Treni ya Umeme huu wa mgawo?

Kidamva

JF-Expert Member
Dec 3, 2013
2,578
1,984
Pamoja na kuipongeza serikali kwa kuanza ujenzi wa reli ya standard gauge ambayo treni zake zitakuwa za Umeme, najiuliza huo umeme wa uhakika upo?
Wenzetu nchi zilizoendelea wanatumia umeme wa nuclear, sisi bado tunabangaiza na umeme wa maji kidogo na gesi. Bado hatujawa na umeme wa Uhakika. Nchi za Kenya, Nigeria zimeshindwa kutumia treni za umeme, sisi tutaweza kweli? Treni zisije kuzimikia maporini kwa kukatika umeme!
 
Masikio yako yanawaza umeme hakuna mpango huo kwa sasa hapa nchini.

Ni standard gauge (reli ya kisasa yenye viwango vya kimataifa ila itakuwa sio kama hizi reli za mkoloni).

Umeme wa kutembeza Treni kilomita 400 haupo hapa nchini
 
Pamoja na kuipongeza serikali kwa kuanza ujenzi wa reli ya standard gauge ambayo treni zake zitakuwa za Umeme, najiuliza huo umeme wa uhakika upo?
Wenzetu nchi zilizoendelea wanatumia umeme wa nuclear, sisi bado tunabangaiza na umeme wa maji kidogo na gesi. Bado hatujawa na umeme wa Uhakika. Nchi za Kenya, Nigeria zimeshindwa kutumia treni za umeme, sisi tutaweza kweli? Treni zisije kuzimikia maporini kwa kukatika umeme!

Mbona wewe Hospitalini hakuna Dawa lkn Baba na Mama yako walikuleta tu Duniani hivyo hivyo? Mbona hawakusubiri kwanza Hospitali kujengwa ndiyo wakutunge?
 
Kwani hii tren ya umeme itakua inafanya kazi kwa kutumia umeme huhu wa hapa kwetu.
Wa kidumu ukiisha mlimani weka kigogo konda anakwenda kwawakala safari inaendelea.
Au Wanaleta na umeme wao maana umeme wa hapa bongo ni wamagumashi watakuwepo vishoka mpaka kwenye umeme wa kwenye tren: kama hakuna siju hatujakwama darajani ruvu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kinyerezi phase two inakamilika mwaka kesho ndo umeme utakaoendesha hyo train
 
Watch It! !
Yaani Sasa Ni Kero
Naamini Rais Akirudi Akikuta Hii Atawatumbua
 
Mkuu, ingekuwa ni vyema kwanza ukaelewa jinsi treni inavyofanya kazi.
Kichwa cha treni kina mota mbili kama zile za mashine ya kusaga. Zile mota ndio zinafanya kazi ya kuzungusha matairi ya treni pamoja na mabehewa yake.
Ili mota iweze kuzunguka inahitaji umeme. Hizi treni za sasa zina genereta ya diesel inayotumiak kuzalisha umeme na kuupeleka kwenye zile mota ambazo ziko chini ya matairi.
Treni za umeme kama zile za ulaya zinatumia umeme wa gridi kuzungusha zile mota mbili kwa hiyo hazina genereta ya diesel ya kuzalisha umeme. Ila hizi za kwetu japo zitakuwa zinatumia umeme wa gridi, pia bado zitakuwa na zile genereta za diesel kwa ajili ya kuzalisha umeme (wa back up) just in case umeme huu wa gridi utakatika.
So kuhusu hilo usiwe na wasi wasi. Wewe nenda kakate tikiti yako na baada ya muda mchache utakuwa umefika mwisho wa safari yako salama salmini...
 
Pamoja na kuipongeza serikali kwa kuanza ujenzi wa reli ya standard gauge ambayo treni zake zitakuwa za Umeme, najiuliza huo umeme wa uhakika upo?
Wenzetu nchi zilizoendelea wanatumia umeme wa nuclear, sisi bado tunabangaiza na umeme wa maji kidogo na gesi. Bado hatujawa na umeme wa Uhakika. Nchi za Kenya, Nigeria zimeshindwa kutumia treni za umeme, sisi tutaweza kweli? Treni zisije kuzimikia maporini kwa kukatika umeme!
Tatizo unawaza matatizo, shida, tabu, na mahangaiko.
Badili mfumo wako wa kuwaza itskusaidia. Jaribu basi kuwaza kidogo tu Kama mimi,yaani hivi treni itafanya kazi kipindi kisicho na mgao.
Au waza Kama watu wazima, yaani hivi wakati treni ya umeme inaandaliwa, team nyingine inajipanga kuweka miundombinu ya kuhakikisha umemeso shida eneo hilo. Yaani like jua ije mvua mgizo utaenda Mza kwa umeme.

Senksi

Sent from my Nexus 5 using JamiiForums mobile app
 
Pamoja na kuipongeza serikali kwa kuanza ujenzi wa reli ya standard gauge ambayo treni zake zitakuwa za Umeme, najiuliza huo umeme wa uhakika upo?
Wenzetu nchi zilizoendelea wanatumia umeme wa nuclear, sisi bado tunabangaiza na umeme wa maji kidogo na gesi. Bado hatujawa na umeme wa Uhakika. Nchi za Kenya, Nigeria zimeshindwa kutumia treni za umeme, sisi tutaweza kweli? Treni zisije kuzimikia maporini kwa kukatika umeme!
Usiwe negative kiasi hicho ndugu yangu. Katika maisha huwezi kusubiri kila kitu kiwe sawa ndio ufanye unavyotaka hilo halitatokea kamwe hata katika maisha yako wewe binafsi. Mambo mengine yanafanyika simulteneously au linafanyika jambo moja then kama kutakuwa na mpungufu yanarekebishwa. Halafu hii tabia ya kuona kwamba kwa sababu kenya au Nigeria hawajafanya basi na sisi hatutaweza ni ujinga na ulofa. Kila nchi ina mipango na vipaumbele vyake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom