Nianze kwa kukiri kwamba huu ni udhalilishaji uliopitiliza. Ni kinyume cha maadili. Hata hivyo anapolaumiwa huyo mama, je, huyo mama anaweza kuwapolisi wafuasi wake wote ili wasikose adabu hivi?
Na je, kwani huyo mama aliwahimiza wafanye hivyo? Yumkini majibu ya maswali haya ni hapana.
Niseme tu kuwa ni tofauti na Trump ambaye alikuwa anahimiza vurugu huku akitamba kwamba atawalipia faini watakazotozwa.
Katika hao wawili, bado naona Trump ndiyo mwenye kasoro kubwa. Na hii ni karma. Yeye amekuwa akiporomosha matusi ya nguoni mfululizo. Sasa yanamrudia.