BABA E's
JF-Expert Member
- Dec 25, 2012
- 354
- 135
Hawa jamaa sasa hivi mbona ni kama wanatukomoa wananchi?, maana akikusimamisha anakuomba leseni hapohapo anaanza kupunch machine yake, hakuna muda wa kukuambia kosa lako na wewe kujitetea, hivi wanafikiri hizi elfu 30 tunaziokota au?. Awali nilifikiri labda sisi wananchi ndio tuna shida lakini leo nimejionea.
Ni kweli kila mtu na kazi yake lakini kuna vitu vinahitaji ubinadamu zaidi. Kwakweli haieleweki kama lengo lao ni usalama barabarani au kukusanya pesa. Na kama naona nimeonewa ni wapi naweza kwenda kudai haki yangu!?.
Waandishi wa habari nafikiri mtusaidie kufuatilia ufanyaji kazi wa hawa askari wetu kwa sasa.