa. Na kwa nini utengeneza uwongo ilhali wajua kuwa mwenzio ukimwleleza atakuelewa? Ni hulka au?Da Mdogo MJ1, kwanza salamu zako sana toka kwa FirstLady1 hapo juu.... ujue tunakumiss sana......
nakubaliana kabisa na wewe hapo kwenye RED, kama si mwelewa........
Vipi kama mwenzio ni mwelewa? unakuwa unamkinga na nini kwa kumdanganya?
Katika huu uzi nitazungumzia sana uaminifu wa mambo ya kawaida tu, siyo kutoka nje ya mahusiano (cheating).
hapo kwenye RED sasa ndo adha ya uongo..... ukishaanza kuusema, ili mwenzio akuelewe, basi hiyo chain itaendelea..... there is no way utaokoka. kinachonishangaza tu ni kwa nini mtu ujiingize kwenye hiyo chain kwa uongo usio na tija? ule wenye tija labda, ingawa kwangu uongo ni uongo, wenye/usio na tija....Na mara nyingi watu hatimae hukamatwa... 🙂 Sasa hapo ndio hadithi nyingine kabisa...
Lets say kaongopa anaenda Sokoni na akagundulika kaenda Saloon..
Je huyo ni muongo mzuri to the extent anaweza toa uongo zaidi kujikomboa?
Oh' baba FB Saloon ninayo enda ni hadi appointment, nilipokua nikienda sokoni nilipigiwa simu kesho niliko panga appointment hawatakuwepo kama nikiweza niende leo; so nikaenda huko. Sababu nilisha kuaga nikaona hakuna haja nikusumbue.
Je ni manipulator na atatumia hiyo kama sababu ya kukulaumu wewe kuwa ndio umesababisha?
Baba FP tatizo wewe siyo mwelewa... Hivi hujui kuwa wake huwa tunasemwa kijiweni nani anatunzwa zaidi? Sasa wewe nikikuaga siku zote naenda saloon unasema nimezidi! Na mimi sitaki kukuangusha hapa mtaani napendeza kwa ajili kutukuza jina lako hapa mtaani. So naona bora nikudanganye ili nisikuumize lakini nihakikisha hapa mtaani RESPECT! Hata wakiona napita wasema mke wa baba FP Kapita...
Je atakuwa genuine na aombe tu msamaha ili yaishe huku akijustify?
Najua hupendi niende saloon mara kwa mara. Leo nimesikia kiharufu kitatoka kichwani kikanikosesha raha nikaona ni kheri nikaoshe...
Its not black and white so hapa sasa ni matokeo FP.
ha haaa, rafiki unanilazimisha twende huko, hakuna ubaya lakini.Hii sentensi ni kama vile imekaa kinyumenyume...!
Kama upo kwenye mahusiano (me & ke) in this case, kutokuwa mwaminifu ( au kuwa mdanganyifu), ni dalili KUU inayoashiria kuwa kuna "cheating"...! Au kwa maana nyingine "kutokuwa mwaminifu kwa mambo ya kawaida" kwa mwenza wako, maana yake ni kuwa upo njia moja kuelekea kwenye "cheating" au tayari una-cheat...!
Siku Njema
babu naomba nikuulize hivi kwann hili swali huwa mnalipenda sana ilihali linawaumiza??
Kaunga hebu nidadavulie what is IMO??