Treni ya abiria yapata ajali Dodoma

Hii ni serikali ya kuhuni sana ,samahani naomba mwongozo hivi mtu akipanga kupinduwa nchi anakuwa na makosa??
 
Hizo ajali mbona zinatokea sana tu ,kule india ,halafu watu wanakufa kila siku,ila waliokufa hapo natumai kabisa kuwa saa na dakika zao pamoja na sekunde na sehemu ambayo watakufa zinalingana wanaweza kupishana muda wa kutoka roho tu ndio mkawaona wengi.
Kuna uyo jamaa apo nyuma ya vyuma amelala hata hana habari sijui alikuwa amekwisha kupata nibu. Sasa hatujui hata tusafirie chombo gani ?
 
Hatari nyingine tena.
Hivi suala la mawasiliano kwa nini linapuuzwa? Ni kwa nini treni mbili zigongane? Ama ndo kusema kuna njama imepangwa?

Asikufiche mtu maximum speed ni 50km/h kwa maeneo mazuri ambayo yako sehemu za Tabora tu. Sehemu nyingine max speed ni 30kph. Kwa kuangalia tu kanuni za mwendo na fatality za ajali utagundua kuwa mambo yanaenda kienyeji mno.

Kwa nini watanzania tunauana???

wewe lile lilokomotivu linatoka bunduki acha mchezo kabisa
 
BBC wakimhoji Mkuu wa Mkoa Lukuvi, leo jioni watu 15 ndo hadi sasa wamefariki.

Wengine bado wapo trapped ndani na Mashine kubwa inasubiriwa toka Ddma kuweza kukata vyuma na kuwatoa watu zaidi!

Treni ya abiria iligonga Treni ya Mizigo iliyokuwa imeharibika na kusimama!

Huu ni uzembe Mkubwa!

Poleni Watz wote mliofiwa na Mungu azilaze mahala pema peponi wote walipoteza maisha. Amen!
 
Treni ukute zinapita maeneo hayo once a week.
Wenzetu treni zinapishana kwa sekunde.
Kwa mwendo huu tutaendelea?
 
Hii ni serikali ya kuhuni sana ,samahani naomba mwongozo hivi mtu akipanga kupinduwa nchi anakuwa na makosa??

Anakuwa na makosa pale mapinduzi yanapokwama. Akifanikiwa kupindua anatambulika kuwa ni kiongozi halali
 
Last edited:
kwa kweli ni uzembe wa hali ya juu, na hili watu wanaweza kuanza kumlaumu Mwalimu
 
kwa kweli ni uzembe wa hali ya juu, na hili watu wanaweza kuanza kumlaumu Mwalimu

...ningekuwa msemaji wa TRC ningesingizia TANESCO walikata umeme mawasiliano yakawa duni.

Mwenyezi Mungu awarehemu waliotangulia, na awape nafuu majeruhi wote.
 
Imefika wakati watendaji wote wa vyombo vya moto wawe wanakwenda kupimwa akili zao kwa lazima kila mwaaka, maana naona unaweza ukampa maelekezo sahihi mtu kumbe wakati wa utekelezaji kichaa kimemjia akafanya tofauti na alivyoelekezwa.

Kwa jinsi ninavyojua, treni yoyote inapoelekea kwenye kituo lazima mawasiliano yafanyike ili kupata kibari toka kituo kingine. Bila kibari, tren hairuhusiwi kuondoka. Hivyo basi kama ni treni la mizigo lilikuwa limepewa njia, likaharibika njiani, signal ingeendelea kuonyesha kuwa kuna tren linakuja hivyo treni la abilia lingeendelea kusubiri. Sasa ilikuwaje treni la abiria likaruhusiwa kuingia kwenye njia ambayo tayari treni lingine lipo linakuja? hapa napata picha kuwa kuna watu wamechanganyikiwa wameachwa kusimamia vyombo vya moto au IQ zao ni ndogo sana kiasi kwamba kumbukumbu zao hupotea kwa muda mfupi. Ili tusiendelee kupoteza maisha ya watu wasio na hatia tuanze kuwapima akili zao kama wanavyofanya kwa waongoza Ndege ambao hupimwa kila baada ya miaka miwili.
 
Wadau ni vyema reli ya kati iwe ya kusafirisha mizigo kwani kwa mtindo huu wa ajali za uzembe hivi. zitamaliza maisha ya wa-Tanzania...nadhani hizo stesheni hazina hata mtu aliye stand-by kutoa taarifa kwenye stesheni nyingine... Hivi sisi wa-Tanzania tumelogwa??? inawezekanaje treni iharibike...halafu hata huyo Driver wa Treni ya kwanza kushindwa kutumia njia za awali/kijima/kizamani kutoa taarifa... mfano kutuma mtu kutoka pale apepee shati/reflector/taa/majani etc kama kilomita 5 hadi 3??? Kwa wale mliosoma vitabu vya zamani mnakumbuka kuna hadithi ya kijana ambaye aliokoa roho za watu katika kitabu cha kidhungu cha wale waliosoma darasa la kwanza miaka ya sabini na mwanzo ya themanini... baada ya daraja la reli kuzolewa na maji...
Ukiachilia mbali uzembe wa Ma-PRIMITIVE STATION MASTERS lkn hiyo sheria hapo juu itambana driver wa train ya awali ya mizigo!!! RIP wahanga mliohusika... poleni wafiwa... MACHOZI YANANILENGA-LENGA...
 
Tanzania train crash 'kills 15'
BBC News Online

At least 15 people have died after a passenger train ploughed into a stationary cargo train in Tanzania.

Bodies of other victims may be trapped in the wreckage in the Dodoma region of central Tanzania, officials say.

William Lukuvi, Dodoma's regional commissioner, said he feared the number of dead would rise.

He said cranes had been ordered to move the wreckage of the trains after the crash, which occurred around midday local time on Sunday.

"We are investigating the cause of the accident, which has already claimed at least 15 lives," Mr Lukuvi told the Associated Press news agency.

"Cranes have been ordered to help separate the crumpled wreckage and retrieve bodies."

Tanzania Broadcasting Corporation said the accident happened in Pandambili, in Dodoma's Mpwapwa District.

In 2002, more than 200 people were killed and hundreds more wounded when a freight train collided with a passenger train outside Dodoma, the worst rail accident in the country's history.
 
Tuwaombee marehemu kwa Mungu awapokee mikononi mwake.

Kama ajali ilitokea kati kati ya mchana Jumapili, mbona habari zimechelewa sana kutufikia?

"Amri" ya crane kutumika katoa nani? Inatakiwa kuwa na First Responders kila mkoa, na wawe na vifanyia kazi. Inawezekana idadi ya waliokufa kuwa kubwa kutokana na kukosekana kwa SEARCH AND RESCUE crews.

Umefika wakati tuwe na kikundi maalumu cha Search and Rescue. Lazima kiwe na helicopter na vifanyia kazi vingine.

Ni matumaini yetu kwamba utafanyika uchunguzi madhubuti ili tusirudie makosa.
 
Tayari hii thread ipo na inaendelea.... just have them into one please
 
29 March 2009

BBC NEWS | Africa | Tanzania train crash 'kills 15'

At least 15 people have died after a passenger train ploughed into a stationary cargo train in Tanzania.
Bodies of other victims may be trapped in the wreckage in the Dodoma region of central Tanzania, officials say.
William Lukuvi, Dodoma's regional commissioner, said he feared the number of dead would rise.
He said cranes had been ordered to move the wreckage of the trains after the crash, which occurred around midday local time on Sunday.
"We are investigating the cause of the accident, which has already claimed at least 15 lives," Mr Lukuvi told the Associated Press news agency.
"Cranes have been ordered to help separate the crumpled wreckage and retrieve bodies."
Tanzania Broadcasting Corporation said the accident happened in Pandambili, in Dodoma's Mpwapwa District.
In 2002, more than 200 people were killed and hundreds more wounded when a freight train collided with a passenger train outside Dodoma, the worst rail accident in the country's history.
 
Kuna taarifa ya kutokea ajali nyingine mbaya kwenye machimbo ya dhahabu katika kijiji cha mugusu wilayani Geita. Inasemekana idadi ya watu wasiopungua 20 wamefukiwa na kifusi usiku wa kuamkia leo na timu ya uokoaji inaendelea na zoezi hilo. Hii ni wiki ya balaa ukianzia ajali ya bajaj ya mheshimiwa chenge, ajali ya treni na hii tena ya machimbo!!!
 
WATU 16 wamejeruhiwa na wengine kufa baada ya treni ya abiria kugongana na treni ya mizigo Mkoani Dodoma.

Ajali hiyo imetokea leo alfajiri katika eneo la stesheni ya Msagali iliyopo Mkoani Dodoma.

Treni iliyobeba abiria ilikuwa inatokea Dar es Salaam kuelekea Mikoa ya Kanda ya Ziwa iligongana na na treni ya mizigo na kusababisha majeruhi na vifo kadhaa.

Taarifa za harakaharaka kutoka kwa maofisa wa stesheni hiyo zilisema kuwa treni ya mizigo ambayo ilikuwa inatokea Mkoani Mwanza iliivaa treni hiyo ya abiria.

Hivyo kusababisha treni iliyokuwa inatokea Dar es Salaam kuelekea njia hiyo kugongwa na kusababisha ajali hiyo.

Hivyo juhudi za uokoaji wa miili iliyokwama kwenye treni hiyo inaendelea na inafanywa ikishirikiana na vikosi vya uokoaji ili kubaini idadi kamili ya watu waliopoteza maisha katika ajali hiyo
 
Jamani mbona sielewi,zimegongana katika mazingira gani?inamana zote husafiri kwa wakati mmoja?ina maana hakukuwa na mawasiliano? Au ndo yale yale ya Tanzania yetu... UZEMBE!!!
 
Jamani mbona sielewi,zimegongana katika mazingira gani?inamana zote husafiri kwa wakati mmoja?ina maana hakukuwa na mawasiliano? Au ndo yale yale ya Tanzania yetu... UZEMBE!!!

Mkuu, visababishi vya ajali ni kuwa: Stesheni ya Msagali ilikuwa imeshafungwa kwa siku nyingi na ilikuwa haitumiki na kwa hiyo mawasiliano ya uhakika na stesheni inayofuata, Madreva wa treni za mizogo huwa na tabia ya kusimama eneo hilo kupakia mizigo ya magendo na kuuza diesel ya treni (ka-EPA kao nao) na hili lililohusika lilisimama kwa nia hiyohiyo, Treni la abiria liliruhusiwa kwa KUKISIA kuwa lile la mizigo limeshafika stesheni inayofuata (hakukuwa mawasiliano) na hivyo kulifumania la MIZIGO bado linapakia magendo / uza diesel, na ndipo bongo la mzinga likatokea na watu 7 kufariki na uharibifu mkubwa wa mali kutokea. Baada ya tukio Madreva wote wamekimbia (kwa kumuiga yule wa bajaj), Stesheni master wa pande mbili (treni itokako na iendako) nao wakakimbia, Utawala (Mkoa na Serikali kuu) umeagiza Madreva nna Master husika wakamatwe!!!!! Licha ya ajali kutokea alfajiri, Mwekezaji Mindi (Kuch Kuch) katinga eneo la ajali saa 10 jioni bila vifaa vya uokozi nk, masaa mawili baada ya waziri wa Miundo Mbinu Dr. Kawambwa kufika eneo la tukio akitokea jimboni kwake. Kweli Tanzania shamba la bibi, Mhindi anaenda kwa raha zake kwenye tukio la ajali iliyoua ajali!!!!!
 
Tanzania train wreck 'deliberate'​
Police in Tanzania suspect a train crash that left seven people dead was caused deliberately so that petrol could be stolen from the fuel tanks.

Seven people have been arrested, including the driver of the cargo train and the station master. The initial death toll was thought to have been 15.

In Sunday's incident, a passenger train hit a stationary cargo train near the town of Dodoma, in central Tanzania.

It happened near Pandambili in Dodoma's Mpwapwa District, local media say.

William Lukuvi, Dodoma's regional commissioner, told AP news agency: "Cranes have been ordered to help separate the crumpled wreckage and retrieve bodies."

In 2002, more than 200 people were killed and hundreds more wounded when a freight train collided with a passenger train outside Dodoma - the worst rail accident in the country's history.

Correspondents say most of Africa's railways date back to colonial times.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom