Wakuu,
Hivi mnajua huo utrafiki ulikua unatafutwa kwa nguvu sana ikiwamo askari wenyewe kuhonga ili wapangiwe kua trafiki? Hapa ukweli wanaujua vizuri wao wenyewe.
Tunapenda ukaguzi barabarani wenye tija lakini kama alivostuka mzee kinana ndio watu wengi hujiuliza kila hatua chache unasimamishwa, ilimradi vurugu tu barabarani, unatoka Dar hadi Mwanza au Dar hadi Mbeya ushasimamishwa zaidi ya mara hamsini hivo kupoteza muda wa safari yako bila sababu ya msingi.
Kisa wakusanye 1000 au 2000 au 5000.
Halafu faini za tochi zinazoandikwa kwa siku nchi nzima ni chache kuliko ambazo haziandikwi yaani kwenye tochi wanakanyaga elfu tano hadi elfu kumi kama wanaigiza vile.
Iwekwe idadi kwamba kila mkoa au wilaya au highway vituo vya ukaguzi ni sehemu fulani na sehemu fulani sio usimame maili moja, usimame kongowe, usimame misugusugu yaani unahisi wanakagua serious kumbe wanataka rushwa hawana lolote.
Wana madudu mengi sana afadhali wazee kama Kinana wameyaona na kuwaeleza kwa staha kiutu uzima lakini sisi tunawachana tu hali halisi.