Jamani nani atakomesha rushwa kwa traffic police? Tarehe 30 July 2016 nimepita njia ya Bagamoyo - Msata mida ya saa 5 asubuhi, ma ma ma ma ma! polisi wa barabarani walijiposition kwenye kibao cha barabarani kilicho andikwa 50 kwenye kona na kifaa chao cha kupima speed ya magari. Jamani!!! Hakuna gari hata moja lililoandikiwa faini ya sh. 30000, magari yooote tulitozwa rushwa ya kuanzia 5000 hadi 10000 tu na kuendelea na safari. Gari langu dogo nimeambiwa nimeendesha speed ya 55km/saa badala 50 na wakati wa kurudi siku inayofuata nikaambiwa nimeendesha km 60. Magufuli rushwa traffic huiwezi bana.