TRL / RAU kuna nini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TRL / RAU kuna nini?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by nkawa, Jul 28, 2009.

 1. nkawa

  nkawa Senior Member

  #1
  Jul 28, 2009
  Joined: May 11, 2009
  Messages: 181
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wanajamii,
  Nina kaka yangu aliajiriwa na TRC tangu amalize chuo cha Reli miaka ya 1990 upande wa karakana kama fundi wa Engine za Treni. Sasa mwaka 2007 akiwa kitengo hicho hicho cha ufundi wizi wa mafuta ulitokea na yeye kuhusishwa na wizi huo kwasababu alikuwa pia ni msimamizi wa store ya vifaa na mafuta. Kesi ikaendeshwa ndani ya TRC yenyewe akakutwa na kosa hivyo afukuzwe kazi. Kwahiyo akawa anaripoti tu kazini akisubiri barua ya kufukuzwa kazi.
  Tatizo lililopo sasa hadi leo hii hiyo barua hajapewa kila akifuatiliwa anapigwa tarehe. TRC ilipobinafsishwa kwa hawa wahindi na kuwa TRL mwajiri huyu mpya alimwiita arudi kazini na kumwambia barua ya kurudi kazini iko kwa mkuu wa idara yake ya ufundi (RAU). Alipoenda kule anaambia kwanza faili lako halionekani na hiyo barua sijaipata. Akahangaika huku na huko na wenzie kumsaidia faili likaonekana lakini baadhi ya barua zake za kazi hazipo. Akarudi kwa mwajiri mpya na kumwelezea. Huyu mwajiri mpya akamwambia nilishaandika barua ya wewe kurudishwa kazini tangu 2007 na malipo yako yote upewe, sasa namwandikia mkuu wako (RAU) barua nyingine kumkumbushia ile barua ya mwanzo ya wewe kurudishwa kazini na kulipwa.
  Kaka yangu akamwambia huyu mwajiri mpya TRL naomba tu unisaidie nipate barua yangu ya kufukuzwa kazi naona kurudishwa kazini inakuwa ngumu, ili nifuatilie pesa yangu ya PPF angalau nihangaike na maisha mengine.

  Hadi sasa ninavyoandika hii hakuna hata moja lililofanikiwa.

  Yaani hata sijui nimsaidiaje, ni baba wa mke na familia ya watoto 3, maisha yenyewe ya Dar, kila anapojaribu kazi hazipatikani, ameuuza chips lakini hali bado ni ngumu.

  Naomba ushauri wenu.

  Tuanzia wapi angalau apate mwanga wa jinsi ya kupata haki yake? kama ni ajira basi arudishwe, kama kufukuzwa basi apewe barua yake!!!!
   
Loading...