badoo
JF-Expert Member
- Jan 4, 2014
- 512
- 246
Kwa masikitiko makubwa sana jana usiku wa saa mbili maeneo ya Shekilango Ubungo askari wa kikosi cha barabarani mmoja wapo akiwa amelewa walikuwa na kazi za kuwakamata wenye Bodaboda na wenye magari ambao wametenda makosa na kuwatolesha pesa.
Hakuna aliyeandikiwa faini, walikusanya pesa kwa wakosaji hao mpaka shilingi elfu tano tano huku wakiwa wakali kwa kuwatishia wasipitoa pesa watawapiga faini ya elfu 60 hata kwa kosa la faini ya elfu 30.
Askari hao walienda mbali zaidi kwa kuwatishia kuwaweka mahabusu hata wale waliodai waandikiwe faini ili wasipotezewe muda ambapo waliwaweka kwa muda mrefu bila kuwaandikia ili watoe pesa na kuwaachilia,aidha mmoja wa askari hao ambao hawakuwa na namba za kijeshi kwenye sare zao alikuwa anaanza kudai elfu 20 na kushuka hadi elfu 5 bila ya aibu.
Tunawaomba sana viongozi wao wawafuatilie hususani walioingia kazini maeneo hayo hapo jana siku ya Jumatano tar 15 May 2019 walifanya kitendo cha aibu sana.
Tunawaomba ma RTO 'na ma DTO kuweka namba zao wazi ili yakitokea waweze kupigiwa.