True story- yalitokea udsm mwaka 1996

nginda

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
744
82
Jamaa alivuta ngororo yake "wengine mnaita boom" na sijui vijana wa siku hizi mnaitaje?

Baada ya kukamata mshiko akazama baa moja huko mwenge "Ingongwe" na "migombani". Akapiga ulabu wa kutosha. Baadae akavuta KCC (Nikumbusheni mliopo kwa sasa mnaitaje?). Akarudi na kcc yake na kushuka kituo cha kafeteria ya chini (manzese). Si unajua tene mbwembwe za wanaume, akaelekea hall 2 huku akimwonesha KCC awake kuwa lile ghorofa ni lake. Kcc (Jamani kumbe wewe ni tajiri hivyo ), Jamaa (ndiyo, hawa wote unaowaona ni wapangaji wangu), KCC (Kweli kaka nimekuogopa, na hawa waliokaa hapa ni nani), Jamaa (wapangaji wango). Basi wakapanda ngazi hadi ghrofa ya tao huko wakafanya walichotaka KCC kapewa elfu tatu akalala mbele.

Baada ya siku tatu jamaa mchezo ukamnogea akarudi tena Igongwe. Kurudi akampata tena yuleyule KCC wa juzi. Wakaenda vizuri ghorofa ya tano na kufanya mambo. sasa wakati wa kushuka, KCC akamwomba jamaa (naomba unisaidie elfu hamsini dia nifungue bishara. Jamaa (kwa sasa sina hela), KCC (jamani huna hela ghorofa lote hili na wapangaji wengi hivi), Jamaa (hawajanilipa kodi, na ninawadai karibu miezi sita kila mmoja). KCC akafura.(Kumbe washenzi ee. Basi walipofika chini kumbe kuna washikaji wamekaa kwenye kiti cha concrete wana cheza daraft baada ya vipindi virefu vya kuboreka na ma-lecture ya hapa na pale. basi KCC kawaangalia majamaa kwa hasira, huku ameshilia kiuno. (Eti nyie wakaka), wakashtuka na kugeukia (Huu ni karibu mwezi wa sita hamtaki kulipa kodi zetu mnafikiri sisi tutaishije?) JAMAA KUONA HIVYO AKALALA MITINI. Kati ya wacheza draft akapandwa na mdadi anampandishia na hata kupiga vibao. bahati nzuri baadhi wakajua kapigwa changa la macho.

Kugeuka nyuma hamuoni jamaa, na nauli hajapewa. Bonge la kilio. Kurudi chumbani walikotoka hafahamu chumba namba ngapi wala ghorofa ya ngapi.

basi KCC akaamua kutangulia kwa miguu.

(It's true story)

Wa UDSM Tupeni yanayojiri kwa sasa.

 
duh..mambo wanayofanyaga wasomi saa nyingine unakubali kuwa'you can take me outta ghetto but you cant take the ghetto outta me'
 
Inanikumbusha mambo ya Asajile Mwaijumba ( Msajili wa Majumba) hadithi za mwanafyare.
 
KCC wapo. Nenda hall 4 utasikia machungwa machungwa. Ukisika leta, akiingia chumbani ni dakika 45 ndo tena utasikia machungwa machungwa.
 
Dah..umenikumbusha "migombani".....walikuwa wanatengeza kitimoto safi sana! Ile hiyo igongwe na nduguye silent inn imetuulia walimu wengi sana hapo mlimani!

KCC, Bovu, etc....wanawake tunawapa majina mengi mno!
 
jamaa alivuta ngororo yake "wengine mnaita boom" na sijui vijana wa siku hizi mnaitaje?

Baada ya kukamata mshiko akazama baa moja huko mwenge "ingongwe" na "migombani". Akapiga ulabu wa kutosha. Baadae akavuta kcc (nikumbusheni mliopo kwa sasa mnaitaje?). Akarudi na kcc yake na kushuka kituo cha kafeteria ya chini (manzese). Si unajua tene mbwembwe za wanaume, akaelekea hall 2 huku akimwonesha kcc awake kuwa lile ghorofa ni lake. Kcc (jamani kumbe wewe ni tajiri hivyo ), jamaa (ndiyo, hawa wote unaowaona ni wapangaji wangu), kcc (kweli kaka nimekuogopa, na hawa waliokaa hapa ni nani), jamaa (wapangaji wango). Basi wakapanda ngazi hadi ghrofa ya tao huko wakafanya walichotaka kcc kapewa elfu tatu akalala mbele.

Baada ya siku tatu jamaa mchezo ukamnogea akarudi tena igongwe. Kurudi akampata tena yuleyule kcc wa juzi. Wakaenda vizuri ghorofa ya tano na kufanya mambo. Sasa wakati wa kushuka, kcc akamwomba jamaa (naomba unisaidie elfu hamsini dia nifungue bishara. Jamaa (kwa sasa sina hela), kcc (jamani huna hela ghorofa lote hili na wapangaji wengi hivi), jamaa (hawajanilipa kodi, na ninawadai karibu miezi sita kila mmoja). Kcc akafura.(kumbe washenzi ee. Basi walipofika chini kumbe kuna washikaji wamekaa kwenye kiti cha concrete wana cheza daraft baada ya vipindi virefu vya kuboreka na ma-lecture ya hapa na pale. Basi kcc kawaangalia majamaa kwa hasira, huku ameshilia kiuno. (eti nyie wakaka), wakashtuka na kugeukia (huu ni karibu mwezi wa sita hamtaki kulipa kodi zetu mnafikiri sisi tutaishije?) jamaa kuona hivyo akalala mitini. Kati ya wacheza draft akapandwa na mdadi anampandishia na hata kupiga vibao. Bahati nzuri baadhi wakajua kapigwa changa la macho.

Kugeuka nyuma hamuoni jamaa, na nauli hajapewa. Bonge la kilio. Kurudi chumbani walikotoka hafahamu chumba namba ngapi wala ghorofa ya ngapi.

Basi kcc akaamua kutangulia kwa miguu.

(it's true story)

wa udsm tupeni yanayojiri kwa sasa.



sisi siku hizi hatuna muda na mambo hayo tunakesha na kitabu ikilazimu hata kwa mishumaa; tunauchungu na hapa tulipofikishwa na vizazi vilivyotutangulia
 
sisi siku hizi hatuna muda na mambo hayo tunakesha na kitabu ikilazimu hata kwa mishumaa; tunauchungu na hapa tulipofikishwa na vizazi vilivyotutangulia
siku iz mnajua kugoma nakushinda mlimani city (samak samak).
na ngoja mtabaki mia mwaka huu mh.
 
Back
Top Bottom