Tribute to David Wakati: His Legacy Will Live On!. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tribute to David Wakati: His Legacy Will Live On!.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pascal Mayalla, Dec 4, 2011.

 1. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #1
  Dec 4, 2011
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,566
  Likes Received: 18,529
  Trophy Points: 280
  Wanabodi

  Mzee David Wakati, amezikwa leo jioni katika makaburi ya Kinondoni.

  Mazishi hayo yamehudhuriwa na umati wa watu, wakiwemo mawaziri, wanasiasa, viongozi wakuu wa dini, waandishi wa habari, na umati mkubwa wa ndugu jamaa na marafiki.

  Ingawa Mzee David Wakati ametutoka, ametuachia legacy ambayo itaishi na sisi milele.

  Nikianzia na kwangu mimi mwenyewe, enzi za primary, nilitokea kusoma darasa moja na mtoto wa David Wakati, Mandela hivyo kumfahamu Mzee David Wakati kupitia kwake.

  Nilipomaliza shule nilijiunga na Chuo cha Uandishi wa Habari (TSJ) na kuajiriwa RTD Mzee David Wakati akiwa ni Mkurugenzi, hivyo Mzee Wakati ndie alinifungulia milango ya fani ya utangazaji ambayo niko nayo mpaka sasa.

  Baada ya kuajiriwa, batch yetu ikiwa na vijana 12. Mimi Pascal Mayalla, Aboubakar Liongo, Swedy Mwinyi, Kassim Mikongolo, Bakari Msulwa, Abdalah Majula, Nswima Ernest, Rukia Machumu, Shida Waziri (Masamba), Rose Japhet, Nyambona Masamba na Jane Lutaserwa.

  Wote tulipigwa kozi ya miezi mitatu ya Radio Induction Course, Mzee Wakati alikuwa ni mmoja wa walimu wetu. Alikuwa ni mwalimu wa somo la Habari na OB. Wakati huo mimi nikiwa nimepania kuwa msomaji wa habari na mtangazaji wa mpira.

  Wakati wa somo la habari, Mzee Wakati alikuja na scrpts za habari na kumpa kila mmoja wetu kusoma. Wakati unasoma yeye amekaa kwenye kiti anakusikiliza huku amefunga macho na kuinua sikio moja juu.

  Baada ya kutusikia sisi wote 12, alitoa majibu kuwa kati yetu wote wasoma habari ni wawili tuu, Swedy Mwinyi na Aboubakar Liongo!. Sio siri nilikata tamaa kutimiza ndoto yangu ya kuwa mtangazaji.

  Mzee Wakati alitutia moyo kuwa kushindwa kusoma habari sio mwisho wa utangazaji, sio kila mtangazaji lazima asome habari, kuna vipindi vingi tuu. Kila mwanafunzi alijaribiwa kila idara, hatimaye mimi nikapangwa External Service, idhaa ya Kiingereza, hivyo huo ndio ukawa mwanzo wangu wa utangazaji. Thanks to David Wakati!.

  Tulio fanya nae kazi, japo alikuwa bosi lakini alikuwa humble na down to earth!. Mzee David Wakati alikuwa ni bosi easy to talk too, yaani unajisikia huru kuingia ofisini kwake kumweleza shida yoyote, alikuwa very reachable.

  Mzee huyu aliipenda radio kwa moyo wake wote!. Alikuwa na anatembea na kijiredio chake kidogo, portable cha Sony akisikiliza redio 24/7 hivyo mtangazaji ukiboronga hewani, kesho yake unapata habari yako!. Kitendo tuu cha kutangaza huku ukijua Mkurugenzi anasikiliza kuliwafanya watangazaji waliopitia RTD kuwa very resiponsible kwa wasikilizaji wao, kulikuwa hakuna upuuzi upuuzi mnaousikia kwa hawa watangazaji wa siku hizi kuna wengine utadhani wako sokoni, na wengine wanazungumza mambo ya vyumbani mchana kweupe!.
  Thanks David Wakati kwa kulea kizazi cha watangazaji wenye nidhamu wa enzi zile, Thanks!.

  Japo baadae nililazimika kuacha kazi ya utangazaji due to family pressure ya kutafuta maisha bora, nikajaribu maisha ya ughaibuni nchini Uingereza, Marekani, Uswisi, Italia na Sweden, kote nilishindwa nikarejea Tanzania, nikaenda Mlimani kusoma sheria na kuhitimu ili niwe wakili.

  Wakati wote nikisoma nilikuwa nikifanya part time za utangazaji, baada ya kumaliza sheria, nimejikuta napenda zaidi utangazaji kuliko kusimama mahakamani. Hivyo ni ushahidi tosha kazi ya utangazaji ni kazi ya wito bila kujali ina maslahi gani, you just do what you love no matter what you get!. Thanks Mzee DavidvWakati!.

  Ile batch yake ya mwisho ya watangazaji 12 aliyewaajiri wote 12 bado ni Watangazaji mpaka leo na 9 kati ya hao 12 bado TBC. Watatu tulioandoka ni mimi Pascal Mayalla, Aboubar Liongo aliyeenda Ujerumani na Abdalah Majura aliyejoin BBC. Msishangae mkisikia ninerudi TBC!. Aboubakar Liongo amerejea nchini na kwenye mazishi alikuwepo hivyo msishangae kama ataibukia TBC!. Majula nae alimaliza mkataba wake BBC na sasa anamiliki Redio yake mwenyewe ila pia msishangae kama mtamsikia nae amerejea TBC!, ili litimie lile neno, " Sikumpoteza hata mmoja kati ya wake thenashara David Wakati, aliyowachagua kabla ya kustaafu rasmi!".

  Leo kwenye mazishi, nimemfanyia kipindi chake cha mwisho kwa kuzungumza na baadhi ya watu wakinipa kumbukumbu zao Mzee David Wakati amewaachia nini.

  Posts zitakazofuatia nitaweka tribute hizo,
  Wengine ambao unazo baadhi ya kumbukumbu za Mzee David Wakati, unaweza ukazitaja humu ili na wengine tuweze kufaidika na alichotuachia Mzee wetu, Baba yetu, Mwalimu wetu, Boss wetu, Mtangazaji wetu, Shujaa wetu, Mshauri wetu, Rafiki yetu, Mtanzania mwenzetu David Wakati,

  Thank You for All This!.

  Pascal Mayalla
  +255 784 270403
  pascomayalla@yahoo.co.uk
  Update 1.

  Kipindi maalum cha David Wakati Legacy kitarushwa hewani na TBC-1 Saa 5:00 usiku huu!.
   
 2. C

  Chupaku JF-Expert Member

  #2
  Dec 4, 2011
  Joined: Oct 15, 2008
  Messages: 1,045
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Pole Paschal. Pole wote mlioguswa na msiba huu. Pamoja na wewe kuweka kumbukumbu hizo,naamini pia ni wakati muafaka kwa TBC kuweka kumbukumbu za waandishi waliotumikia radio km David.
   
 3. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #3
  Dec 4, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,503
  Likes Received: 5,616
  Trophy Points: 280
  Duh! Kumbe umepita kwenye mikono ya huyu Mzee! Kiongozi bora ni yule anayeweza kutengeneza mwenyewe timu bora ya kufanya nayo kazi.kwa hiyo list ya wateule 12 kweli Mzee wakati alikuwa kichwa!
   
 4. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #4
  Dec 5, 2011
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,566
  Likes Received: 18,529
  Trophy Points: 280
  Kipindi Maalum cha David Wakati Legacy kitarushwa hewani na TBC- 1 any moment kuanzia saa 5 kamili usiku wa huu
   
 5. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #5
  Dec 5, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  poleni na hongereni pia kwa kupata nafasi ya kukutana na Dacid Wakati katika maisha yenu na
  kuwaachia kitu 'positive' katika maisha yenu.....

  David Wakati alikuwa zaidi ya mkurugenzi na mwanahabari......
  alikuwa mzalendo alieipenda nchi yake..........

  angeweza kwenda nchi nyiingi sana lakini alijitolea kuitumikia nchi yake

  licha ya malipo duni saana......

  na kitu kizuri kuliko vyote aliwaambukiza uzalendo watu wengi alokutana nao........

  sikuwahi kukutana personal na David Wakati lakini jina lake popote linapotamkwa

  linatamkwa na 'full integrity'.........kitu ambacho siku hizi hata 'viongozi wetu wa kisiasa' hawakipati

  kuna weengi mno ambao David Wakati ameshiriki kwa namna moja au nyingine 'kuwafikisha'
  walipofika na kuna mengi tunaweza zungumza kuhusu Davidi Wakati......lakini

  itoshe kusema 'alitoa mchango wake wote kwa nchi yake katika maisha yake'

  ni vipi taifa litamkumbuka na kumshukuru????
  au je tulimtumia vya kutosha kwa faida ya tasnia ya uandishi wa habari kwa ujumla????

  mungu ailaze roho yake mahali pema peponi .ameen

  THE BOSS
   
 6. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #6
  Dec 6, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  pole kaka pascal kwa kuondokewa na mzee David. kuna wkt nkisika ulipata ajali ya pikipiki hope umepona sasa
  tafadhali utuwekee hiyo clip ya TBC walau tulio mbali tuwezee kuona kilichojiri
   
 7. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #7
  Dec 6, 2011
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,566
  Likes Received: 18,529
  Trophy Points: 280
  Lokissa, asante, ni kweli nilipata ajali mbaya ya bike, Thank God nimepona minus one hand!, but life goes on.

  Nitaiweka hiyo clip humu, baada ya kuipunguza, iko kwenye HD hivyo nitaipunguza mpaka ifit kwenye MP 4
   
 8. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #8
  Dec 6, 2011
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,569
  Likes Received: 1,935
  Trophy Points: 280
  Pole ndugu Pasco kwa ajali, pia poleni kwa msiba.
   
 9. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #9
  Dec 6, 2011
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,566
  Likes Received: 18,529
  Trophy Points: 280
  Jmushi, asante
   
 10. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #10
  Dec 6, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  Mungu ni mwema
  Minus one hand sijaelewa pole sana
  Itakuwa vemaa kama ukarudi TBC walau kutakuwa na mabadiliko walau tunapata redio online ila quality ya vipindi aliondoka nayo Tido kazi kwenu kurejesha hadhi ya TBC
  ntafurahi sana kuiona hiyo clip
   
Loading...