Lengo lao sio Yanga, lengo lao ni rais wa Yanga, Injinia Hersi Said

bryan2

JF-Expert Member
Jun 8, 2016
3,323
4,667
Hakika ingekuwa kama ni mashambulizi ya kimtandao CYBERATTACKS mpaka sasa Timu ya YANGA ingekuwa inaongoza kwa kushambuliwa na ukiishambulia, Yanga means una mshambulia rais wao Kipenzi rais Kijana aliyeitwa mpaka Rais Mhuni Eng HERSI SAID ila uzuri wa mtu huyu sio mzungumzaji sana sio mtu wa kucheza na media kama upande ule mwingine sio mtu wa Longolongo.

Hakika ni mtu wa vitendo angalia saga la Usajili wa AZIZ Kni mambo mengi sana yaliibuka kila aina ya picha pamoja na machapisho kutoka kwa wanaojiita wachambuzi uchwara wa kibongo ila KIKO WAPI?? Leo Aziz K anachezea Yanga.

Wanayanga tambueni sana maadui wenu hawapo mbali na nyie wengine wanaifahamu club yenu nje na ndani sema tu baada ya mirija yao ya upigaji kufungwa ghafla wamegeuka kuwa maadui wetu haya yote yamefanyika chini ya Rais Kijana Hersi Said sasa unategemea watampenda kweli? Jibu ni hapana.

Ukiangalia kwa sasa hizi propaganda za Usajili zinazoendelea Asilimia 99.99% habari nyingi zinahusu Yanga tena zote ni negative kumbe basi lengo lao ni kuwaonyesha Wanayanga viongozi wenu hawafai na nyie mkikubali kuingia kwenye huu mkumbo ndio furaha yao wapo wachambuzi wengine bila kuisemea Yanga wanapata Zero comment

Wapo wachambuzi wengine leo wamejipambanua wao ni maadui wa Yanga kwao hakuna zuri la Yanga wachambuzi hawa wanatoka kituo kimoja cha Radio sio ajabu baada ya Yanga kupoteza mchezo wa kwanza dhidi ya Usmalgers kwao ilikua ni furaha.

Hivi leo Eng chini ya GSM kiboko cha madoa mtu aliyeamua kuifanya Yanga mpya tena kwa maamuzi magumu kwa kuachana na wachezaji karibia wote na kuanza upya tena Yanga ikiwa kwenye kipindi kigumu haswa leo hii unataka kuniambia ashindwe kunegociate mikataba ya wachezaji na makocha hapana.

Tuelewe YANGA KWA SASA INAJIJENGA KIUCHUMI YANGA INATAKA KUONDOKANA NA KUWA TIMU YA MTU MMOJA NA KUWA TIMU YA WANANCHI, YANGA WANA BAJETI YAO YANGA WANA VIWANGO VYAO VYA MISHAHARA KUTOKANA NA KIPATO CHAO HAIWEZEKANI GHAFLA FROM NO WHERE UNATAKA ULIPWE MSHAHARA WA MILIONI 100 TENA GHAFLA TU HILI HALIPO.

Sisi sisi mashabiki ndio mwisho wa siku tutaanza kelele Viongozi wanakula Fedha zetu kumbe ni Bajeti mbovu na mishahara isiyoendana na uhalisia/Bajeti.

Eng.Hersi Saïd ndio mtu aliyesimamia mchakato mzima wa mabadiliko ndani ya Yanga mpaka leo hii tunaiona Yanga imara angekua mhuni mwingine angekuja na kuchoma zake mwisho wa siku angeondoka huu ni ujasiri wa hali ya juu sana huu ni uzalendo uliopita viwango.

Hivi bila Eng Chini ya GSM nani angemfahamu Morrison, Saido, Mayele, Tk Masta, Moloko, Bangala, Aucho Dr nani alitegemea siku moja atamwona Shabani Djuma yule wa As vita anachezea Yanga hakika vitu vingine vilikua kama ndoto cha mchana ila kwa sasa ni uhalisia.

Nimependa sana viongozi wote wa Yanga walivyoamua kukaa kimya na kuacha medias waseme watakalo ila mwisho wa siku ndio hawa hawa watakuja na kauli zao hii Yanga ya Moto na kuanza kumpa sifa Kemkem Rais wa Yanga.

Wanayanga trust the process huu ukimya sio wa hivi hivi una kitu kizito sana ndani yake.

C&P
 
IMG_8107.jpg
 
Hizo milioni 50 alikwambia wewe kama anazitaka?

Hahaha ajabu sana wanasimba kujifanya mnaumia zaid ya sisi wenye timu. Vip alikwambia wewe anataka ngapi semaji la Yanga.
 
Back
Top Bottom