Mimi naamini hawa jamaa wana fitna sana , lakini ni pale wenyeji wanapokuwa hawana msimamo, kwani inajulikana kuwa wameshafanya mengi ikiwamo kuisambaratisha urusi iliyokuwepo, ila naamini wanapata nafasi baada ya kuona kuna mwanya kati ya wananchi wenyewe, kwani hata huko uarabuni kuna nchi zinafanya unyama kwa wananchi wao lakini bado hawajafanyiwa alivyofanyiwa Gadaffi, lakini mfano wa nchi kama India au China , Malaysia kwa uchache mbona zinaonekana zimeweza kuendelea, je kunani hapo??, lakini kama hao jamaa shida yao kubwa ni mafuta basi na sisi watanzania tunaosema tuna mafuta tusubiri fitna itupige chini manake siamini kama viongozi wetu wanao msimamo wa kuwatunishia misuli hao wa magharibi, kwani madini yanavyochukuliwa kimya kimya kwa mikataba ambayo hata chizi hawezi kuingia, labda ndiyo maana ya kusema bado nchi yetu ni salama. Au ndiyo motomoto ya Zanzibar kutoka povu kuhusu mafuta inaweza kuwa fitna imeshaanza ya kutusambaratisha. Mungu tusaidie.