Trafiki mbashara wakusanya rushwa Shekilango

badoo

JF-Expert Member
Jan 4, 2014
512
246
Kwa masikitiko makubwa sana jana usiku wa saa mbili maeneo ya Shekilango Ubungo askari wa kikosi cha barabarani mmoja wapo akiwa amelewa walikuwa na kazi za kuwakamata wenye Bodaboda na wenye magari ambao wametenda makosa na kuwatolesha pesa.

Hakuna aliyeandikiwa faini, walikusanya pesa kwa wakosaji hao mpaka shilingi elfu tano tano huku wakiwa wakali kwa kuwatishia wasipitoa pesa watawapiga faini ya elfu 60 hata kwa kosa la faini ya elfu 30.

Askari hao walienda mbali zaidi kwa kuwatishia kuwaweka mahabusu hata wale waliodai waandikiwe faini ili wasipotezewe muda ambapo waliwaweka kwa muda mrefu bila kuwaandikia ili watoe pesa na kuwaachilia,aidha mmoja wa askari hao ambao hawakuwa na namba za kijeshi kwenye sare zao alikuwa anaanza kudai elfu 20 na kushuka hadi elfu 5 bila ya aibu.

Tunawaomba sana viongozi wao wawafuatilie hususani walioingia kazini maeneo hayo hapo jana siku ya Jumatano tar 15 May 2019 walifanya kitendo cha aibu sana.

Tunawaomba ma RTO 'na ma DTO kuweka namba zao wazi ili yakitokea waweze kupigiwa.
 
...Hapo ndipo majirani zetu wa Kenya ndipo wanapotuzidi!
Hivi wote mliosimamishwa hapo na mnaona kabisa kuwa jamaa wanavunja sheria ikiwemo kilevi wakiwa kazini na sare za kazi, mlishindwa kuamua kufanya tukio na kuwabeba msobe msobe hadi kituo cha Polisi kilicho karibu??
Napenda kuamini kuwa njiani kuelekea Polisi waheshimiwa hao wenyewe wangewaomba Msamaha...
 
Boda nazo yapasa kufuata sheria sio kila cku matatizo. Ndio maaana daily mnatoa hela za kiwi anyway kila mtumishi atakula kwenye madhabahu yake
 
Kama ni kweli naomba utuwekee Picha za hao maskari.
kama huna itakuwa ni majungu...
 
Kwa masikitiko makubwa sana jana usiku wa saa mbili maeneo ya Shekilango Ubungo askari wa kikosi cha barabarani mmoja wapo akiwa amelewa walikuwa na kazi za kuwakamata wenye Bodaboda na wenye magari ambao wametenda makosa na kuwatolesha pesa.

Hakuna aliyeandikiwa faini, walikusanya pesa kwa wakosaji hao mpaka shilingi elfu tano tano huku wakiwa wakali kwa kuwatishia wasipitoa pesa watawapiga faini ya elfu 60 hata kwa kosa la faini ya elfu 30.

Askari hao walienda mbali zaidi kwa kuwatishia kuwaweka mahabusu hata wale waliodai waandikiwe faini ili wasipotezewe muda ambapo waliwaweka kwa muda mrefu bila kuwaandikia ili watoe pesa na kuwaachilia,aidha mmoja wa askari hao ambao hawakuwa na namba za kijeshi kwenye sare zao alikuwa anaanza kudai elfu 20 na kushuka hadi elfu 5 bila ya aibu.

Tunawaomba sana viongozi wao wawafuatilie hususani walioingia kazini maeneo hayo hapo jana siku ya Jumatano tar 15 May 2019 walifanya kitendo cha aibu sana.

Tunawaomba ma RTO 'na ma DTO kuweka namba zao wazi ili yakitokea waweze kupigiwa.

Vijana acheni roho ya kimaskini, kwahiyo akiwaandikia 30,000.00 mtafurahi wakati mwingine kazi inatakiwa ikunufaishe, huyo polisi siku akistaafu mtaanza kumcheka kwa namna ambavy maisha yake yatakuwa ya hali ya chini. Kuna ndugu yangu kaastafu miaka 3 iliyopita alikuwa uhamiaji kwakweli anatia huruma.
 
Mimi natoa tu bora efu 5 kuliko efu 30...
Mana ninavojua mimi traffic kama hujafanya kosa na gari imetimia ngumu sana kukuandikia faini..
Sasa unakuta dereva ushakosea unasaidiwa ubakiwe na chenji ya wese efu 25 unakuja kuleta unoko huku
 
Wanaume wa Dar hao wewe hujui?
...Hapo ndipo majirani zetu wa Kenya ndipo wanapotuzidi!
Hivi wote mliosimamishwa hapo na mnaona kabisa kuwa jamaa wanavunja sheria ikiwemo kilevi wakiwa kazini na sare za kazi, mlishindwa kuamua kufanya tukio na kuwabeba msobe msobe hadi kituo cha Polisi kilicho karibu??
Napenda kuamini kuwa njiani kuelekea Polisi waheshimiwa hao wenyewe wangewaomba Msamaha...
 
Wewe unataka wakahonge nini? Hujui Eid Mubarak inakaribia?
Waache wachukue usiwasumbue hao ndio walinzi wa amani!!)
 
Ukiambiwa uchague kati ya kuandikiwa faini ya 30,000/= na kutoa 5,000/= ya kubrashia viatu utachagua ipi?
 
...Hapo ndipo majirani zetu wa Kenya ndipo wanapotuzidi!
Hivi wote mliosimamishwa hapo na mnaona kabisa kuwa jamaa wanavunja sheria ikiwemo kilevi wakiwa kazini na sare za kazi, mlishindwa kuamua kufanya tukio na kuwabeba msobe msobe hadi kituo cha Polisi kilicho karibu??
Napenda kuamini kuwa njiani kuelekea Polisi waheshimiwa hao wenyewe wangewaomba Msamaha...
Huyu mtoa mada analeta majungu tu.
 
Hivi inawezekana raia akajipigisha zile nguo na vikoti vya reflector akapiga hela naomba kuuliza usiku unaruhusiwa kuomba kitambulisho cha traffic ili kujiridhisha usawa umekaba koo inawezekana wajanja wanajichomeka alafu usiku ni vigumu kuona namba za kwenye vazi la askari.
 
Vijana acheni roho ya kimaskini, kwahiyo akiwaandikia 30,000.00 mtafurahi wakati mwingine kazi inatakiwa ikunufaishe, huyo polisi siku akistaafu mtaanza kumcheka kwa namna ambavy maisha yake yatakuwa ya hali ya chini. Kuna ndugu yangu kaastafu miaka 3 iliyopita alikuwa uhamiaji kwakweli anatia huruma.
Jambo afande
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom