Traffic Police Arusha (Omba Omba) ni Mafisadi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Traffic Police Arusha (Omba Omba) ni Mafisadi?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by PauliMasao, May 10, 2012.

 1. P

  PauliMasao JF-Expert Member

  #1
  May 10, 2012
  Joined: Nov 26, 2007
  Messages: 286
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mimi nimechoka na hawa traffic police hapa Arusha. Baadala ya kuongoza magari au kuangalia wavunja sheria barabarani wao hujikusanya sehemu mbali mbali ya jiji letu, kazi kubwa ni kuomba pesa. Unasimamishwa halafu wanajifanya kucheki gari wakiona hamna kitu wanakuomba japo buku tano ya lunch. Sasa kwa hesabu za haraka haraka, traffic police mmoja akisimamisha magari ishirini kwa siku, anweza kujipatia shilingi laki moja kwa siku. Je huu sio ufisadi?
   
 2. seniorgeek

  seniorgeek JF-Expert Member

  #2
  May 10, 2012
  Joined: Sep 18, 2008
  Messages: 500
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Wakikuomba buku tano, basi watakua wamekuona wewe sharo.
  Buku buku natoaga mara moja moja kwa roho safi.
   
 3. Mentor

  Mentor JF-Expert Member

  #3
  May 10, 2012
  Joined: Oct 14, 2008
  Messages: 18,647
  Likes Received: 8,207
  Trophy Points: 280
  kumbe wanaomba tu..nlidhani wanakubambikia kesi..apo ngoma droo, ukiombwa si lazima utoe!
   
 4. m

  massai JF-Expert Member

  #4
  May 10, 2012
  Joined: May 2, 2011
  Messages: 655
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  hivi na sisi wenye magari tukaombe wapi?kama ni hayo magari hata wao wanayo tena sio moja au mawili,inakera sana wametugeuza mtambo wao wa kutengeneza hela
   
 5. O

  OMEGA JF-Expert Member

  #5
  May 10, 2012
  Joined: Jul 12, 2011
  Messages: 671
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 60
  We unadhani mshahara wa laki na nusu ataishije jiji kama Arusha.
   
 6. Ndallo

  Ndallo JF-Expert Member

  #6
  May 10, 2012
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 7,127
  Likes Received: 1,083
  Trophy Points: 280
  Aisee kweli wamezidi kuomba juzi kuna mmoja kanisimamisha nikamwambia ndio asubuhi hii nakwenda kutafuta, hakunielewa nikamwambia hapa nilipo nina Buku 2 tu! Akaniambia aisee tugawane hata Bukubuku angalau nikatoe Lock! Nilimuonea huruma sana na ukizingatia baridi iliyopo Arusha sasa hivi.
   
 7. P

  PauliMasao JF-Expert Member

  #7
  May 10, 2012
  Joined: Nov 26, 2007
  Messages: 286
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kwa hiyo hawa hawana tofauti na omba omba wengine mitaani
   
 8. P

  PauliMasao JF-Expert Member

  #8
  May 10, 2012
  Joined: Nov 26, 2007
  Messages: 286
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kuna mshahara unaotosha kweli?
   
 9. P

  PauliMasao JF-Expert Member

  #9
  May 10, 2012
  Joined: Nov 26, 2007
  Messages: 286
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Nasikia wengine wana dala dala mbili au tatu
   
 10. seniorgeek

  seniorgeek JF-Expert Member

  #10
  May 11, 2012
  Joined: Sep 18, 2008
  Messages: 500
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Hawana tofauti na wanaogongea pombe bar au club (kama unanisoma)
   
 11. broken ages

  broken ages Senior Member

  #11
  May 11, 2012
  Joined: Mar 23, 2012
  Messages: 160
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  Kinachoudhi zaidi ni pale wanapokutamkia ya kuwa gari haiwezi kukosa kosa ikikaguliwa kwa hiyo wewe nipe tu changu mapema ama nikukague ukalipe notification kuna kipindi nilitembelea Arusha nikakumbana na hilo janga ikabidi nimpe elfu tano anasema haitoshi ongeza maana tuko watatu haigawanyiki ikabidi niongeze elfu ili niondokane na adha ya kuvurigiwa ratiba yngu ya siku hiyo
   
Loading...