Traffic University

Call me GHOST

Member
Jan 18, 2019
53
95
Hi Socrates,

Wengi wetu tumekuwa tukishindwa kusoma vitabu kwa kigezo cha kukosa muda kutokana na kuwa busy na utafutaji n.k, Je nkisema sio kweli nitakuwa nakosea..!?

Twende pamoja, Najua wengi wetu kila asubuhi tunawahi makazini au kwenye mihangaiko na kurudi jioni na pia wengi wetu kulingana na mazingira tunayofanyia kazi au shughuli zetu inatubidi tupande daladala au hata wengine kutumia usafiri binafsi ili kufika kazini kwa urahisi zaidi. Je unapokuwa upo kwenye usafiri unaelekea kwenye shughuli zako unautumiaje huo muda..!?

Kwa wastani kila siku utatumia muda wa nusu saa mpaka lisaa limoja ukiwa kwenye daladala wakati wa kwenda kazini asubuhi na wakati wa kurudi na pengine unaweza kutumia zaidi ya lisaa kutokana na foleni. Hivyo basi katika huu muda unaweza tumia earphones kusikiliza audiobooks au podcast mbalimbali ndani ya wiki utakuwa tayari umeshatengeneza muda wa ziada usiopungua masaa 15 ambayo utakuwa ukiyatumia tu kusikiliza audiobooks vp ndani ya miezi mitatu utakuwa umesikiliza vitabu vingapi..!?

Je bado jibu lako litakuwa vile vile kwamba hauna muda..!?

Law of Forced Efficiency inasema “There is never enough time to do everything, but there is always enough time to do the most important things."

Tafsiri isiyo rasmi inasema " Hatuwezi kuwa na muda wa kufanya kila kitu lakini siku zote lazima tutapata muda wa kuyafanya yale mambo yenye umuhimu sana kwetu"

Fanya usomaji/kujifunza kuwa sehemu ya ratiba zako za kila siku kwa kuupa umuhimu kwenye ratiba zako.

Mwaka 1991, Utafiti uliofanywa katika Chuo kikuu cha Southern California ulibainisha kwamba Muda ambao watu wanautumia kwenye magari asubuhi kwenda ofisini ukiujumlisha ndani ya miaka mitano ni sawa sawa na muda unaohitajika kwa mtu kumaliza degree chuo kikuu ndani ya miaka mitatu

Ndio maana kuna kitu kinaitwa 'Traffic University' ikiwa na maana kwamba unaweza kujifunza wakati ukiwa njiani kuelekea/kutoka kazini kwa kusikiliza maarifa tofauti tofauti kwa njia ya sauti ikiwepo kusikiliza audiobooks, podcast n.k

Fanya chombo chako cha usafiri(daladala/usafiri binafsi) kuwa 'Traffic University' kwa kujifunza kupitia kusikiliza audiobooks au podcast mbalimbali zenye maarifa yatakayokubadilisha fikra na mtazamo wako kila siku kuliko kuuacha huo muda upotee tu bure.

Mwandishi Robin Sharma anasema "The hours that ordinary people waste, extraordinary people leverage" ikiwa na tafsiri ya " Muda ambao unaupoteza bure wengine wanautumia muda huo huo kufanya mambo yanayowajenga"

Kwanini usiutumie huo muda kusikiliza audiobooks, podcast au pengine kitu chochote chenye manufaa kwako kwa lengo la kukupanua fikra na kukuongezea maarifa..!?

Asanteni,

Ghost..
IMG_20210620_180942.jpg
 
Back
Top Bottom