TRL Worker - Uzalendo Kwanza Kutetea Taifa Letu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TRL Worker - Uzalendo Kwanza Kutetea Taifa Letu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Zakumi, Sep 23, 2009.

 1. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #1
  Sep 23, 2009
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,813
  Likes Received: 321
  Trophy Points: 180
  [​IMG]

  Tanzania Railways Limited (TRL) technicians yesterday asked an investor in the company, Rites Consortium of India, to support maintenance of locomotives and engines rather than sabotaging the firm’s rolling stock.
  Speaking in Dar es Salaam soon after launching two rehabilitated locomotives, the local technicians called on the investor and other stakeholders to support their motives to revive the remaining eight engines which were left as scrap by the Rites management.
  The call came barely four days after local engineers managed to rehabilitate two engines, which currently are operating smoothly.
  TRL mechanical technician Hendry Luganga said the locally rehabilitated engines could manage to pull a minimum of 22 wagons.
  He said there was no need for the government to import foreign engineers from India to revive the dilapidated engines.
  Electrical technician Aulelius Mville said by the end of this week they were planning to release another three engines which were in the final stages of rehabilitation.
  He said their aim was to show the investor that once enabled local engineers could perform better.
  According to him, the rehabilitated engines travelled yesterday to Morogoro with 710 tonnes of luggage
   
  Last edited: Sep 23, 2009
 2. mnyikungu

  mnyikungu JF-Expert Member

  #2
  Sep 23, 2009
  Joined: Jul 26, 2009
  Messages: 1,441
  Likes Received: 581
  Trophy Points: 280
  i like it,huu ni mfano wa kuigwa yaa uzalendo kwanza kutetea taifa letu
   
 3. J

  JokaKuu Platinum Member

  #3
  Sep 23, 2009
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,730
  Likes Received: 4,949
  Trophy Points: 280
  ..hawa wanakumbuka shuka wakati majogoo yanawika.

  ..kwanini hawakukarabati hizo engines kabla ya Wahindi kuamua kukodisha toka India?
   
 4. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #4
  Sep 23, 2009
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,813
  Likes Received: 321
  Trophy Points: 180
  Jokakuu:

  Hata mimi najiuliza. Hivi hii imefanyika kama public stunt au moyo wa kizalendo.

  Na kama ni moyo wa kizalendo basi ulitakiwa kuwepo kabla.
   
 5. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #5
  Sep 23, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Mimi nadhani hawakupewa nafasi. Lawana zisukumizwe si kwao bali mamlaka makuu aka serikali. Tumeleweshwa mvinyo wa uwekezaji kiasi kwamba tunasahau kuwa hata sisi tunaweza.
   
 6. mnyikungu

  mnyikungu JF-Expert Member

  #6
  Sep 23, 2009
  Joined: Jul 26, 2009
  Messages: 1,441
  Likes Received: 581
  Trophy Points: 280
  mbona hatuna utamaduni wa kuwapa nafasi wataalamu wetu ndo maana hata hao wametuonyesha kama wanaweza,suala la kusema walikuwa wapi sio sahihi labda saa hizi ndo wamepewa nafasi tutajuae? Nawapa hongera na waendelee na moyo huohuo
   
 7. Companero

  Companero Platinum Member

  #7
  Sep 23, 2009
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,474
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Ulikuwepo kabla. Ila wakuu mliamua kufa na wawekezaji. Hebu cheki tarehe ya tukio hili:

  Monday, April 7, 2008

  Mwekezaji Anapowezeshwa!


  Kwa mujibuwa Vyombo vya Habari Mheshimiwa Waziri Mkuu, ametatua mgogoro uliopelekea wafanyakazi wa Shirika la Reli lililobinafsishwa kwa kampuni kutoka India kugoma. Sio siri ni jambo la kufurahisha kuona kuwa wafanyakazi hao watalipwa mishahara yao. Ila swali la kujiuliza ni iweje mwekezaji ashindwe kuhudumia wafanyakazi wake mpaka Serikali imkope shilingi bilioni 3.6? Yaani ule uwezeshaji wote wa vivutio wanavyopewa na TIC havitoshi?

  Na hizo dalili za wingu la ufisadi ambazo zinajidhihirisha zitachunguzwa au yaliyopita si ndwele tugange yajayo? Naam yajayo yatatokea baada ya hiyo miezi 5 ambapo hizo bilioni 3.6 zitakuwa zimekwisha. Je, mwekezaji atakuwa amejizatiti au atataka kuwezeshwa tena na Serikali yetu iliyoelemewa na mizigo mingi ya madeni ya uwekezaji mbovu na inayowezeshwa na wafadhili?

  Hakika ndio maana Mwalimu Nyerere alilalamika kuwa mbona wanatuambia tubinafsishe vya kwetu wakati vyao hawabinafsishi. Ndio maana alisisitiza kuwa 'you cannot nationalize nothing' yaani huwezi kubinafsisha kisichopo. Kumbe tulikuwa navyo na fedha tunazo. Kuifadhili TRL kunadhihirisha kuwa bongo tambarare kama anavyouliza kwa bezo mtoa maoni wa blogu ya Michuzi?

  Source: http://udadisi.blogspot.com/2008/04/mwekezaji-anapowezeshwa.html
   
 8. M

  Magezi JF-Expert Member

  #8
  Sep 24, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Ukweli ni kwamba kwa utawala wa CCM, wataalamu huwa hawasikilizwi. Tuna viongozi wasiojua lolote jinsi ya kuendeleza nchi, wanawaza kuuza kila kitu na hii inasababishwa na mawazo ya kimaskini ya kutaka kula leo na ya kesho yatajujua bila kupanga mikakati ya muda mrefu na mfupi.

  Tanzania tunao wataalamu wa kutosha kuendeleza mashirika mbali mbali tatizo ni pesa zinaishia kwenye mikutano, semina , warsha, usafiri wa vigogo n.k. Nawapongeza mafundi wa TRL na nawaomba waendelee na moyo huo.
   
 9. omarilyas

  omarilyas JF-Expert Member

  #9
  Sep 24, 2009
  Joined: Jan 24, 2007
  Messages: 2,127
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Mwenzenu natatizwa sana na hii dhana ya Uzalendo wa hawa ndugu ambao miaka yote ndio waliokuwa wakisabotage shirika lao. Wao ndio waliokuwa wamegeuza karakana za TRC kuwa karakana za shughuli zao binafsi, ni hawahawa ndio waliokuwa wakiharibu hizo engine za treni ili wapate tenda za kufanyia matengenezo na overtimes, ni hawahawa ndio waliokuwa wakiliibia TRC katika mauzo ya ticket, ni hawahawa walikuwa wakithubutu kuangusha treni ili kushinikiza madai yao ambayo mengi yalikuwa ni ya kidanganyifu, ni hawahawa ndio walikuwa wakiwanyanyasa wasafiri wa treni haswa mabinti wa shule, ni hawahawa waliokuwa mabingwa wa kibia treni zao dizeli na mengine hovyohovyo mengi....

  Sasa wanapokuja na huu uzalendo wa kina ALOYCE KIMARO inakuwa ngumu kuwaamini.....

  Kwa kweli nashindwa kuelewa uzalendo wa enzi hizi......nashindwa kabisa

  omarilyas
   
  Last edited: Sep 24, 2009
 10. J

  JokaKuu Platinum Member

  #10
  Sep 24, 2009
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,730
  Likes Received: 4,949
  Trophy Points: 280
  ..nakubaliana na hoja zako 100%.
   
 11. K

  Koba JF-Expert Member

  #11
  Sep 24, 2009
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 6,144
  Likes Received: 494
  Trophy Points: 180
  Uzalendo my a$$$,hawa wamekuwa na shirika likawafia mikononi mwao,na sio siri these as$$es kwa uzembe,rushwa na kutowajibika ndio maana shirika limekufa,anyway sasa wanapoteza kazi zao na hawana pa kula ndio wanakuja na stunt zao za danganya toto...hili shirika lingeuzwa lote 100% kwa mtu competent na serikali isingejiingiza na kutoa pesa ya aina yeyote,hawa wapuuzi acha warudi barabarani wawe ombaomba tuu na hao matapeli wa RITES wachukue hiyo 50% watimue zao shirika lianze upya kabisa!
   
 12. King Zenji

  King Zenji Senior Member

  #12
  Sep 25, 2009
  Joined: Feb 18, 2008
  Messages: 178
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33

  ,,,Wamegundua kwamba muda si muda watarudi VIJIJINI kuchoma MAHINDI kiukwelikweli,mijamaa ilikua MINYANG'AU,inakwiba kila kitu cha shirika,yaani walikua wanafanya shirika ka la kwao,mnakumbuka enzi zile gogo likifunga behewa 25,ni shs ngapi per trip??,lakini asikuambie mtu,wafanyakazi wa reli wote walikua NJEMA ile mbaya,kuanzia VITUMBO mpaka VIJUMBA vyao,tena kwa mshahara wa 84,000 tu,ni wizi MTUPUUUU ndo umelifikisha hilo shirika hapo lilipo.
   
Loading...