Kwa masikitiko makubwa sana jana usiku wa saa mbili maeneo ya Shekilango Ubungo askari wa kikosi cha barabarani mmoja wapo akiwa amelewa walikuwa na kazi za kuwakamata wenye Bodaboda na wenye magari ambao wametenda makosa na kuwatolesha pesa.
Hakuna aliyeandikiwa faini, walikusanya pesa kwa wakosaji hao mpaka shilingi elfu tano tano huku wakiwa wakali kwa kuwatishia wasipitoa pesa watawapiga faini ya elfu 60 hata kwa kosa la faini ya elfu 30.
Askari hao walienda mbali zaidi kwa kuwatishia kuwaweka mahabusu hata wale waliodai waandikiwe faini ili wasipotezewe muda ambapo waliwaweka kwa muda mrefu bila kuwaandikia ili watoe pesa na kuwaachilia,aidha mmoja wa askari hao ambao hawakuwa na namba za kijeshi kwenye sare zao alikuwa anaanza kudai elfu 20 na kushuka hadi elfu 5 bila ya aibu.
Tunawaomba sana viongozi wao wawafuatilie hususani walioingia kazini maeneo hayo hapo jana siku ya Jumatano tar 15 May 2019 walifanya kitendo cha aibu sana.
Tunawaomba ma RTO 'na ma DTO kuweka namba zao wazi ili yakitokea waweze kupigiwa.
...Hapo ndipo majirani zetu wa Kenya ndipo wanapotuzidi!
Hivi wote mliosimamishwa hapo na mnaona kabisa kuwa jamaa wanavunja sheria ikiwemo kilevi wakiwa kazini na sare za kazi, mlishindwa kuamua kufanya tukio na kuwabeba msobe msobe hadi kituo cha Polisi kilicho karibu??
Napenda kuamini kuwa njiani kuelekea Polisi waheshimiwa hao wenyewe wangewaomba Msamaha...
Bila picha hayo ni majungu we ulishindwa hata kuwaphotoa kwa mbali tuKila siku nasema kuna haja ya kuendelea kuwa na kitengo cha Takukuru?
Huyu mtoa mada analeta majungu tu....Hapo ndipo majirani zetu wa Kenya ndipo wanapotuzidi!
Hivi wote mliosimamishwa hapo na mnaona kabisa kuwa jamaa wanavunja sheria ikiwemo kilevi wakiwa kazini na sare za kazi, mlishindwa kuamua kufanya tukio na kuwabeba msobe msobe hadi kituo cha Polisi kilicho karibu??
Napenda kuamini kuwa njiani kuelekea Polisi waheshimiwa hao wenyewe wangewaomba Msamaha...
Jambo afandeVijana acheni roho ya kimaskini, kwahiyo akiwaandikia 30,000.00 mtafurahi wakati mwingine kazi inatakiwa ikunufaishe, huyo polisi siku akistaafu mtaanza kumcheka kwa namna ambavy maisha yake yatakuwa ya hali ya chini. Kuna ndugu yangu kaastafu miaka 3 iliyopita alikuwa uhamiaji kwakweli anatia huruma.