Treni ya Mwakyembe bado sana, SUMATRA waikwamisha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Treni ya Mwakyembe bado sana, SUMATRA waikwamisha

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwana Mpotevu, Oct 2, 2012.

 1. Mwana Mpotevu

  Mwana Mpotevu Platinum Member

  #1
  Oct 2, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 3,294
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  Soma habari hii:

  SUMATRA wakwamisha Treni ya Mwakyembe

  Aidan Mhando na Zaina Malongo

  USAFIRI wa treni ya abiria uliokuwa umepangwa kuanza jijini Dar es Salaam jana umekwama kufuatia Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) kutopewa leseni na kutoidhinishiwa viwango vya nauli na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra).

  Uongozi wa TRL ulisema jana kuwa, inasubiri kauli ya mwisho ya Sumatra kuhusu usafiri huo ili itoe taarifa rasmi kwa umma juu ya treni hiyo kuanza huduma ya usafiri kwa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam.

  Msemaji wa TRL, Midladjy Maez aliliambia gazeti hili jana kuwa usafiri huo unatarajiwa kuanza kazi siku yoyote kuanzia sasa, lakini mpaka Sumatra watakapotoa leseni ya usafirishaji na kuweka viwango vya nauli.

  Alisema tayari wamewasilisha mapendekezo ya viwango hivyo vya nauli na kuomba leseni ya usafirishaji Sumatra, ikiwa ni pamoja na kuitaka mamlaka hiyo ikague treni hiyo kujiridhisha na usalama wake.

  “Hatuwezi kusema usafiri utaanza lini, lakini tayari kila kitu kimekamilika kwa sababu tulishapeleka Sumatra mapendekezo ya nauli na maombi ya leseni ya usafirishaji na sasa tunachosubiri ni majibu...,” alisema Maez na kuongeza;

  “Tunafahamu kuwa, watu wengi wanataka kujua siku ya kuanza usafiri wa treni, ila tunaomba wasubiri maandalizi yakikamilika kila kitu kitawekwa wazi…”

  Maez alifafanua kuwa usafiri huo utajumuisha mabehewa 14 ambayo kwa sasa yote yapo tayari na kwamba kutakuwa na treni mbili zitakazokuwa na mabehewa sita kila moja, mabehewa mawili yatakuwa ya akiba.

  Akizungumzia ratiba ya treni hiyo, Maez alisema kuwa kutakuwa na safari mbili kwa siku.

  “Asubuhi kutakuwa na treni kutoka Ubungo Maziwa hadi mjini, jioni treni hiyo itatoka mjini hadi Ubungo Maziwa. Vituo vya treni vitakuwa vinane na itakuwa ikibeba abiria 950 na kila behewa litapakia abiria 160.” alisema Maiz.

  Alipotakiwa kuzungumzia madai hayo ya TRL, Meneja Uhusiano wa Sumatra, David Mziray alisema taarifa zitawekwa wazi baadaye na kusisitiza kuwa usafiri huo uko chini ya taasisi mbalimbali za Serikali.

  “Taratibu za kuhakikisha treni inaanza kutoa huduma zinaendelea na taarifa rasmi itatolewa.”

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Omari Chambo alisema kuwa, pamoja na kuchelewa, usafiri huo wa treni utaanza ndani ya mwezi huu kama ilivyopangwa.

  “Hatukusema kuwa usafiri utaanza Oktoba Mosi, bali tulisema utaanza mwezi Oktoba na hakuna kilichobadilika mpango huo bado upo palepale,” alifafanua Chambo.

  Hivi karibuni Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dk Charles Tizeba alisema usafiri huo utaanza mwezi Oktoba baada ya kukamilika ukarabati wa reli kutoka Ubungo hadi Stesheni.

  Alisema kufikia mwezi huu, treni hiyo itaanza kubeba abiria ili kupunguza matatizo ya usafiri kwa wakazi waishio maeneo inapopita treni hiyo.

  MY TAKE: Nahisi kama siasa zinatawala zaidi zoezi hili kuliko uhalisia. Walikuwa wapi kufanya taratibu zote hiz tangu mwanyembe atangaze Julai mwaka huu??
   
 2. Mwana Mpotevu

  Mwana Mpotevu Platinum Member

  #2
  Oct 2, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 3,294
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  aliyetuletea post ya kwamba treni imeanza na picha ya kughushi jana asubuhi anastahili kushughulikiwa na mods
   
 3. Khakha

  Khakha JF-Expert Member

  #3
  Oct 2, 2012
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 2,983
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Wakuu heshima mbele,
  Ninasikiliza kipindi cha magazeti RFA nimesikia kuwa sumatra wamezuia usafiri wa treni kuanza sbb uchunguzi wa mambo ya usalama na majadiliano khs viwango vya nauli yalikuwa hayajakamilika.

  nawasilisha.
   
 4. Khakha

  Khakha JF-Expert Member

  #4
  Oct 2, 2012
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 2,983
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  zis kantri bhana!
   
 5. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #5
  Oct 2, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,291
  Likes Received: 19,446
  Trophy Points: 280
  vibosile wa sumatra nao wanamiliki madala dala?
   
 6. saragossa

  saragossa JF-Expert Member

  #6
  Oct 2, 2012
  Joined: Jan 3, 2011
  Messages: 2,141
  Likes Received: 147
  Trophy Points: 160
  I smell a rat somewhere!
   
 7. M

  Mkwe21 JF-Expert Member

  #7
  Oct 2, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 1,836
  Likes Received: 454
  Trophy Points: 180
  Mjue Usalama ni Pamoja na kuweka Barriers Kwenye barabara kuu kama Mabibo, Mandela, Tabata, Mandela, Msimbazi, Na Nyerere ili kuondoa ajali ambazo zitajitokeza Ambazo kwa weledi Wangu sio za lazima!! Sasa Huyu ndugu anaongelea usalama umekamilika ni Usalama Upi Huo? Sijaona Vituo vya kupandia Abiria pamoja na Taa (Usalama wa abiria) Sijaona sign and blocking barriers kwenye High ways (Barabara kuu na sign bosrds kwa barabara ndogo) na Mengiine Mengi!! Ila huu usalama anaousemwa na huyu Mheshimiwa ni Upi?? Kalagabaho bora mkono uende Kinywani
   
 8. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #8
  Oct 2, 2012
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,288
  Likes Received: 22,053
  Trophy Points: 280
  SUMATRA kwa taarabu.... hawajambo
   
 9. andrewk

  andrewk JF-Expert Member

  #9
  Oct 2, 2012
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 3,103
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Acha kukurupuka, ebu tafuta hii taarifa uisome na uelewe.......

   
 10. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #10
  Oct 2, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Mwenye macho haambiwi tazama,akili za kuambiwa changanya na zako!! Mchezo mchafu huo,mwakyembe na sumatra wamekaa mezani na kukubaliana kwamba sumatra waikwamishe ili waendelee kurekebisha miundombinu kwani bado haijatengemaa!! This country bwana usanii mwingiiiiiiiii........
   
 11. 2

  21DEC2012 Senior Member

  #11
  Oct 2, 2012
  Joined: Oct 25, 2011
  Messages: 116
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  collusion between SUMATRA and Government..wanataka kujustify kwa nini usafiri wa treni haujaanza October kama walivyotudanganya.
  uchunguzi wa maambo ya usalama unafanyika baada ya mradi kuisha au wakati unaendelea?
  ukaguzi ungefanyika kabla ya mwezi wa kumi.
   
 12. mujusi

  mujusi JF-Expert Member

  #12
  Oct 2, 2012
  Joined: Jan 22, 2010
  Messages: 237
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Mimi kitu ambacho sijakielewa ni cha kuwa na treni moja tu asubuhi na moja tu jioni. Kutoka Ubungo hadi mjini na Mjini hadi Ubungo. Hii kweli inalipa gharama zote za miundo mbinu na uendeshaji na kuwafanya watu wawahi makazini na kupunguza msongamano? Kwa maoni yangu ningeona afadhali zingekekuwa mbili kwa asubuhi na mbili kwa jioni.

  Hii inaweza sababisha nauli ziwe kubwa ili kugharamia gharama za uendeshaji labda ndio maana SUMATRA wana kigugumizi.
  Tusubiri tuone kwanza tusianze kuvuka daraja kabla hatujafika.
   
 13. Tiba

  Tiba JF-Expert Member

  #13
  Oct 2, 2012
  Joined: Jul 15, 2008
  Messages: 4,511
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Huyo jamaa anastahili kula ban bila huruma hata kidogo. Alileta taarifa ya uongo hapa!!!!

  Tiba
   
 14. Mr Suggestion

  Mr Suggestion JF-Expert Member

  #14
  Oct 2, 2012
  Joined: May 2, 2011
  Messages: 605
  Likes Received: 121
  Trophy Points: 60
  Kuna mtu jana alipendekeza mtu binafsi apewe kazi ya kuendesha train hiyo, sikufanikiwa kumuunga mkono ila leo namuunga mkono, suala hapa ni kupunguza foleni lakini kwa mtazamo wa mbali kama hili litafanikiwa inamaana vijana wengi ajira zao zitakuwa hatarini hapa nawazungumzia makondacta, madereva, mateja, wauza magazeti, wale jamaa wa Azam, wauza Cd, wauza vifaa vya kwenye magari,,,,,,, kimsingi matatizo yetu ndio faida ya mafisadi, siombei mabaya ila kimsingi project hii kufanikiwa inahitaji nguvu kubwa mno kutoka kwa wananchi manake kwa viongozi tulionao na watumishi waliopo pale TRL haitowezekana, itafanya kazi siku mbili kesho yake utaambiwa exhaust pipe imekatika tumeagiza spea india
   
 15. b

  bariadi2015 Member

  #15
  Oct 2, 2012
  Joined: Sep 26, 2012
  Messages: 22
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sumatra wanafikisha ujumbe tu,kuwa mwakyembe hakumanisha alichokiahid.
   
 16. Khakha

  Khakha JF-Expert Member

  #16
  Oct 2, 2012
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 2,983
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  mkuu sikukurupuka. niliandika kile mtangazaji wa rfa alichokuwa anasoma ktk vichwa vya habari vya magazeti ya leo.
   
 17. idawa

  idawa JF-Expert Member

  #17
  Oct 2, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 18,527
  Likes Received: 10,441
  Trophy Points: 280
  ilikua kwenye majaribio.! Hivyo bado kuzinduliwa rasmi.!
   
 18. m

  mamanalia JF-Expert Member

  #18
  Oct 2, 2012
  Joined: Nov 7, 2009
  Messages: 671
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Mwakyembe turudishie TRC yetu, kila nikisoma neno TRL napata hasira mno, inanikumbusha wale wahindi wa kawambwa.
   
 19. M

  Mujwahuzia Senior Member

  #19
  Oct 2, 2012
  Joined: Nov 17, 2011
  Messages: 137
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nawapongeza Vingozi wa SUMATRA kwa kuliona hili wiki mbili zilizopita, naandika juu ya usafiri wa Treni nikimuomba waziri wa Uchukuzi Dr. H.Mwakyembe pamoja na nia yake nzuri kutafuta ufumbuzi wa kupunguza shida ya Usafiri mkoani DSM.

  Lakini jambo hili lifanywe kwa umakini zaidi baada ya kugundua hata marekebisho ya hiyo reli itakapopita treni ilikuwa haijafanyiwa marekebisho ya kutosha kama, Kusawazisha njia ya hiyo reli.

  Baadhi ya Mataluma yamechoka mbaya hayakuondolewa na kuwekwa mapya, kimsingi reli nzima bado haijafanyiwa matengenezo ya kutosha hata kushindilia zile Kokoto na niliwaasa Watanzania wenzangu tunaotarajia kupanda chombo hicho kuwa makini kwani uwezekano wa kuleta maafa ni mkubwa zaidi kuliko mafanikio, na shukuru watu wa Sumatra pengine hilo nalo mmeliona na mmelizingatia
  .
   
 20. KOMBAJR

  KOMBAJR JF-Expert Member

  #20
  Oct 2, 2012
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 5,848
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Nashauri kuwe na umakini tusikimbilie kuanza kitu ambacho bado hakija pita kwenye njia au taratibu stahiki!
   
Loading...