Transfer Window updates 2013/2014 season - Europe

Transfer Window updates 2013/2014 season - Europe

David Moyes anasema Wayne Rooney haondoki ManUtd.
Carlo Ancelotti anasema Higuain haondoki Real Madrid
 
Anelka alikuwa Juventus nusu ya pili ya msimu uliopita, lakini alicheza mechi 3 tu.

We umeongea.....sio huyo hapo juu anajiona mpira anaujua peke yake...sikuwa aware kabisa na hii deal
 
Takriban siku 40 kabla ya msimu mpya wa EPL kuanza timu zote kubwa zimeshaanza kufanya usajili wa nguvu, ...kasoro ARSENAL tu! Alichofanya mzee Wenger hadi sasa ni kumchukua kinda mfaransa Yaya Sanogo (free transfer)
 
kichwat

Tunashukuru kwa newz unayotuangushia.
Na ingali nilikuwa mbali na mji ila hakika baada ya kutua na kutinga ndani ya Jf hakika nimefarijika!

Hakika kichwat tu pamoja mwanzo mwisho Kamanda wangu!
 
Last edited by a moderator:
Paulinho ametua Tottenham kwa dau la £17m.



Hii peleka pale juu kwenye thread ni muhimu kwa wadau wa soka wapitie Mkubwa!
Na kuna hili la kiungo matata wa Liverpool FC (Njonjo) kuihama club na kujiunga na Swansea City na ameuzwa moja kwa moja!
 
Mshambualiaji Arouna Kone (29) amehamia Everton kwa dau linalofikia £6.5m, mkataba wa miaka 3. Kone alikuwa Wigan pamoja na kocha Roberto Martinez msimu uliopita.
 
Arsenal bado wanamatumaini makubwa ya kukamilisha dili la kumchukua Gonzalo Higuain, pamoja na longolongo zote wanazowekewa na Real Madrid. Mkakati wa Wenger ni kuwapata washambuliaji wawili WAKUBWA kwa msimu ujao.
 
Victor Wanyama ametua Southampton, ndani ya EPL kwa mkataba wa miaka 4.

Wanyama aliitungua Barcelona kwa kufunga bao la ushindi kwenye mechi ya Champions League msimu uliopita.
wanyama.jpeg
 
Jaman, na sisi Newcastle vipi? Kimya? Au ndo kazi yetu kuuza tuu
 
Timu ya Fulham imeuzwa kwa bilionea wa Kimarekani Shahid Khan (62), baada ya kumilikiwa na Mohamed Al Fayed (84) kwa miaka 16, kwa dili linalokadiriwa kuwa £150 - £200m.
Khan anamiliki kampuni kubwa ya vifaa vya magari Flex-N-Gate.
 
Arsene Wenger akiongelea fedha za usajili msimu huu: "We have better financial resources than the years before, and it's the resources WE HAVE CREATED OURSELVES. That's massively important to us."
 
Official: Bayern Munich confirm the transfer of Barcelona midfielder Thiago Alcantara (22), for whom they pay 20M #fcblive
 
hatimaye Edinson Cavani amekamilisha uhamisho kwenda PSG kwa dau la £55.4m baada ya kufaulu vipimo, mkataba wa miaka 5.
 
Luis Suarez (26): Arsene Wenger sasa amepewa RUKSA ya kumwaga dau la £40m. Lakini Liverpool sasa wamepandisha bei hadi £55m.
 
Christian Benteke sasa amebondoka kwenye kelele za usajili baada ya kusaini mkataba wa miaka 4 kuendelea kubaki Aston Villa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom