nguruka wa kig0ma
JF-Expert Member
- Jan 16, 2020
- 2,946
- 2,929
Saaalam wana JF,
Ndugu zangu, nimefuatilia maandamano nchini marekani ninejifunza jambo kubwa sana, mpaka nikajiuliza kwanini sisi Tanzania?
Kwanza nikamtathimini Trump, kwa amri ya kutumia polisi kuzima maandamano kisha jeshi. Nikaona hakuna tofauti na nchi yetu kwa sasa. Kila kitu jeshi, nikajiuliza nini maana yake (mwenye jibu tafadhali)
Cha tofuati nichokiona na kujifunza, polisi na JW wa marekani hawapigi watu, hawahoji watu barabarani, hawatishi kabisa, hatumii maji ya kuwasha, hatupi mabomu ya machozi. Ingelikuwa ni hapa kwetu wafu wangekuwa wengi kwelikweli zaidi ya vifo vya covid19, majeruhi hospitali zingejaa nako wangeambiwa wasitibiwe atakayewatibu kazi hana.
Nikalinganisha na wakati wa mgogoro gas ya Mtwara, Chinga waligogwa mpaka wakaacha ndoa zao wakawa wanalala maporini. Wakati wa korosho mwaka jana, wakulima walizikimbia korosho, watu walikimbia mashamba yao, kisa mikwara vitisho vya JW wa Tz.
Nikajiuliza ivi sisi ni watu au wanyama? Kama ni watu mbona utashi wetu ni kama wanyama?
KUNA SIKU VIONGIZI WETU NA MAJESHI YETU YATASTAABIKA KWELI
JW wa Marekani wangekuwa wataka sifa wangejipendekeza kwa Trump,l akini hawajafanya hivyo, hata yule polisi aliyemsukuma raia, polisi wenzie walimtia nguvuni palepale.
AMA KWELI TANZANIA MMH!!!
Tutayaona mwaka huu kwenye uchaguzi.
Karibuni, povu ruksa!