Treni Imeanza Kazi Dar Es Salaam (Dar Subway)

Treni Imeanza Kazi Dar Es Salaam (Dar Subway)

MaxShimba

Platinum Member
Joined
Apr 11, 2008
Posts
36,008
Reaction score
4,093
Treni ya abiria iliyoanza kazi leo Dar es Salaam ikiwa kituo cha Ubungo Maziwa​

Baadhi ya abiria wakipanda kwenye treni kituo cha Ubungo Maziwa kabla ya kuanza safari kuelekea katikati ya jiji.​

Baadhi ya abiria wakikata tiketi za treni muda mfupi kabla ya kuondoka kuelekea katikati ya jiji la Dar es Salaam.​

Baadhi ya wafanyakazi wa TRC wakiendelea kukatisha tiketi ndani ya treni kwa abiria wanaopandia njiani ama kutokuwa na tiketi wakati wa safari.​

Hapa ni ndani ya behewa la treni kama linavyoonekana kwenye picha​
Na Joachim Mushi
USAFIRI wa kutumia treni jijini Dar es Salaam kutokea eneo la Ubungo Maziwa kuelekea katikati ya Jiji la Dar es Salaam (Stesheni ya Treni) umeanza leo. Treni ya kwanza imeondoka Ubungo majira ya saa 12:00 asubuhi kuelekea katikati ya jiji, ambapo kwa mujibu wa maofisa wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) imetumia wastani wa dakika 30 kufika katikati ya jiji.
Treni ilioanza kazi leo iliyokuwa na injini mbili (vichwa vya traini) moja ikiwa imefungwa nyuma na nyingine mbele huku ikiwa na mabehewa sita, yaani matano ya abiria wa kawaida (watu wazima) na moja likiwa ni maalumu kwa ajili ya kubeba wanafunzi. Abiria mmoja ni sh. 400 kwa tripu huku wanafunzi wakitakiwa kulipa sh. 100 kwa kila mmoja.
Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe ndiye aliyezindua usafiri wa leo ambao ni wamajaribio, akiwa pamoja na viongozi waandamizi kutoka TRC, Mamlaka ya Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA), TAZARA pamoja na Polisi Kitengo cha Reli. Treni hiyo pia imezinduliwa pamoja na treni ya TAZARA ambayo itafanya kazi kama ya Ubungo, lakini yenyewe ikianzia eneo la TAZARA kuelekea Mwakanga.

Kwa utulivu na usafiri wa starehe kama hivi kwanini usisome gazeti ukiwa safarini..! Abiria akijisomea gazeti ndani ya treni leo kama alivyonaswa na mpigapicha.​

Akizungumza mara baada ya ufunguzi huo Waziri Mwakyembe alisema atahakikisha treni hiyo inaendelea kufanya kazi ili kuwasaidia kiusafiri wananchi wa Dar es Salaam ambao wamekuwa wakisumbuliwa na kero ya usafiri hasa kwa foleni, ambapo utumia muda mrefu njiani kuingia na kutoka jijini.Alisema jumla ya mabehewa ya treni 14 pamoja na injini mbili zimekarabatiwa na mafundi wazalendo nchini, ambayo ndiyo yatakayokuwa yakifanya kazi ya kusafirisha abiria kuingia na kutoka jijini kila asubuhi na jioni. Alisema kwa sasa inafanya treni moja kwa majaribio lakini baada ya uzinduzi mkubwa zitafanya kazi treni mbili, na zitakuwa zikipishana njiani moja ikirudi na nyingine ikienda.

Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe (katikati anayepunga mkono dirishani) akiwa na baadhi ya viongozi walioshiriki katika uzinduzi wa treni leo.​

Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe (aliyesimama) akizungumza kwenye hafka fupi ya uzinduzi mdogo wa treni ya abiria jijini Dar es Salaam leo. Wengine ni baadhi ya viongozi walioshiriki katika uzinduzi huo.​

44504_495602323797488_1510482659_n.jpg

373990_283815475070980_715311811_n.jpg

431691_546660822027539_703270575_n.jpg

IMG_00111.jpg

Leo baadhi ya wakazi wa jiji la Dar-es-Salaam wameanza rasmi matumizi ya usarifi wa kutumia treni. Una maoni yeyote juu ya usafiri wa treni jijini?
 
mkuu Mbuzi Mzee!zile za kwenda mkoani huwa zina choo!!vipi hizi nazo zina choo kwa abiria wake!!!
 
Last edited by a moderator:
It's an offense calling it a subway!

Kiasi itasaidia kupunguza muda tunaopoteza katika foleni.
Cha muhimu kuzingatia muda, na uwe ni usafiri wa UHAKIKA! (sio leo upo then kesho tunaongea mengine)

Much effort iwekwe kwenye RBT,na watu wawe encourage kutumia than private cars(only if kukiwa na Safe/Secured Vehicle park)!
 
Why do you think it is improper to call it "subway"?

Hebu nenda Nigeria ujionee wanavyo safikiri na boda boda, ndipo unaelewa kuwa Bongo Wanaanza kupiga hatua. Just thinking loud.
 
hizo train zinapiga route za wapi? Mbagala pia inakwenda.
 
  • Thanks
Reactions: awp
pamoja na kero za dala dala uliwahi kuona huduma ya choo? kama ukijisikia umevimbiwa lisha bata

Mkuu hata Subway za NYC hazina choo, sasa kwanini za Bongo ziwe na Choo ndani ya Behewa. Mbona Wabongo mna makuu nyie.
 
pamoja na kero za dala dala uliwahi kuona huduma ya choo? kama ukijisikia umevimbiwa lisha bata
ha ha ha ha!!tunaongelea tren mkuu!!au huyafahamu mabehewa ya tren yalivyotengenezwa,hususan tren zetu za bongo!!!!!!kila behewa lina choo,je wameviziba au vipo!!!unatapikia kwenye vidole!!
 
Watanzania tumuunge mkono kiongozi Dr.Harison Mwakyembe ametuonyesha njia kumbe hili linawezekana. Tuyatunze hayo mabehewa ya treni, ikitokea mtu anafanya uharibifu kama uliotokea uwanja wa taifa tumripoti kwa wahusika.
 
hizo train zinapiga route za wapi? Mbagala pia inakwenda.

Mkuu zinaanzia UBUNGO-STESHENI KUU kwa treni inayotumia RELI YA KATI.TAZARA inaanzia MWAKANGA-KURASINI, kumbuka treni inapita kwenye reli sasa MBAGALA inakujaje hapa. Ikiwa utapanda lazima ulingoje KURASINI,MTONI
 
Usafiri wa treni jijini Dsm utasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza tatizo la usafiri hasa muda wa asubuhi na jioni endapo tu utakuwa ni mpango endelevu. Haya ndio tunaita maendeleo, yaani katika hatua moja kwenda hatua nyingine iliyo bora zaidi. Chonde chonde Mh. Mwakyembe kesho msije sema mara ooooh leo treni hakuna maana imepata pancha, mara oooooh treni hakuna leo iko service.

Pongezi kwa Mh. waziri Mwakyembe na safu yake yote, pongezi kwa serikali ya Mh. J. M. Kikwete. Pongezi kwa serikali ya CCM. Mawaziri wengine waige katika kutekeleza ahadi wanazo toa kwani huu ni mfano mzuri.

Wenye roho za kwa nini wataanza kuhoji na kuponda ovyo kwani wao huwa hawaoni zuri la serikali ya CCM. Mimi nasema (kama Mh. Pinda - liwalo na liwe) hivi MNYONGE MNYONGENI LAKINI HAKI YAKE MPENI!!!
 
Tunashauri isiwe nguvu ya soda. Maana watu wetu wanateseka bila sababu kutokana na kuwa na utawala usio na akili wala mipango zaidi ya kupiga deals. Na wananchi nao waitumie vizuri siyo kuiharibu kwa vile ni mali ya umma ambao ni wao wenyewe. Laiti hata vyoo vya Mnazi mmoja vingefufuliwa ili watu wakaachana na kuaibika na kuchafua mazingira.
 
Usafiri wa treni jijini Dsm utasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza tatizo la usafiri hasa muda wa asubuhi na jioni endapo tu utakuwa ni mpango endelevu. Haya ndio tunaita maendeleo, yaani katika hatua moja kwenda hatua nyingine iliyo bora zaidi. Chonde chonde Mh. Mwakyembe kesho msije sema mara ooooh leo treni hakuna maana imepata pancha, mara oooooh treni hakuna leo iko service.

Pongezi kwa Mh. waziri Mwakyembe na safu yake yote, pongezi kwa serikali ya Mh. J. M. Kikwete. Pongezi kwa serikali ya CCM. Mawaziri wengine waige katika kutekeleza ahadi wanazo toa kwani huu ni mfano mzuri.

Wenye roho za kwa nini wataanza kuhoji na kuponda ovyo kwani wao huwa hawaoni zuri la serikali ya CCM. Mimi nasema (kama Mh. Pinda - liwalo na liwe) hivi MNYONGE MNYONGENI LAKINI HAKI YAKE MPENI!!!

mia kamanda.
 
Why do you think it is improper to call it "subway"?

Hebu nenda Nigeria ujionee wanavyo safikiri na boda boda, ndipo unaelewa kuwa Bongo Wanaanza kupiga hatua. Just thinking loud.

Maybe because it ain't a Subway

[FONT=arial,sans-serif][SIZE=-1]sub·way[/SIZE][/FONT] (s
ubreve.gif
b
prime.gif
w
amacr.gif
lprime.gif
) [SIZE=-2]KEY[/SIZE]

[SIZE=-1]NOUN:[/SIZE]

    1. An underground urban railroad, usually operated by electricity.
    2. A passage for such a railroad.
  1. An underground tunnel or passage, as for a water main or for pedestrians.
 
Maybe because it ain't a Subway

[SIZE=-1]sub·way[/SIZE] (s

Some lines in NYC don't even go underground and still is SUBWAY.
 
subway.1.jpg

Angalia Number Seven ikielea Shia Stadium sasa inaitwa Citi

Hapa chini angalia namba moja ikikatisha Harlem NYC

1272706233.jpg
 
Maybe because it ain't a Subway

[SIZE=-1]sub·way[/SIZE] (s
ubreve.gif
b
prime.gif
w
amacr.gif
lprime.gif
) [SIZE=-2]KEY[/SIZE]

[SIZE=-1]NOUN:[/SIZE]

    1. An underground urban railroad, usually operated by electricity.
    2. A passage for such a railroad.
  1. An underground tunnel or passage, as for a water main or for pedestrians.

Kwa tafsiri hiyo basi haitakuwa subway, bali itakuwa metro
 
Back
Top Bottom