True story: Ushuhuda wa ndoa yangu

ni jambo ambalo limetokea kwenye maisha yangu, ni hakika na kweli. Mungu ndiye shahidi wa kwanza katika hili. nitamshukuru Mungu maisha yangu yote, kwasababu alinikumbuka kipindi cha dhidi yangu. Mungu nakupa utukufu wote, Utukufu wako hatochukua mwanadmau yeyote.

nimewashauri watu wachague makanisa ya kwenda, mimi nilipitia makanis amengi, nilitangatanga sana kutafuta msaada, ajabu yake mambo yalipobadilika, wachungaji kadhaa hasa wa makanisa ambayo niliyastukia nikayakimbia, wakaanza kujitangaza kuwa wao ndio wameniombea mimi na mke wangu hadi tukafunguliwa....wengine wakawa wanataka nikatoe sadaka....sasa wachungaji zaidi ya watatu wote kila mtu anavutia kwake kwamba yeye ndiye aliomba nami...ajabu yake wote hao niliwastukia nikawakimbia. kuna imani nyingi sana siku hizi, wengine wamejificha kwenye makanisa ya kilokole kumbe watafuta pesa tu na wanaiba utukufu wa Mungu. nilienda kuwaambia mimi sitoi sadaka kwasababu wao wamesema, nikakata na mawasiliano yao, niliwaambia siwezi kumpa utukufu mwanadamu wakati Mungu amefanya. kamwe sitaiba utukufu wa Mungu kumpa mwanadamu. ndio maana nawaambia chunguzeni pa kwenda, hasa kwa nyakati hizi.

however, ukweli upo palepale, imani yenye wokovu ni imani ya Kilokole tu, na huko ndiko nilitafuta Mungu nikampata. nilitangatanga mwanzoni, lakini nilipopata kanisa halisi, ndipo hapo nilipata nguvu za Roho Mtakatifu mimi na mke wangu na maisha yakabadilika.
uliponea kanisa gani mkuu
 
uliponea kanisa gani mkuu
Niwe mkweli dadangu, kiujumla niseme makanisa ya walokole. Ninasali kanisa la TAG kwasasa niko mkoani, lakini wakati wa dhiki yangu nimezunguka makanisa mengi sana ya kilokole. nimesali sana kwa mwingira pale mwenge, nimesali sana kwa gwajima, nimesali sana kwa katunzi, nimesali sana kwa makanisa mengi tu, ila sijawahi kwenda kwa lusekelo. hapo dsm makanisa karibia yote hayo makubwa nimesali. semina nyingi zikitangazwa nilikuwa nahudhuria, wakati mwingine sina nauli natembea kwa mguu. kuzunguka sana kulinisaidia kujua kanisa halisi ni lipi na la uongo ni lipi. huku kote nilikozungua i recomend uende ukitaka. watasema mengiii lakini mimi ninachojua ni kwamba nilipona....wanadamu ni wanadamu wana mapungufu yao lakini mponyaji ni Mungu. uwezo wa kutembea kwa mguu toka ubungo hadi mwenge, toka ubungo hadi posta, toka ubungo hadi kimara, ubungo hadi tabata vilikuwa vitu vya kawaida na joto lote la dar hilo. kwasasa siko dsm. sio kwamba nilikuwa napenda kutembea, sikuwa na nauli ya kulipa route moja ya daladala and yet moto wa kumtafuta Mungu unawaka ndani yangu.
 
Niwe mkweli dadangu, kiujumla niseme makanisa ya walokole. Ninasali kanisa la TAG kwasasa, lakini wakati wa dhiki yangu nimezunguka makanisa mengi sana ya kilokole. hapo dsm makanisa karibia yote hayo makubwa nimesali. semina nyingi zikitangazwa nilikuwa nahudhuria, wakati mwingine sina nauli natembea kwa mguu. uwezo wa kutembea kwa mguu toka ubungo hadi mwenge, toka ubungo hadi posta, toka ubungo hadi kimara, ubungo hadi tabata vilikuwa vitu vya kawaida na joto lote la dar hilo. kwasasa siko dsm. sio kwamba nilikuwa napenda kutembea, sikuwa na nauli ya kulipa route moja ya daladala and yet moto wa kumtafuta Mungu unawaka ndani yangu.
sifa na utukufu ni kwa mwenyenzi Mungu pekee barikiwa
 
ni jambo ambalo limetokea kwenye maisha yangu, ni hakika na kweli. Mungu ndiye shahidi wa kwanza katika hili. nitamshukuru Mungu maisha yangu yote, kwasababu alinikumbuka kipindi cha dhidi yangu. Mungu nakupa utukufu wote, Utukufu wako hatochukua mwanadmau yeyote.

nimewashauri watu wachague makanisa ya kwenda, mimi nilipitia makanis amengi, nilitangatanga sana kutafuta msaada, ajabu yake mambo yalipobadilika, wachungaji kadhaa hasa wa makanisa ambayo niliyastukia nikayakimbia, wakaanza kujitangaza kuwa wao ndio wameniombea mimi na mke wangu hadi tukafunguliwa....wengine wakawa wanataka nikatoe sadaka....sasa wachungaji zaidi ya watatu wote kila mtu anavutia kwake kwamba yeye ndiye aliomba nami...ajabu yake wote hao niliwastukia nikawakimbia. kuna imani nyingi sana siku hizi, wengine wamejificha kwenye makanisa ya kilokole kumbe watafuta pesa tu na wanaiba utukufu wa Mungu. nilienda kuwaambia mimi sitoi sadaka kwasababu wao wamesema, nikakata na mawasiliano yao, niliwaambia siwezi kumpa utukufu mwanadamu wakati Mungu amefanya. kamwe sitaiba utukufu wa Mungu kumpa mwanadamu. ndio maana nawaambia chunguzeni pa kwenda, hasa kwa nyakati hizi.

however, ukweli upo palepale, imani yenye wokovu ni imani ya Kilokole tu, na huko ndiko nilitafuta Mungu nikampata. nilitangatanga mwanzoni, lakini nilipopata kanisa halisi, ndipo hapo nilipata nguvu za Roho Mtakatifu mimi na mke wangu na maisha yakabadilika.
Hongera sana mkuu ubarikiwe sana!
 
Hongera sana mkuu ubarikiwe sana!
kwakweli naomba mnisaidie kumshukuru Mungu. na ukikutana na mtu mwenye shida kama hizo, mwambieni kila jambo lina wakati wake na mwisho wake. amwamini tu Mungu. historia kama hiyo kama nilivyoiandika imetokea kwenye maisha yangu na kamwe sitasahau.siwezi kusema mimi ni malaika kabisa sijatenda dhambi, lakini ukweli uko palepale nitaendelea kumtukuza Mungu na kusimulia ukuu wake kwani alinihurumia nisiyestahili wakati wa dhiki yangu, akanifunika aibu yangu na kunijaza utajiri nilioutafuta kwa miaka 5...utajiri wa watoto ambao haununuliwi kwa pesa..ni kwa neema yake.
 
mkuu pesa zipo saidie unifadhili masomo yangu plz ni pm nikupe a\c number yesu atakulipa mkuu
 
Asiye na wake ana MUNGU
hakika, wengine wametaja magari, wengine wametaja farasi, lakini sisi tutalitaja Jina la Mungu wa Ibrahim Isaka na Yakobo, amesema tuombe lolote kwa Jina la Yesu tutapokea. Hapana jina lingine chini ya Mbingu tulilipewa sisi wanadamu litupasalo kuokolewa kwalo ila Jina la Yesu Kristo. Naye ameliinua sana jina hili kwani kwa Jina la Yesu kila goti litapigwa la vitu vilivyoko juu mbinguni, vilivyoko duniani na vilivyoko chini ya nchi. na kila atakayeliitia Jina la Bwana ataokoka. Liitie Jina lake tu nawe utamwona Mungu Haleliyah.
 
Dah historia yako imenisisimua sana,kwa mtu ambaye hajayapiyia haya hawezi kuamini ila mitihani IPO,Mimi na mkewangu tulipitia haya tena kwa ujauzito kutoka namshukuru mungu sasa tuna mtoto wakike na maisha yanaendelea ,mungu yupo na unaweza jamani tusiache kumuomba iwe kwa shida au raha
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom