comrade igwe
JF-Expert Member
- Jan 12, 2015
- 7,295
- 3,939
Rais wa Marekani Bw Donald Trump ameiasa nchi ya Korea Kaskazini kufanya mazungumzo kuhusu mpango wake wa silaha za kinyuklia, Rais Trump ameongea hayo leo tarehe 7.11.2017 wakati anaongea na waandishi wa habari pamoja na Rais wa Korea Kusini Moon jae jijini Seoul akiwa katika ziara ya nchi tano za Asia, Trump alisema " Korea Kaskazini njoo kwenye meza ya mazungumzo kuhusu silaha za kinyuklia ninashukuru mungu sitaweza kutumia nguvu ya kijeshi Pyongyang",aidha, ziara ya Bwana Trump katika bara la Asia ina agenda ya mazungumzo ya nyuklia kuhusu Korea Kaskazini, wakati huo huo Wizara ya Ulinzi ya Korea kaskazini imesema itafanya jaribio la saba la kinyuklia mwishoni mwa wiki hii.