Treni ya abiria yapata ajali Dodoma | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Treni ya abiria yapata ajali Dodoma

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Sekenke, Mar 29, 2009.

 1. Sekenke

  Sekenke Senior Member

  #1
  Mar 29, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 132
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Jumapili, 29 Machi 2009, Saa Mbili na Robo Asubuhi. TBC wametoa taarifa hii fupi kimaandishi kwenye luninga:

  Treni ya abiria imegongana na treni ya mizigo katika eneo la Msagali na Gulwe wilaya ya Mpwapwa. Tayari waokoaji wameanza kupasua behewa moja la treni ya abiria ili kutoa watu waliomo ndani.
   
 2. S

  Son of Alaska JF-Expert Member

  #2
  Mar 29, 2009
  Joined: Jun 2, 2008
  Messages: 2,813
  Likes Received: 102
  Trophy Points: 0
  LETS HOPE,they are no fatalities
   
 3. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #3
  Mar 29, 2009
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,316
  Likes Received: 1,784
  Trophy Points: 280
  Lets hope hakuna maafa.But it sounds odd...no journey planning or it is because of poor communication
   
 4. Ilulu

  Ilulu Senior Member

  #4
  Mar 29, 2009
  Joined: Mar 22, 2008
  Messages: 161
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Jirani yangu katumiwa ujumbe wa simu toka kwa rafiki yake aliyeko Dodoma kuwa kuna uvumi watu 100 wamefariki ktk ajali hiyo. walioko karibu wajaribu kufuatili kutapa ukweli wa kina wa taarifa hii..
  Nawasilisha
   
 5. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #5
  Mar 29, 2009
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Inahuzunisha -- hasa vifo vya raia wasiokuwa na hatia. nauliza: Hizo treni ziligongana zikiwa zinarudi kinyumenyume? na hivyo madereva hawakuonana? Msishangae kwani miaka kadha iliyopita watu 300 walikufa kwa ajali ya treni ya abiria iliyokuwa inarudi kinyumenyume!
   
 6. M

  Mundu JF-Expert Member

  #6
  Mar 29, 2009
  Joined: Sep 26, 2008
  Messages: 2,719
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Ajali nyingi za Tanzania ni matokeo ya uzembe. Kinachosikitisha ni kuwa hakutakuwa na hatua zitakazochukuliwa kwa wahusika. Kilio kinabaki tu kwa wale wahanga waliokumbwa na ajali hizi.

  Mungu na atunusuru.
   
 7. The Farmer

  The Farmer JF-Expert Member

  #7
  Mar 29, 2009
  Joined: Jan 7, 2009
  Messages: 1,581
  Likes Received: 433
  Trophy Points: 180
  Yani Tanzania inamatatizo sana, mpaka Treni zinagongana! mawasiliano hakuna kabisa kati ya Railway station moja na nyingine. Mh lakini kama waokoaji ndio wanakata behewa la treni ya abiria ili kuwatoa walioko ndani ya behewa hilo basi impact itakuwa ni kubwa sana na kuna uwezekano wa kuwa na Fatality.
   
 8. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #8
  Mar 29, 2009
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,001
  Trophy Points: 280
  Asilimia kubwa ya ajali zetu ni uzembe tu, kwa impact ya aina hiyo fatality ni lazima
  we needs changes
   
 9. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #9
  Mar 29, 2009
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Uzembe ambao pia umechangiwa na mwekezaji mbovu. Baada ya kupata mwekezaji mpya tulitumaini ajali hizi za treni za abiria zingetoweka -- kama vile wakati wa ukoloni -- kulikuwa hakuna, au nadra mno, kwani treni za abiria kuleta ajali na kuua kwani zilikuwa zinaangaliwa sana kiusalama.

  Hakuna sababu kwa nini hicho kisifanyike hivi sasa. Siku hizi mambo ni bora twende -- treni za abiria zinaendeshwa kama vile ni za mizigo.

  Waziri husika -- Shukuru Kawambwa, inapasa ajiuzulu. Ni kweli, hakuwa anaendesha treni hizo au kuwepo katika eneo la ajali, lakini ni bora sasa afungue njia kwa serikali ya JK kuwajibika -- kumsaidia swahiba wake kuleta heshima ktk utawala wake. Najua kuna watu watamtetea kwa hili! Hawa wanaendeleza tu hali ya kutokuwepo utamaduni wa uwajibikaji.

  Ubinafsishaji wa TRC kwa mwekezaji huyu umekuwa unalalamikiwa sana, kutokana na huduma duni katika uendeshaji wa shirika hilo na kwamba kuna dalili nyingi ubinafsishaji ulikuwa ni wa kifisadi.

  Hivyo ajali hii itaongeza kuwasha moto. Na bila shaka kuna watu humu ktk JF hivi sasa wanaanza kuchonga kalamu zao kuzidi kutetea ufisadi huo na hata ajali yenyewe, kwamba ni ajali tu, haihusiani kabisa na mwekezaji mpya.
   
 10. Buswelu

  Buswelu JF-Expert Member

  #10
  Mar 29, 2009
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 1,989
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Imegongana na tren ya mizigo kwenye mabehewa mawili ya nyuma mpaka sasa ni watu wawili comfirm kufa...majeruhi wapo...na kuna behewa jingine ndio wametuma mafundi kwenda kulikata kuona nini....kitajiri
   
 11. 911

  911 Platinum Member

  #11
  Mar 29, 2009
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 761
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 60
  Kilele cha uzembe!Period
   
 12. The Farmer

  The Farmer JF-Expert Member

  #12
  Mar 29, 2009
  Joined: Jan 7, 2009
  Messages: 1,581
  Likes Received: 433
  Trophy Points: 180
  kilele cha uzembe ni kupata Dictator ambaye anaweza kutupigisha kwata na mchakamchaka hata kwa mwaka mmoja, uzembe na ufisadi utakwisha!
   
 13. Victoire

  Victoire JF-Expert Member

  #13
  Mar 29, 2009
  Joined: Jul 4, 2008
  Messages: 10,445
  Likes Received: 7,185
  Trophy Points: 280
  kwa nini uzembe unagharimu maisha ya watu wasio na hatia?inatia sana hasira yaani treni kugongana?ina maana hakukuwa na mawasiliano?
  Yaani inaudhi sana tena sana!
   
 14. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #14
  Mar 29, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Inahuzunisha sana tena mno train zigongane?Hakuna mawasiliano?Zinaenda kwa kuviziana nyingine ipack au ndo hivyo mastetion master wanasikiliza mlio wa mataruma kuwa ipo jirani?Tutaendelea kuwakumbatia wazembe mpaka lini jamani?Amkeni jamani.
   
 15. Timtim

  Timtim JF-Expert Member

  #15
  Mar 29, 2009
  Joined: Feb 9, 2008
  Messages: 603
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 45
  Wakuu atakaepata data za ziada atupe. Huu msiba wa wote. Haina haja kulaumiana kwa sasa.
   
 16. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #16
  Mar 29, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Mods unganisha na ile ingine ambayo ipo tayari.
   
 17. BabaH

  BabaH JF-Expert Member

  #17
  Mar 29, 2009
  Joined: Jan 25, 2008
  Messages: 703
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Jamani tuelezeni, nini kinaendelea hapo, na je kuna waliopoteza maisha
  kwa sababu kwa sasa ni kujua hali ya abiria waliokuwa wakisafiri na hiyo treni
  Eeh Mungu tusaidie Watanzania
  Maana viongozi wenyewe ndo hao, full uzembe kila siku linatokea lingine na hakuna lolote linalofanyika ili kuzuia uzembe huo
   
 18. Mkereketwa

  Mkereketwa JF-Expert Member

  #18
  Mar 29, 2009
  Joined: May 19, 2007
  Messages: 202
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kun utata hapo,nilikuwa nafuatilia Clouds FM wanasema inawezekana zaidi ya 5 wamekufa papo hapo.
   
 19. Ngonalugali

  Ngonalugali JF-Expert Member

  #19
  Mar 29, 2009
  Joined: Jan 12, 2008
  Messages: 658
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 0
  Hatari nyingine tena.
  Hivi suala la mawasiliano kwa nini linapuuzwa? Ni kwa nini treni mbili zigongane? Ama ndo kusema kuna njama imepangwa?

  Asikufiche mtu maximum speed ni 50km/h kwa maeneo mazuri ambayo yako sehemu za Tabora tu. Sehemu nyingine max speed ni 30kph. Kwa kuangalia tu kanuni za mwendo na fatality za ajali utagundua kuwa mambo yanaenda kienyeji mno.

  Kwa nini watanzania tunauana???
   
 20. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #20
  Mar 29, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  [​IMG]

  [​IMG]

  [​IMG]


  Source: Mzee wa Sumo
   
Loading...