Transvestism | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Transvestism

Discussion in 'JF Doctor' started by X-PASTER, Nov 2, 2009.

 1. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #1
  Nov 2, 2009
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  TRANSVESTISM

  Haya ni maradhi au kichaa cha mtu kupendelea mavazi au mapambo ya watu wa jinsia nyingine. Maradhi haya hurandana sana na yale ya Transsexualism, lakini wengi pia hupenda kujipamba kwa vipambo vya watu wa jinsia nyingine bila ya wao kuwa na silka za watu hao.

  Haya ni maradhi ya mwanaume kupenda kuvaa nguo au mapambo ya kike, au mwanamke kupenda kuvaa nguo za kiume. Mwenye maradhi haya huitwa Transvestite. (Husomwa Transevestait)

  Wenye maradhi haya walio wengi ni wanawake, hawa ni sawa na wale wanao ielewa vibaya dhana ya "usawa". Ni nadra kumkuta mwanaume amevaa sketi na blauzi, lakini siku hizi tunawaona wanaume waliotoboa masikio na kuvaa hereni, na wengine huacha vifua wazi ili mikufu yao ya dhahabu ionekane.

  Wagonjwa wengi wenye maradhi haya wako kule Ulaya na Marekani. Wagonjwa walio huku kwetu mara nyingi huambukizwa maradhi haya kwa kupitia Mavazi mapachiko (Programmed Mind) kwamba chochote wanachokifanya watu wa Ulaya na Marekani ndiyo maendeleo, kwa hiyo vijana huiga yanayoonekana kwenye televisheni hata kama yanafanywa na wanaume mashoga. Hivyo, Trasvestite wengi wa humu kwetu huwa na maradhi mengine yanayoitwa Copycatism, ugonjwa wa kuiga bila ya kuelewa maana ya kinachoigwa.

  Wagonjwa wa kike wa maradhi haya mara nyingi huwa na michanganyiko ya maradhi. Mwanamke anayevaa nguo za kiume, hasa makaptula au suruali na shati, mara nyingi huwa na maradhi ya Sexual Sadium, kwa kupenda wanaume wahemkwe kwa umbile lake popote anapopita, kwa vile huziacha wazi sehemu zake za mvuto.

  Pili, mgonjwa huyu wa kike pia yawezekana kuwa ameathirika na wazo mpachiko la kuwa "sawa" na wanaume, kwa hiyo labda yeye ni Transsexual.

  Tatu inawezekana kuwa ni miongoni mwa malimbukeni ambao wako ndani ya hali ya kuchanganyikiwa kiasi cha kutojielewa afuate mila gani (Identity Crisis) na ndipo wanaishia kuwa Copycats kila siku wanaangalia Mzungu kavaaje ili na yeye avae hivyo.

  Kwa hiyo siku Mzungu akivaa gunia basi na yeye unaweza kumkuta mitaa ya Tandale akichagua magunia matupu akashone vazi aliloliona kwenye luninga. Wagonjwa wengine hurithishwa tabia ya kuvaa kiume tangu wadogo, hivyo wazazi malimbukeni huchangia sana katika kutengeneza jamii ya ma-Transvetite. Mara nyingi watoto wa kike tu ndio huzoeshwa kuvaa mavazi ya kiume, lakini sijapata kuona watoto wa kiume (waliofikia umri wa kukimbia) wakivalishwa vigauni au wakatogwa masikio.

  Wanaoshangaza zaidi ni wale wagonjwa wa kiume wanaotoga masikio na kuvaa hereni na vidani. Hawa nao huenda ni Transsexuals, wana shauku ya kuwa wanawake, ila tu kwa bahati mbaya huku kwetu hakuna hospitali za kufanyia operesheni, pengine wangependa kubadilishwa viungo vyao vya mwili vinavyowafanya wanaume. Kama sio madume jike (transsexuals) basi ni malimbukeni waliopapia miji. Au wako kwenye vurugu la mawazo ua kujitambua (identity crisis). Au pengine labda ameona wanawake wamependelewa kwa kuachiwa wapendeze peke yao, kwa hiyo na yeye anataka apendeze kama dada zake, au mabinti wa jirani.

  Cha kumuuliza ni:

  Unataka upendeze kama akina dada ili iweje? Halafu ukishapendeza watu wakikupenda, wafanyeje? Labda walete posa!

  Uislamu umechukua zaidi tahadhari kwa wanawake Waislamu wasije wakawaiga majahili katika kujipamba, kwa kuwaambia:

  "... Wala msijipambe kujipamba kwa majahili waliopita (yaani msiwaige majahili)"
  Q33:33


  Abu Hurairah amesema kwamba Mtume Muhammad (s.a.w.) amewalaani wanaume wanaovaa mavazi ya kike na wanawake wanaovaa mavazi ya kiume.
  Abu Daud
   
Loading...