Ngigana
JF-Expert Member
- Apr 16, 2010
- 2,108
- 1,449
Taarifa kwa kamanda wa usalama barabarani. Traffic Police wa Same, na leo walikuwa na gari lenye namba za usajili T353 BAJ wanawatoza faini madereva bila kuwa EFD risiti. Mheshimiwa rais ametuagiza kuwa ni wajibu wa kila anayelipa kodi au faini apewe risit ya EFD. Wao leo saa za jioni kati ya saa 10 -12 walikuwa wanawatoza madereza faini kwa makosa yasiyoeleweka na kuwapa risiti za kuandikwa kwa mkono. Tena wengine walikuwa wamelewa. Huu ni wizi na pia utovu wa nidhamu kazini. Hawa wachunguzwe ili kutoikosesha serikali mapato halali. Lakini pia tabia ya ulevi wakiwa wamevaa sare za kiaskari ni fedheha kwa jeshi la polisi, wamulikwe