Trafic jamani punguza kupokea hongo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Trafic jamani punguza kupokea hongo

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Calist, Nov 26, 2011.

 1. C

  Calist Senior Member

  #1
  Nov 26, 2011
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 131
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hapa niko jirani na kituo cha trafic naendelea na shughuli zangu na trafic kama kawaida wanaendelea na kazi yao ya kukusanya hongo. Kila gari linalopita linasimama konda au tingo anatoa kitu kidogo safari inaendelea, magari mengine ni mabovu hata kwa kuyaangalia tu lakini wakishatoa wanaruhusiwa tu. Kwa mtindo huu ajari zitakwisha ? Sijui nichukue video yao kama J. Muro ingawa haisaidii kitu maana inaonekana hata wakubwa hapa wana mgao wao, kuwa wazalendo jamani.
   
 2. Sokwe Mjanja

  Sokwe Mjanja JF-Expert Member

  #2
  Nov 26, 2011
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 579
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Uko wapi?
   
 3. vipik2

  vipik2 JF-Expert Member

  #3
  Nov 26, 2011
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 1,175
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Yupo barabarani..., Ukweli tutawalaumu bure kwani hali ya maisha ni mbaya kwa kila mtanzania na tumeoza kuanzia kichwa hadi vidoleni, hiyo rushwa ndugu yangu huenda kugawanwa na wakubwa zao na wasipofanya hivyo wako hatarini kupelekwa Mtimbira, kawaulize pale Chalinze walivyokosea tu wote wakapigwa PI ktk barabara maarufu
   
 4. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #4
  Nov 26, 2011
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,150
  Likes Received: 2,110
  Trophy Points: 280
  Rushwa kuiondoa siyo jitihada za traffic. Umejiuliza kwa nini mtu anatoka na kushawishi kutoa RUSHWA? kuna tatizo katika mifumo yetu. Kama sumatra wamemupa route, kama TRA wamemupa lesseni ya biashara na gari lake bovu, unadhani polisi ataanzia wapi kukomesha hali hiyo? hizi taasisi zote, ni wehu tu, masaburi @ work every nukta, usitegemee ajali kuisha.

  kuna OCD mmoja alisimamia sheria ya kupiga disco kusini mwa tanzania. aliyekuwa anapiga disco, alikuwa ni KOMBA. Mda ulipofika OCD akaeenda kumkumbusha mwisho wa makubaliano yetu 6 usiku, watu wakasema tunataka hadi majogoo, komba akamsihi amruhusu, OCD akagoma, komba akamwambia ukininyima ruhusa ya kukesha, iko sehemu nitaruhusiwa. Komba akapiga simu, akaruhusiwa na yule OCD kuamriwa kumlinda komba mpaka majogoo. Kulipokucha, OCD alifatwa na RPC wake kuwa anaitwa kwa mkuu wa mkoa, alipigwa transfer na kushushwa cheo hadi mshauri wa mgambo wilaya.

  walioshikilia system wakiwa waovu, hata wanaoisaidia sysytem kuendelea kuwepo watakuwa waovu, hautapata msafi hata siku moja
   
 5. G

  Gurtu JF-Expert Member

  #5
  Nov 26, 2011
  Joined: May 15, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Kwa kweli habari ndiyo hiyo. Mkuu wa kaya ndiyo bosi wa mabosi wanaosimamia hongo hizo. Hao wadogo wanapochukua hongo hupeleka mgawo kwa walioko juu. Angalia ngazi yao ya madaraka na vivyo hivyo hongo hizo huwafikia huko huko. Hii ni Tanzania na lazima ulielewe hilo. Vinginevyo kama una uchungu na nchi hii basi tukiitisha maandamano ya kuwaondoa madarakani hao wanaosimamia hongo/rushwa basi ujitokeze.
   
 6. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #6
  Nov 26, 2011
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,150
  Likes Received: 2,110
  Trophy Points: 280
  Hakika, kuna mdau mmoja katoka BOTSWANA kimatembezi, alifanikiwa kuongea na askari wa cheo cha chini kabisa kule, akambiwa pesa anayolipwa askari wa chini kabisa, ambapo pesa zile kwa pesa yetu ni sawa na 1,800,000/- sasa katika mazingira haya, nani atachukua rushwa? halafu kiburi cha botswana ni diamond na gold pekee, ambapo mwekezaji 50% ya mrahaba huku akiwajibika kulipia vitu vingine kama kodi, lesseni na mambo kibao.

  Tanzania tuna zaidi yao karibia mara 100. tuna gold, diamond, uranium, coal, tanzanite, rubi, chuma na mengine siyajui jina, lakini mrahaba wetu asilimia 1-5% matokeo yake mishahara kwa watumishi wa umaa 150,000/-300,000/= kwa wale wenye kataaluma ka shahada.

  Katika mazingira haya, ukiangalia na mfumuko wa bei, mtu mwenye familia ataishije? akiwa na nafasi ya kupokea mlungula, lazima atapokea.

  waliopewa uongozi wakiwa waovu, usitegemee watendaji wa chini kuwa safi, ni rushwa kwenda mbele ili mwezi uishe salama

   
 7. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #7
  Nov 26, 2011
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,150
  Likes Received: 2,110
  Trophy Points: 280

  inahitaji uelimishaji wa hali ya juu sana. Jana nilikuwa na dereva tax, alikuwa ananipeleka hospitali, wife anaumwa, yeye akaanza kuwaponda waarabu eti wamezidi. Mwisho akasema, mie siwezi kuandamana eti nadai fulani atoke, aingie fulani kwani wote lao moja.

  nilimjibu nikamwambia siku ukielewa siasa ni nini na kazi yake ni nini, utaingia mtaani kudai uhuru wako. Babu zetu hawakuwa wajinga kuwatimua wakoloni pamoja na kuwa na risasi za moto, Marekani leo kila mtu anatamani kwenda, kwa kuwa Martin Luther king jr, alikubali kufa kwa kuandaa mazingira ya hawa wanaokimbila leo marekani waende bila kubaguliwa. Ukiwa mbinafsi, huwezi kushiriki, lakini wanao watakuja kukuhoji, umetuachia nini cha maana zaidi ya mikataba mibovu, maisha duni, kusoma kwenyewe shule za kata mwl. mmoja na mtatizo kibao, atakulaumu sana.

  Kidogo akaanza kunielewa

   
 8. C

  Calist Senior Member

  #8
  Nov 26, 2011
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 131
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Niko Iringa au unataka kujua Iringa sehemu gani? Sasa hivi ndio anapokea mkwanja kwenye bus moja mkweche unatoka kijijini umeshona abiria kibao. Kama vile walishapangiana kiasi maana wafika wanatoa sent wanaondoka hakuna kuulizana.
   
 9. C

  Calist Senior Member

  #9
  Nov 26, 2011
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 131
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Cha ajabu wakiona DFP, ST, au gari ya mwarabu wanaangalia pembeni, kama hii kusanya kusanya ingekuwa haiendi hadi kwa wakubwa hawa wadogo wangekuwa wanakamatwa kirahisi muno, we kamanda wa Iringa hebu jaribu kushtukiza sasa hivi halafu wakague hao walioko barabara zinazoingia Iringa mjini uone kila mmoja ana shs ngani na kazipata wapi, saa hizi.
   
 10. Ngisibara

  Ngisibara JF-Expert Member

  #10
  Nov 26, 2011
  Joined: Jan 2, 2009
  Messages: 2,083
  Likes Received: 431
  Trophy Points: 180
  Ukitaka utamu wa Askari hawa na wasikupe shida toka Bukoba hadi Songea wee tafuta na nunua pesa bandia za Tsh 10,000/=, kila wakikusimamisha toa aione kidogo halafu ikunjekunje kwa sanaaaa halafu naye ataipokea haraka haraka na kuificha tena walivyo huwa hawapendi wenzie wajue kuwa hapo imetoka u..ten ili baadaye awazime, jioni wee umeshafika safari yako yeye anafunga mahesabu au anaagiza bia basi hapo ndio msala unakuwa wake
   
 11. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #11
  Nov 26, 2011
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,150
  Likes Received: 2,110
  Trophy Points: 280
  hayo ni magari ya serikali, haywezi kukamatwa labda kuwa na ulazima wa kuyakamta. Halfu mengi hayana makosa kama yalivyo magari ya kiraia
   
 12. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #12
  Nov 26, 2011
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,150
  Likes Received: 2,110
  Trophy Points: 280
  kuna wengine wana machale, watakukamata nazo halafu ubaki na kesi ya kumiliki noti bandia. Kuna jamaa alifanya kama ulivyosema, alaikuwa ana noti za 6,000,000/-, kwalambisa askari wengi alipofika mahali fulani akashitukiwa, mpaka sasa yko gerezani. ni mshikaji namfahamu sana
   
 13. m

  mjaumbute Member

  #13
  Nov 26, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 41
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hatari hatari zaidi ya umeme

   
Loading...