"Traffic" Nunua gari yako upande

"Traffic" Nunua gari yako upande

Mkuu, yule mtu aliyetoa ile kauli nina uhakika kuna mambo yaliyomkuta. Niliwahi kumpa lift askari wa usalama barabara. Baada ya kukaa na tumekwenda kama mita mia mbili akaanza kusema lakini mheshimiwa taa yako moja imevunjika na hilo ni kosa. Sikumjibu. Nilichofanya ni kusimama sehemu karibu na kituo cha daladala na kumuuliza, ulinisimamisha kwa kwa makosa yangu au lifti? Wakati anashangaa nikamwambia shuka kwenye kwenye gari yangu. Akashuka nikaendelea na safari yangu.

Tatizo nao wanakuwaga wanajidai ni kama wanaishi dunia yao. Mtu akupe lift uanze tena kukosoa. Anyway nimejifunza kitu mkuu
 
Ngoja nikumegee siri kuna mmoja anasimama (panahifadhiwa kwa sasa) kwa kuwa mimi si msemaji wa familia yake...ila for sure ukimpa ride hutojutia muda wako...in fact ana faa sana kwa matumizi binafsi!

Mkuu mtaje kwa faida ya wanaJF wakaprove unachokiongea ukizingatia ameutesa moyo wako kwa muda mrefu.
 
Haaa nyie hamjui traffic police walivyo washenzi, mimi simpi lift labda aniombe, kuna siku nilikuwa natoka bagamoyo Polisi aliomba lift nikampa lakin mle ndani tulikuwa na jamaa yangu tunakula samaki na mazagazaga mengine tukamnyima shenzi

Hahaha na Samaki alitaka tena, hahaa trafik wanajidhalilisha sana sometym.
 
Nani kakwambia ulaya hawapeani lift? Nchi zilizoendelea gari ni kitu cha kawaida sana, ukikuta mfanyakazi anaenda kazini kwa mguu ujue ameamua, wengi wanatumia usafiri wa umma na baiskeli kuepuka foleni na kupunguza matumizi yasiyo ya msingi. Sisi gari ni kama ng'ombe kwa mmasai, ni alama ya wealth, mtu akiwa na funguo ya gari hataki hata kuitia mfukoni, full time mkononi na masimu yake mawilimawili kama hana mifuko!

Vijana kazi tunayo,ukishakuwa na gari lazima ujionyeshe tena kwa jinsia tofauti ndiyo inanoga:.......God forbide
 
Wapo ambao wanafanya kazi zao kwa haki na wapo waoneaji poa

Mimi sijaona wa namna hiyo. Kuna siku nilikuwa Ipogolo napandisha Iringa mjini, mvua inanyesha nikamwona traffic police analowa, nikaona isiwe taabu ngoja nimpe lift. Cha ajabu anakaa tu ananinyuka swali " hii ni aina gani ya gari" nikajibu, si akaanza kuipondea! From there mimi na wao maji na mafuta.
 
Hahahaa, kwa hiyo wewe ili muendane na mtu lazima akusifie? We unatoka kule zinakoliwa senene kwa wiingi:heh:?
 
Mkuu mtaje kwa faida ya wanaJF wakaprove unachokiongea ukizingatia ameutesa moyo wako kwa muda mrefu.

Wakishafaidika wengi hii sio faida tena bali hasara....ni WP 8385 kama akipata muda wa kupitia hapa atambue wazi ''sisi'' wanaume tusiofungamana na upande wowote tuko tayari kufanya smooth crime barabarani mbele yake ili atupeleke kituoni na tukifika tutaandika ombi maalum kwa mkuu wa kituo ili yeye(aliyetupeleka) atulinde walau tutoke tukiwa raia wema!
 
Wakishafaidika wengi hii sio faida tena bali hasara....ni WP 8383 kama akipata muda wa kupitia hapa atambue wazi ''sisi'' wanaume tusiofungamana na upande wowote tuko tayari kufanya smooth crime barabarani mbele yake ili atupeleke kituoni na tukifika tutaandika ombi maalum kwa mkuu wa kituo ili yeye(aliyetupeleka) atulinde walau tutoke tukiwa raia wema!

Ujumbe mzito sana huu mkuu. I wish WP 8383 angepita huku.
 
Haaa nyie hamjui traffic police walivyo washenzi, mimi simpi lift labda aniombe, kuna siku nilikuwa natoka bagamoyo Polisi aliomba lift nikampa lakin mle ndani tulikuwa na jamaa yangu tunakula samaki na mazagazaga mengine tukamnyima shenzi

Sasa ushenzi wake ni upi?
Kumyima samaki au lifti yako unaona umemnyima kitu kikubwa sana??
Usiwape lifti, wapo watakaowabeba.
 
Back
Top Bottom